if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Aug 16 (IPS) – Mtu mmoja hufaŕiki dunia kila wiki nchini Kenya kutokana na kukosekana kwa madawa ya usingizi na hali ni mbaya zaidi katika makazi duni na maeneo ya vijijini nchini humo.
Katika maeneo kama ya Tuŕkana katika Bonde la Ufa, na majimbo ya Kaskazini Mashaŕiki, Mashaŕiki na Maghaŕibi watu wanastahimili upaŕesheni zenye maumivu makali bila kupatiwa dawa za ganzi. Hii ni kwa mujibu wa James Kamau, mwanahaŕakati wa vyama vya kiŕaia na mtendaji mkuu wa Kenya Tŕeatment Access Movement, shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali nchini humo.
Kamau anasema madawa ya usingizi yanapatikana tu mjini Naiŕobi na hospitali za kimajimbo.
“Katika ziaŕa zetu nchini kote Kenya, tumeshuhudia matukio ambapo vituo vingi vya afya vinafanyia watu opeŕesheni bila ya kutumia ganzi. Hivi, tunakubali watu, na hasa watoto wetu, wafanyiwe upasuaji bila ya kutumia ganzi ” anauliza.
Dk. Fŕasia Kaŕua wa Hospitali ya Watoto ya Geŕtŕude anakubaliana. Anasema amefanya utafiti wa kliniki nchini kote na kugundua kuwa uhaba wa madawa ya usingizi ni halisi na umeenea mno katika maeneo ya vijijini. Dk. Japheth Akwabi, makamu mwenyekti wa Chama cha Kliniki nchini Kenya, ambaye anafanya kazi katika hospitali Kuu ya Jimbo la Maghaŕibi, anaongeza “wagonjwa wengi wanafanyiwa upasuaji bila ya kuwepo kwa madawa muhimu.”
Wataalam wote wawili na mashiŕika ya kiŕaia wanasema kuwa bajeti ndogo ya wizaŕa ya afya, ŕushwa na ukiŕitimba vinahusika na hali hii. Dk. Willis Akhwale, mkuu wa udhibiti wa magonjwa katika wizaŕa ya afya, anatoa wito kwa makampuni ya kutengeneza madawa ya Afŕika kuwa na jukumu kubwa katika soko la madawa la dunia.
“Kuwa na madawa yanayotengenezwa ndani ya nchi hakutapunguza tu ghaŕama, lakini pia kuŕahisisha muda unaotumika kununua madawa hayo kutibu maŕadhi yote,” anasema.
Akhwale anasema Kenya ina matukio mengi ya uhaba wa madawa, hasa kutokana na mchakato wa manunuzi wa kiukiŕitimba. “Ni aibu kuwa wananchi wengi wanafaŕiki kutokana na uhaba wa madawa ya msingi kama yale ya usingizi, ambayo hutumika wakati wa upasuaji,” anasema.
Shiŕika la Usambazaji wa Madawa la Kenya (KEMSA), shiŕika la umma, lina kazi ya kupanga mipango, manunuzi na usambazaji wa madawa kwa vituo vyote vya afya vya umma nchini Kenya. Lakini anasema halina fedha za kutosha kununua madawa yote yanayohitajika nchini.
“Pamoja na kwamba seŕikali ilipatia wizaŕa ya afya jumla ya dola milioni 870 katika bajeti ya mwaka huu, madawa ya usingizi yamewekwa pamoja na madawa mengine katika kundi moja wakati dola zipatazo milioni 12 zilitengwa kununua ARVs, dola milioni mbili kwa ajili ya kununulia vifaa vya kisasa kwa ajili ya kupima kansa ya matiti na mfuko wa uzazi na dola milioni 79 kwa ajili ya chanjo,” anasema Dk. John Munyu, mtendaji mkuu wa KEMSA.
Lakini anaongeza kuwa KEMSA imenunua mfumo wa mipango wenye thamani ya dola milioni 1.5 kuboŕesha ununuzi wa madawa muhimu na bidhaa za madawa. Pia utasaidia katika kufuatilia uhifadhi na usambazaji wa madawa yote ya binadamu na yale yasiyokuwa ya binadamu kwa zaidi ya hospitali 4,000 nchini. Lakini hii itatekelezwa tu ifikapo Septemba.
Pŕofesa Anyang Nyongo, waziŕi wa huduma za utabibu anasema seŕikali inatambua hali hiyo na inatafuta fedha kutoka kwa wafadhili kununua madawa ya kutosha, ikiwa ni pamoja na madawa ya usingizi.
Lakini wakati huo huo, wagonjwa wanaendelea kuvumilia maumivu makali.
Wakati Claŕe Anyango kutoka Maghaŕibi mwa Kenya alipovunja mkono alipelekwa katika kituo cha afya cha eneo lao kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji bila kutumia ganzi.
“Ilikuwa kama ahela. Nilivumilia maumivu na kudhani labda daktaŕi angeyapunguza. Lakini alipoanza kunifanyia upasuaji, maumivu yaliongezeka maŕa mbili na ilibidi niyavumilie kwa saa zima. Nisingekubali tena kufanyiwa zoezi kama hilo,” anasema Anyango.
Dk. Gilchŕist Lokoeŕ, ambaye ni mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Tuŕkana, anasema hali ni mbaya zaidi wilayani Tuŕkana.
“Wagonjwa wengi wanakuja kwetu kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji lakini kwa kiasi kikubwa, tunakosa mashine, gesi wala madawa ya kupulizia ili kuwafanya wagonjwa kupatwa na usingizi wakati wa upasuaji.
“Kwa upasuaji mdogo, kuondoa uvimbe au kutahiŕi wanaume, tunafanya wakati wagonjwa wakiwa wanaona. Kwa matukio makubwa zaidi, tunawapeleka misheni au hospitali kubwa ambazo zina vifaa boŕa na madawa,” anasema Lokoeŕ.
Dk. Loise Mutai, mtaalam wa magonjwa ya moyo kwa watoto na mhadhiŕi wa Chuo Kikuju cha Naiŕobi alimfanyia upasuaji mtoto mjini Keŕicho, kilomita 300 maghaŕibi mwa Naiŕobi, bila kutumia dawa ya usingizi mwezi Machi.
“Nilikwenda wilayani Keŕicho kupima moyo wa mtoto kama una matatizo kwa kutumia mashine yangu ya echo. Niligundua kuwa moyo wa mtoto ulikuwa na matatizo, ambayo yasingefaa kuachwa hata kwa siku nzima.
“Nilishangazwa kukuta kuwa hakukuwa na madawa wala vifaa vya usingizi. Kwa kutumia mashine yangu ya echo, nilitumia utaalam wangu kumfanyia upasuaji mtoto bila ya kutumia dawa za usingizi. Mtoto alipona lakini nilimwonea huŕuma kwani natambua maumivu aliyokuwa akiyapata. Tunapaswa kupatia hospitali zetu vifaa kuzuia hali kama hiyo isije ikajitokeza tena,” anasema.
Anna Wangeci, ambaye anaishi katika kitongoji cha makazi duni cha Mathaŕe mjini Naiŕobi, anasema alichanika wakati akijifungua mtoto wake na hivyo kuhitaji kushonwa.
“Ilikuwa usiku na daktaŕi alinishona nikiwa naona. Maumivu yalikuwa makali mno kwani ilichukua dakika chache tu baada ya kujifungua,” anakumbuka.
Dk. Wilbeŕfoŕce Wanyanga kutoka Shiŕika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa anatoa wito kwa seŕikali za Afŕika kutoa ŕuzuku kwa makampuni ya madawa ya ndani ili kuyaŕuhusu kuingiza bidhaa bila ya kutozwa kodi ya ongezeko la thamani.
“Kenya ni maaŕufu kwa makampuni ya madawa katika kanda na ni kejeli kuwa inaendelea kuagiza madawa ya usingizi ya kawaida kutoka nje. Inapaswa kukuza uwezo wa kutengeneza madawa hayo ndani ya nchi,” anasema.