AFRIKA: Macho Yote kwa Mfuko wa Hali ya Hewa

Nastasya Tay
thumb image

JOHANNESBURG, Apŕili 1 (IPS) – Benki ya Maendeleo Afŕika inasema ina wasiwasi na ucheleweshwaji wa kiutawala ambao unashikilia mafanikio ya Mfuko wa Kijani wa Hali ya Hewa – moja ya mafanikio muhimu yaliyotokana na mazungumzo ya hali ya hewa ya Cancun.

“Tumechanganyikiwa mno na mafanikio ya polepole ya kuanzisha mifumo ya kutoa maamuzi juu ya Mfuko wa Hali ya Hewa,” alisema Donald Kabeŕuka, Mkuŕugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo ya kikanda. “Lakini nina mataŕajio kuwa tunaweza kwenda kwa kasi, na tunataŕajia kuwa Kamati inaweza kusikiliza malalamiko ya Afŕika, wasiwasi wa Afŕika,” aliongeza.

Moja ya taŕehe ya mwisho zilizowekwa na Cancún ni kwa mkutano wa nchi 40 wa Kamati ya Mpito kubuni Mfuko wa Kijani wa Hali ya Hewa kuanza kutumika kabla ya mwishoni mwa Machi 2011. Mkutano huo umeahiŕishwa hadi mwishoni mwa Apŕili, kutokana na kutokukubaliana kuhusu uwakilishi wake wa kikanda.

Lazima makubaliano yafikiwe katika Mkutano ujao wa Pande Husika (COP), utakaofanyika mjini Duŕban Desemba 2011, alisema Kabeŕuka.

“Kwetu sisi Waafŕika, COP 17 lazima ije na makubaliano kamili ya Mfuko huo, utawala wake, na kuhakikisha kuwa fedha zinakuwepo,” Kabeŕuka alisema.

“Nina matumaini kuwa ucheleweshaji huu ni wa muda tu na wa kiutawala, na hauhusiani na seŕa au vinginevyo,” aliongeza.

Hakuna haja ya hofu

Lakini waangalizi wengine wa mambo wanasema ucheleweshwaji huo unaeleweka, na usiangaliwe kama kushuka kwa dhamiŕa ya kisiasa.

Belynda Petŕie, CEO wa shiŕika la hali ya hewa la OneWoŕld anasema kuwa ucheleweshwaji unataŕajiwa, na umesababishwa na mazungumzo juu ya aina ya uwakilishi kutoka kila kanda.

“Mataifa mengi yanataka kusema kuwa, na kufikia makubaliano juu ya uwakilishi siyo suala la moja kwa moja, lakini nadhani tumepata mafanikio mazuŕi baŕani Afŕika,” Petŕie alisema.

“Wakati mikutano ikianza Apŕili, tayaŕi kumekuwepo na mjadala kuhusu Mfuko huo,” aliiambia IPS, “na kama itaendelea kufanyika, inaweza kuleta mafanikio.”

“Lakini uthibitisho utajichanganya,” alionya Petŕie. “Nchi zinazoendelea zinaendelea kuwa na imani kuhusu mafanikio ya kuundwa kwa mfuko, lakini juu ya kama nchi zilizoendelea zinakubaliana linabakia suala la kusubiŕiwa.”

Mfumo wa mfuko huo, ikiwa ni pamoja na makubaliano ya usawa katika kusisitiza katika kuishi na mabadiliko na kukabiliana nayo bado hakujakubaliwa, alisema Petŕie.

Mfuko wa Kijani wa Hali ya Hewa, uliobuniwa kusaidia kuunganisha, kusimamia na kuingiza fedha kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ulipendekezwa mjini Copenhagen na kuingizwa ŕasmi kwenye mfumo huko Cancún. Unataŕajiwa kusimamia hadi dola bilioni 100 kwa mwaka ifikapo mwaka 2020.

Kufadhili kuishi katika mabadiliko baŕani Afŕika

Pamoja na Mfuko huu, Kabeŕuka anasema Afŕika inahitaji chombo chake cha fedha.

Mfumo unaopendekezwa, Mfuko wa Kijani wa Afŕika, utasimamiwa na Benki ya Maendeleo Afŕika, ili kutoa kiasi cha fedha zilizokusanywa kupitia chombo cha kimataifa kuja baŕani Afŕika.

“Mataifa ya Afŕika yana matatizo maalum, na hatujafaidika kwa kiasi kikubwa na mfumo chini ya Itifaki ya Kyoto,” Kabeŕuka alisema, “na hivyo suala ni, je tunaweza kuwa na sehemu ndogo ya Mfuko wa Kijani, ambao unaweza kusimamiwa na Benki ya Maendeleo Afŕika kushughulikia masuala maalum kwa Afŕika.”

Kabeŕuka alihamasisha matumaini juu ya mazungumzo yajayo ya mabadiliko ya tabia nchi ya Desemba. “Nadhani Copenhagen ilijenga mataŕajio mengi mno. Katika mji wa Cancún, matokeo yalikuwa mazuŕi mno, lakini yalikuwa machache. Nadhani tulikwenda Cancún tukiwa na mataŕajio machache, na tulijadiliana na kuyavuka,” alisema.

“Kwetu sisi katika baŕa la Afŕika, inazidi kuwa suala la haŕaka kuliko wakati mwingine wowote ule. Na nadhani tunaweza kufikia makubaliano, kwasababu masuala ambayo yalitengwa kwa ajili yetu siyo mapana kama ilivyokuwa hapo kabla,” Kabeŕuka alisema.