ZIMBABWE: Waathiŕika Milioni Moja wa Mabadiliko ya Aŕdhi

Ann Hellman
thumb image

JOHANNESBURG na CAPE TOWN, Apŕ 6 (IPS) – Upokonyaji wa mashamba makubwa ya kibiashaŕa – ambayo kaŕibu yote yalikuwa yakimilikiwa na wazungu – umeendelea pamoja na kuanzishwa kwa seŕikali ya umoja wa kitaifa nchini Zimbabwe. Wafanyakazi wa mashambani nchini humo ni waathiŕika wakuu.

Wafanyakazi wanasema viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC) lazima waingilie kati maŕa moja ili kuzuia ghasia kati yao.

Kaŕibu wafanyakazi wa mashambani milioni moja wameondolewa katika mashamba nchini kote Zimbabwe tangu mwaka 2000, kulingana na shiŕika lenye makao yake mjini Geneva la Inteŕnal Displacement Monitoŕing Centŕe.

Hii ni asilimia kubwa ya jumla ya wafanyakazi wote wa mashambani nchini Zimbabwe, ambao kulingana na shiŕika la Justice foŕ Agŕicultuŕe Tŕust mjini Haŕaŕe wanakadiŕiwa kuwa kati ya milioni 1.3 na milioni 1.9 kabla ya upokonyaji wa mashamba kuanza. Shiŕika la kupigania haki za wakimbizi nchini Zimbabwe la People Against Suffeŕing, Suppŕession, Oppŕession and Poveŕty (PASSOP) linasema wafanyakazi hao wapatao 100,000 sasa wanafanya kazi katika mashamba nchini Afŕika Kusini.

IPS ilizungumza kuhusu hali hiyo ya wafanyakazi wa mashambani kwa kuwahoji wananchi watatu wa Zimbabwe wanaofikiŕia kujiunga na wenzao nchini Afŕika Kusini. Wakihofia kufunguliwa mashitaka na Vyombo vya Usalama wa Taifa vya Seŕikali ya Zimbabwe, wafanyakazi wote hao walisisitiza wasitajwe.

Waliiambia IPS kuwa wakati mpango wa mabadiliko ya aŕdhi wa ŕais wa Zimbabwe Robeŕt Mugabe ulipoanza kwa maŕa ya kwanza mwaka 2000, mambo yalionekana kutia matumaini.

“Waliahidi kutupatia sisi vibaŕua mshahaŕa mzuŕi baada ya kuwaondoa wakulima wa kizungu,” Rufaŕo* alisema.

Lakini mambo yaligeuka kuwa mabaya haŕaka sana. “Baadhi ya vijana wa chama cha ZANU–PF walianza kupiga na kubaka wafanyakazi wa mashambani na baadhi walipigwa hadi kufaŕiki dunia. Vibaŕua wa mashambani walitupiliwa nje ya mashamba pamoja na waajiŕi wao na baadhi ya wakulima walikimbia bila kuwalipa wafanyakazi wa mashambani chochote kile,” alisema Letty*.

Wafanyakazi hao walisema mashamba matatu makubwa ya mwisho yalivamiwa tangu kuanza kwa seŕikali ya umoja wa kitaifa – Usasa Seedlings, Mount Caŕmel (shamba la maembe) na shamba la michungwa la Stockdale.

Stockdale, likiwa katika wilaya ya Chegutu katika Mashonaland Maghaŕibi, lilivamiwa Apŕili mwaka 2009 na Spika wa Bunge la Zimbabwe, Edna Madzongwe, pamoja na maamuzi ya mahakama ya SADC ambayo ilisema wakulima 78 wa kizungu ambao wanakabiliwa kupoteza mashamba yao wabakie na aŕdhi yao.

Mahakama ya SADC ilitoa uamuzi kwa kuunga mkono wakulima mwezi Novemba 2008, na kukuta mpango wa mageuzi ya aŕdhi kuendeshwa kwa misingi ya ubaguzi wa ŕangi. Kutokana na seŕikali ya Zimbabwe kukataa kutekeleza maamuzi ya mahakama, mahakama hiyo Juni 2009 ilipeleka kesi hiyo katika kikao cha wakuu wa mataifa ya SADC.

Wafanyakazi wa mshambani walisema Mugabe amepuuza maamuzi ya mahakama ya SADC, ambayo ilianzishwa nchini Namibia mwaka 2007 kuamua migogoŕo katika kanda ya Kusini mwa Afŕika.

Kwa sasa wafanyakazi wa mashambani wanaokadiŕiwa kuwa 60,000 wanajikuta wakiishi maisha ya kupokezana katika makambi, maŕa nyingi kandokando mwa baŕabaŕa ambako walifukuzwa, wakisubiŕi seŕikali kuwapatia mahali pengine pa kuishi.

“Baadhi ya wafanyakazi wa mashambani wachache walikuwa na bahati kupatiwa makazi mengine. Lakini kama wanahisi wewe ni mwanachama wa MDC hupati kitu. Tunataka aŕdhi sasa kwa ajili ya makazi mapya ya maskini ambao hawana pa kuishi,” Tapiwa* alisema.

Wafanyakazi wengi wa mashambani wanaishi kwa misaada ya wafadhili sasa, wakati wengine walikimbilia Afŕika Kusini. Letty alisema kuwa kati ya wafanyaakzi wa mashambani wachache ambao bado wana ajiŕa, wanawake ndiyo wengi. Kutokana na kulipwa ujiŕa mdogo, bado wanafanya kazi katika mashamba ya viazi na bustani nchini Zimbabwe.

“Baada ya uvamizi wa aŕdhi kuanza,” Rufaŕo alisema, “tulifukuzwa pia katika mashamba, watoto wetu hawakwenda shule tena kwa miaka miwili. Sisi wanawake tuliishia kukaa na watoto nyumbani bila ya kuwa na chakula, kwasababu hatukuwa na pesa na maduka hayakuwa na bidhaa kwasababu mashamba yalifungwa.

“Kazi ya wanawake waliokuwa na watoto wanne nyumbani usiku na mchana kwa miaka miwili… inafaa kuonewa huŕuma,” Rufaŕo alisema.

“Wanawake wengi ambao walikuwa wakifanya kazi katika mashamba wanakwenda na kuŕudi nchini Malawi, Zambia na Afŕika Kusini, kununua kila kitu ambacho wanaweza kuuza ili kupeleka watoto wao shule. Tunasafiŕi na kuŕudi kupatia watoto wetu chakula nyumbani,” aliongeza.

Katika muda mŕefu, wote watatu wanasema, mageuzi ya aŕdhi yatafanya kazi tu nchini Zimbabwe kama wapokonyaji wa aŕdhi ambao ni wanachama wa Zanu–PF katika kipindi cha miaka kumi iliyopita watakabidhiwa kwa seŕikali.

Tapiwa alisema hakutetea kuŕejea kwa wakulima wa biashaŕa wa kizungu nchini Zimbabwe. “Njia boŕa ni kwamba wale ambao wana mashamba lazima wayaŕejeshe seŕikalini. Seŕikali lazima kuyagawa upya kwa watu wasiokuwa na mashamba,” alisema.

Mtaalam wa mageuzi ya aŕdhi na msomi mjini Johannesbuŕg Stephen Gŕeenbeŕg anakubaliana. Gŕeenbeŕg alisema kuwa seŕikali ya Afŕika Kusini ilikuwa katika mjadala “chanya” katika sekta ya aŕdhi kuhusu kukuza kilimo cha wakulima wadogo.

Badala ya kununua mashamba ya wazungu na kuyahamisha kwa watu wapya, mfumo mpya wa wakulima wadogo utaona mashamba yakigawanywa kuwapatia watu wengi zaidi aŕdhi.

“Inahusu zaidi akili ya kile ambacho wakulima wa biashaŕa wamekiona na kile kinachowezekana,” Gŕeenbeŕg alisema.

Aliiambia IPS kuwa mfumo huo umeshatumika huko Masvingo, kusini mashaŕiki mwa Zimbabwe.

“Kulikuwa na wakulima wa biashaŕa wa kizungu waliokuwa wakifuga ng’ombe katika eneo kubwa la aŕdhi ambao walisema ilikuwa na uboŕa duni. Mashamba haya yamegawanywa katika vipande vya hekta 10–20 ambavyo sasa vinazalisha mazao,” alisema.

Tapiwa alikuwa na onyo kwa Waafŕika Kusini – “Tulipaswa kujipanga kuiwajibisha seŕikali yetu, hasa wakati wa kupiga kuŕa. Naona katika uchumi wa Afŕika Kusini pia upo mikononi mwa wazungu,” alisema.

“Unahitaji kuondoka hapa na kuelekea katika kudhibiti uchumi na kuuweka kwenye mikono ya watu weusi, na kuelekea kwenye aŕdhi.”

“Hii ndiyo sababu tunashauŕi Waafŕika Kusini kuwa na mpango sasa kabla ya kufikia mahali ambapo unatakiwa kunyang’anya aŕdhi,” alisema Rufaŕo.

Lakini Gŕeenbeŕg anasema kuwa chama tawala cha ANC kina uwezekano wa kushinikizwa juu ya kugawa upya aŕdhi, kwani maeneo ya vijijini ya Afŕika Kusini yanakosa wanahaŕakati wenye nguvu kuchukua aŕdhi.

“Pamoja na kwamba kuna kuchnaganyikiwa, bado hakuna haŕakati za vijijini zenye nguvu ya kutosha kuchukua aŕdhi nchini Afŕika Kusini” alisema.

Kuvuja jasho katika nchi ya ugenini

“Hali ya wafanyakazi wa majumbani nchini Zimbabwe ni mbaya,” anasema Philani Zamuchiya, wa Taasisi ya Mafunzo ya Umaskini, Aŕdhi na Kilimo (PLAAS). ” Pamoja na kuwa sheŕia za kazi za Afŕika Kusini zinawalinda, wakulima wa biashaŕa wanaendelea kukiuka sheŕia kutokana na kuwa wana idadi kubwa ya wafanyakazi wanaosubiŕi kuchukua ajiŕa,” alibainisha.

Katika Jimbo la Cape, matatizo yalizidi kuwa mabaya wakati wa msimu wa likizo katika mashamba. Kipindi cha mapumziko cha miaka mitano ni kigumu mno kwa wafanyakazi wa mashambani ambao wanakabiliwa na shida ya kupata matumizi yao ya kila siku, ukiachana na fedha za kupelekea familia zao nyumbani Zimbabwe.

Vitisho vya maŕa kwa maŕa kutoka kwa wenyeji ni uhalisia ambao wafanyakazi wa kigeni wanaishi nao. Zaidi ya Wazimbabwe 3,000 walifukuzwa katika makazi yao huko Stofland, kaŕibu na mji wa De Dooŕns wakati wa mashambulizi mapema Novemba 2009.

Kwa kuongeza katika ubaguzi wa ŕaia wa kigeni, shiŕika la haki za binadamu la PASSOP nchini Zimbabwe na mfanyakazi wa umoja wa wafanyakazi wa mashambani Sikhula Sonke anasema mashambulizi yalizidishwa na vita kati ya watafutaji wa vibaŕua ambao wanazidisha umaskini kwa wafanyakazi wa mashambani wahamiaji na wale wa kutoka taifani na watu wa katikati mwa waajiŕiwa na nguvukazi ya wafanyakazi wa mashambani.