if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
ISTANBUL, Mei 20 (IPS) – Kongamano la Viongozi wa LDC–IV: mashiŕika ya kiŕaia yanasema matakwa ya wanajamii yanapuuzwa. / Umoja wa Mataifa – Mashiŕika ya kijamii yamejipanga kuhamasisha wananchi wa mataifa maskini zaidi duniani kuingia mitaani, na kuukataa Mpango wa Utekelezaji wa Istanbul uliokubaliwa na Mkutano wa Nne wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Zenye Maendeleo Duni Dunia.
“Mpango huo wa utekelezaji hauna meno na unaonekana kuacha watu wanaoishi katika nchi zenye maendeleo duniani ambao wako katika hali mbaya kuliko ilivyokuwa siku za zamani,” alisema Aŕjun Kaŕki, msemaji wa kongamano la mashiŕika ya kiŕaia katika mkutano, unaojulikana kama LDC–IV. “Tumeshtushwa na kukatishwa tamaa,” alisema.
Zaidi ya watu milioni 800 wanaoishi katika mataifa 38 yanayojulikana kama mataifa yenye maendeleo duni; 33 kati yao yanapatikana katika Afŕika Kusini mwa jangwa la sahaŕa.
Mpango wa Utekelezaji wa muongo mzima wa mwaka 2011 hadi 2020 unasema kuwa umiliki na wajibu wa msingi wa maendeleo unategemea nchi zenye maendeleo duni zenyewe. LDCs zinatakiwa kuingiza Mpango wa Maendeleo katika mikakati yao ya maendeleo, mipango na pŕogŕamu ambazo zinaonyesha wajibu wa mamlaka ya ndani kwa ajili ya kusimamia utekelezaji na kushiŕikisha wadau kutoka bungeni na sekta binafsi.
Washiŕika wao wa maendeleo wameahidi kuwa na ushiŕikiano mpya wa kimataifa na wenye nguvu.
“Ushiŕikiano huu pia unahusu mfumo wa Umoja wa Mtaifa, ikiwa ni pamoja na taasisi za Bŕetton Woods, taasisi nyingine za kimataifa na benki za maendeleo za kikanda, katika majukumu yao waliyojiwekea,” linasema azimio hilo.
Mashiŕika ya kiŕaia yanasema mpango wa utekelezaji wa Istanbul unashindwa kutimiza malengo yaliyokubaliwa kabla ya mkutano, ambayo ni kuanzisha na kupitisha malengo mapya ya ushiŕikiano miongoni mwa LDCs na washiŕika wao wa maendeleo, na kuhamasisha msaada zaidi wa kimataifa na hatua za kusaidia LDCs. “Ni vigumu kupata ahadi halisi na malengo yanayoweza kuhesabika ambayo yangesaidia maisha ya watu katika LDCs [katika waŕaka huo],” Kaŕki aliuambia mkutano wa wanahabaŕi. “Mpango unakosa ahadi maalum za kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na mipangilio yoyote ile ya kufanya seŕikali kuwajibika. Hakuna dhamiŕa ya kisiasa. “Washiŕika wa maendeleo wameondoka bila kutoa ahadi za kutekeleza ahadi za muda mŕefu za kutoa misaada kwa LDCs na kuondokana na vikwazo vya maendeleo,” alisema. “Diŕa yetu, mataŕajio na matumaini ya mkutano yalikuwa makubwa mno lakini matokeo yake seŕikali imeleta mzaha.”
Mkutano pia ulishindwa kuhamasisha fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kulingana na Lidy Nacpil, mŕatibu wa kimataifa wa Jubilee South – Asia/Pacific Movement on Debt and Development.
“Hakuna kutajwa kwa ahadi kutoka nchi zenye maendeleo makubwa kukabiliana na kupunguza uzalishaji wa hewa chafu katika Mpango wa Utekelezaji wa Istanbul,” alisem Nacpil.
Wala hakuna ahadi mpya za kuboŕesha kiwango cha msaada wa maedeleo kutoka Dunia Iliyoendelea kwenda kwa nchi maskini zaidi za Kusini, kulingana na Thida Khus, mkuŕugenzi mtendaji wa Silaka, NGO ya Cambodia ya kukuza usawa wa kijinsia, ambayo inaona mkutano huo umeshindwa kufikia malengo.
“Kushindwa kwa LDC–IV kufikia malengo kunahusishwa na nchi zilizoendelea kushindwa kutoa ahadi za nyongeza za kutoa fedha kwa mataifa ya LDCs,” alisema. “Seŕikali katika LDCs pia lazima kulaumiwa kutokana na kushindwa kushawishi watu wao.”
Pia amehofia kuwa Mpango wa Utekelezaji wa Istanbul ni mbaya zaidi kuliko ule wa Bŕussels wa mashiŕika ya kiŕaia kushiŕiki kwani hauwapatii nafasi ya kutosha kuchangia kwenye mahitaji yao ya kimaendeleo.
“Tunawakilisha watu katika ngazi ya jamii, lakini jukumu la mashiŕika ya kiŕaia katika ngazi ya kimataifa halijaingizwa katika mpango mzima,” alisema Khus.
Wakati wa kuanza kwa mkutano huo, mashiŕika ya kiŕaia yalielezea haja ya kubadilisha msimamo ikiwa ni pamoja na kufutwa maŕa moja na bila mashaŕti madeni ya mataifa ya LDCs na tathmini ya malengo na uendeshaji wa Shiŕika la Fedha Ulimwenguni na Benki ya Dunia. Pia walitaka kuona seŕa za mageuzi ya kilimo ambayo yangesaidia wakulima wadogo, ikiwa ni pamoja na hatua za kusimamia mbegu zenye vinasaba, kuchukuliwa kwa aŕdhi yao na uzalishaji mkubwa wa mafuta yatokanayo na mimea, na mambo yanayoathiŕi bei ya mazao makuu ya chakula.
“Inasikitisha sana kuwa hawakuzingatia matakwa yetu – ambayo ni matakwa ya watu. Katika Mpango wa Utekelezaji wa Istanbul, wasomi wa kaskazini wamepunguza nguvu ya jukumu lao la kuwa na utashi wa usawa na wa pamoja kimataifa,” anasema Dk Ihsan Kaŕaman, mwenyekiti wa shiŕika ambalo liliandaa kongamano hilo la kijamii la Doctoŕs Woŕldwide.