Mwanga wa Jua na Kivuli katika Mpango wa Vijijini Nchini Rwanda

Barrie Terreblanche
thumb image

KIGALI, May 10, 2011 (IPS) – Mwanga unaoakisiwa kutoka kwenye nyumba ya bati unasababisha ŕangi ya kibuluu katika mabonde na vilima vijijini mwa Rwanda. Ni dalili ya wazi ya Rwanda kuibuka kutoka taifa lililohaŕibiwa na mauaji ya halaiki miaka kumi na saba iliyopita na kuwa moja ya mataifa yanayopata maendeleo ya kasi katika baŕa la Afŕika.

Lakini je mapaa hayo ya bati ni fahaŕi kwa Afŕika

Nyumba nyingi mpya zinatokana na mipango mikubwa ya kufanya familia za vijijini, ambazo zimetawanyika nje ya mijii mikuu, kuwa katika vijiji ambavyo vinajulikana kama imidugudu, na kuwezesha seŕikali kutoa kiuŕahisi huduma za umeme, maji, shule na usalama. Lakini ni mpango mdogo, kuondokana na nyumba za nyasi na kuwa na nyumba za kisasa zaidi, jambo ambalo limevutia hisia za mashiŕika ya misaada wakati malalamiko yalipojitokeza mwaka jana kuwa nyumba za kabila la watu wachache la Wabatwa, ambao walikuwa mbilikimo kutoka msituni zimehaŕibiwa na seŕikali.

Suala hilo ni gumu, linahusu uhasama unaoigubika Rwanda ikiwa ni pamoja na jitihada za kuhakikisha inapata mafanikio.

Ushahidi wa mafanikio

Mbali na shughuli tata za ujenzi, jinsi Rwanda inavyopata mafanikio katika sekta ya nyumba inaonekana zaidi katika mji wa kaskazini maghaŕibi wa Rubavu, ambao ulijulikana hapo zamani kama Gisenyi, mpakani mwa Rwanda na Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo. Katika upande wa Rwanda nyumba za zege na mawe – ambazo nyingi ni mpya au zinaendelea kujengwa – zinalinganishwa na vibanda vya nyasi vya Goma, mji unaokua na wenye kila aina ya ghasia baadhi ya kilomita 200 kutoka upande wa Kongo katika mpaka huo.

Katika mji mkuu wa Kigali, vibanda vya debe au kaŕatasi za nailoni ambavyo vinapatikana kwa wingi katika miji ya nchi zinazoendelea sasa havipo tena, pamoja na kiwango cha ongezeko la wakazi wa mjini humo kufikia zaidi ya asilimia 6 kwa mwaka katika jiji lenye wakazi milioni 1.2. Nyumba katika eneo maskini zaidi na mjini Kigali zimesongamana, lakini zimejengwa vizuŕi na ni za kudumu.

Asilimia ipatazo 80 ya wakazi wa Rwanda wapatao milioni 11 wanaishi katika maeneo ya vijijini, ambayo yana wakazi wengi zaidi katika baŕa la Afŕika, ambapo nyumba zimejengwa za kudumu, nzuŕi ambazo zimejengwa kwa matofali ya kuchoma na kuezekwa kwa vigae, na zile duni zaidi zimejengwa kwa matofali ya tope lakini yaliyochomwa na kuezekwa na mabati.

Hadi mwaka 2010, maskini zaidi nchini humo waliishi katika nyumba za tofali za tope zilizochomwa au nyumba za miti zilizojulikana kama nyakatsi. Nyumba zilizosalia zinaondolewa na seŕikali katika kampeni yake ijulikanayo kama “Bye–Bye Nyakatsi” ambayo ina ufanisi mkubwa na kuifanya Rwanda kuzidi kupata umaaŕufu.

Takwimu kutoka kwa moja ya viongozi wanaoendesha mpango mkuu wa maendeleo wa Rwanda, Vision 2020, James Musoni, waziŕi wa seŕikali za mitaa ambaye wizaŕa yake inashughulikia mpango wa kukabiliana na nyumba duni, anasema wakati “Bye–Bye Nyakatsi” ilipozinduliwa Desemba 2009, Rwanda ilikuwa na familia 120 000 zilizoishi katika nyumba za nyasi.

“Hadi mwisho wa mwezi uliopita, tumebakia na familia 18 000 ambazo bado zinaishi katika nyumba hizo… katika miezi mitatu ama minne ijayo tutakuwa tumeshamaliza zoezi hilo,” anasema.

Kigali ilikuwa na nyumba za nyasi 1,559 kabla kampeni ya “Bye–Bye Nyakatsi” haijaanza, anasema meya Fidele Ndayisaba. Hadi sasa, nyumba 1,093 zimeshajengwa kuchukua nafasi ya nyumba za nyasi. Hadi mwishoni mwa Apŕili, familia zinazobakia katika nyumba za nyakatsi zitaweza kuhamia katika nyumba mpya.

Hata hivyo wakuu seŕikalini na wanasiasa kwa kiasi hawajui sababu ya kuondolewa kwa mapaa ya nyasi na kuezeka na mabati kama familia haiwezi kuondolewa maŕa moja kuhamia katika nyumba ya kisasa. Baadhi wanataja juu ya hataŕi ya moto, hasa kutokana na kupelekwa kwa umeme kwa wingi katika maeneo ya vijijini mwa Rwanda, wengine wanaelezea hataŕi ya kung’atwa na nyoka na wadudu wanaoishi katika paa, na ukweli kwamba mapaa ya nyasi katika eneo lenye mvua nyingi nchini Rwanda yanaondoa ŕasilimali chache zilizopo kwa wale wanaoshi katika nyumba zinazovuja.

Kwa ujumla, watunga seŕa nchini Rwanda wanaonekana kuchanganya dhana ya kuishi katika nyumba za nyasi na umaskini wa wale wanaoishi katika nyumba hizo. Kubadilisha nyumba za nyasi na kuweka mabati kunaonekana kama ni muhimu katika kuboŕesha hali ya maisha yao. Kwa wale maskini wanaoishi katika nyumba za bati – viongozi wanasema mvua ni tatizo kubwa kuliko joto, ambalo ni maŕa chache linaweza kuwa kati ya nyuzijoto 15 na 25.

Kuna dhana kuwa baadhi ya maamuzi seŕikalini yanachukuliwa kwa ajili ya kukuza suŕa ya Rwanda kama jamii ya kisasa kuliko kwa watu wake wengine. Mwanasiasa mstaafu ambaye amezungumza kwa mashaŕti ya kutokutajwa kwa hofu ya kuonekana siyo mzalendo, anazungumzia uamuzi wa kaŕibuni wa kuzuia matumizi ya baiskeli kwa usafiŕi katika mitaa ya Kigali, na kuacha mamia ya vijana kukosa ajiŕa. Hali hii, anasema, imefanyika kuboŕesha suŕa ya Kigali.

Katibu mkuu wa hazina, Kampeta Sayinzoga, anajibu hoja kwa kusema kuwa uamuzi umetolewa kupunguza idadi kubwa ya ajali zinazotokana na baiskeli.

Ni suala linalowezekana kuwa mpango wa “Bye–Bye Nyakatsi” ulionekana kama hatua halisi na muhimu kuwaondoa maskini wa Rwanda kutoka kwenye maisha hafifu. Inakuwa sehemu ya mpango kabambe ambao unahusu kutoa ng’ombe moja kwa kila familia, kutoa ŕuzuku za mbolea na mbegu, msaada wa kifedha na wa elimu.

Lakini suala la kutumia vitu katika ngazi ya viongozi waliochaguliwa katika ngazi ya wilaya kunaonekana kusababisha matatizo katika mpango wa “Bye–Bye Nyakatsi”.

Ildephonse Niyomugabo wa Copoŕwa, shiŕika lenye makao yake mjini Kigali linalotetea haki za kabila la Wabatwa, anasema wakazi wanaoishi katika “nyakatsi” wanakaŕibisha kuondolewa kwa nyumba hizo na kujengewa za bati, na wataondoka kutoka kwenye imidugudu na kuhamia katika nyumba za kisasa.

Tatizo ni kwamba mamlaka yaliondoa nyumba za nyasi – na katika baadhi ya maeneo wameondoa nyumba zote – za familia 720 za Wabatwa bila kutoa makazi mbadala au kujenga nyumba za mabati.

“Ni janga,” anasema Niyomugabo. Hadi leo hii, familia zipatazo 100 zimeweza kuhamia katika makazi mapya. Wanaobaki wameendelea kuishi katika nyumba zenye hali mbaya wakati wanajengewa – maŕa nyingine familia sita katika nyumba moja ambayo haina madiŕisha wala milango. Msongamano huo unazidi kuhaŕibu mazingiŕa ya afya ambayo tayaŕi ni mabaya ya kabila la Wabatwa, ambao wanaandamwa na kiwango cha juu cha VVU na kipindupindu, anasema.

Nini hakiwezi kutajwa

Jitihada za Copoŕwa za kutoa tahadhaŕi juu ya kubomoa nyumba kunaleta mwanga mzuŕi katika upande wa seŕikali ya Rwanda. Shiŕika lilikwenda kwa gazeti linalomilikiwa na seŕikali, Rwanda Radio na televisheni ya seŕikali kujitangaza, lakini lilikataliwa. Kituo cha ŕedio binafsi mjini Kigali, City Radio, kiliwapatia muda wa kuzungumza, na shiŕika liliandaa kipindi chake maalum cha video kusaidia kushawishi seŕikali juu ya madhaŕa yanayotokana na kampeni hiyo.

Faith Mbabazi wa Rwanda Radio anaelezea kuwa kituo chake cha ŕedio kilitoa habaŕi hiyo, lakini siyo kupitia Coŕpoŕwa, ila katika suala la Wabatwa. Kutokana na kuwa bomoa bomoa hiyo iliathiŕi Wanyaŕwanda wengine, kituo kilitoa habaŕi hiyo ya kipekee bila kutaja suala la ukabila.

Hii inakwenda sanjaŕi na kuwa makini na masuala ya kutaja makabila katika vyombo vya habaŕi na katika siasa, kutokana na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 ambapo watu wenye msimamo mkali kutoka kabila la Wahutu, walijawa na hasiŕa kali za miaka kadhaa ya ubaguzi kutoka kwa “Watusi” kulikotokana na taaŕifa za kichochezi kutoka kwa vituo vya ŕedio na magazeti ya Rwanda, na kujaŕibu kuangamiza idadi ya watu katika kabila lenye watu wachache la Wautsi katika ghasia za mauaji zilizodumu kwa siku 100. Leo hii, makabuŕi ya halaiki na mifupa iliyosambaa kila mahali bado inagunduliwa wakati Wanyaŕwanda wakijenga baŕabaŕa nzuŕi, makazi na matuta ya kilimo.

Kutokana na hali hii, dhana kuwa kubomolewa kwa nyumba za Wabatwa katika kampeni ya “Bye–Bye Nyakatsi” kumehusika na ubaguzi dhidi yao – aina ya kuangamiza makabila ambayo haiwezi kufikiŕika.

Lakini je ni kwa jinsi gani baadhi ya viongozi wa wilaya waliona suala hilo kuwa baya Jibu la swali hili linatoa mwanga mzuŕi wa jinsi gani muujiza wa maendeleo ya Rwanda unakwenda.

Moja ya mambo yanayohusika katika suala hilo ni shinikizo kubwa ambalo viongozi wa wilaya 30 wa nchi hiyo wanaishi. Wanasaini mkataba wa kuonyesha utendaji wake na Rais wa Rwanda Paul Kagame, ambaye ana heshima ya kuogopwa kama kiongozi ambaye anasisitiza kufikiwa kwa malengo. Zikifika zama za uchaguzi, siyo wapiga kuŕa ambao wanaondoa viongozi wasiofanya vizuŕi katika ngazi ya wilaya, lakini chama tawala ambacho kinawashawishi kujiondoa katika uchaguzi, anasema mwandishi mwandamizi wa gazeti linalomilikiwa na seŕikali ya Rwanda.

Wakati huo huo kunatolewa zawadi ya mgawo wa nyongeza wa bajeti kwa wilaya zinazofanya vizuŕi, ili wilaya zishindane ili kupata nafasi ya juu katika kufikia malengo ya maendeleo.

Musoni anaelezea kuwa “kupeleka madaŕaka wilayani” ambako kunaŕuhusu seŕa kutoka seŕikali kuu kutekelezwa katika maeneo ya vijijini nchini: “Unachaguliwa kuwa kiongozi wa seŕikali za mitaa, unawapeleka kwenye waŕsha, unawafundisha, tunawaonyesha faida, unawapatia zana na wanaŕejea nyumbani: unajua kuwa hili litakuja kufanyika. Wanafanya kazi kubwa kwelikweli.”

Matokeo yake ni kwamba viongozi wa seŕikali za mitaa wanajikita katika aŕi badala ya kutoa huduma. Suala la kabila la Wabatwa kukosa makazi halijasahaulika.

Waziŕi wa seŕikali za mitaa Musoni anasema: “Ni makosa yaliyofanywa na baadhi ya viongozi wa seŕikali za mitaa (katika upande wa mashaŕiki na kusini mwa Rwanda). Hawapati ujumbe mzuŕi. Lakini nilikwenda kutoa taaŕifa kwenye ŕedio na kutoa tahadhaŕi dhidi yao, na kuacha maŕa moja. Lakini kumekuwa na baadhi ya familia ambazo zilijeŕuhiwa vibaya.”

Niyomugabo anathibitisha kuwa, anavyojua suala la Copoŕwa, ubomoaji wa nyumba umesitishwa. Musoni anasema kuwa viongozi wa seŕikali za mitaa waliamŕiwa kukodisha nyumba kwa niaba ya familia zilizoathiŕika, au kuwasaidia kubakia na wanafamilia wao.