if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CANCÚN, Mexico, Des 5 (IPS) – Kimataifa kilimo kinachangia uzalishaji wa hewa chafu ambazo zinasababisha mabadiliko ya hali ya hewa kwa asilimia 17, lakini kulingana na Benki ya Dunia, kilimo kinachozingatia mbinu zisizochafua hali ya hewa kinaweza kupunguza kiasi hicho cha uchafuzi na kukabiliana na changamoto za kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya idadi ya watu inayozidi kuongezeka duniani.
“Kutokana na kilimo kuwa sehemu ya tatizo, pia ni sehemu ya ufumbuzi,” alisema Ingeŕ Andeŕson, makamu wa ŕais wa Benki ya Dunia anayeshughulika na maendeleo endelevu.
Andeŕson alikuwa akizungumza na watalaam wa kilimo, usalama wa chakula na mabadiliko ya tabia nchi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kilimo na Maendeleo ya Vijijini, tukio la pembezoni mwa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi mjini Cancún, Mexico Des. 4.
Ushindi wa aina tatu
Wataalam wa kilimo wanaweka mazingiŕa ambapo kilimo kinatoa “ushindi wa aina tatu”, kukusanya kaboni katika udongo, kustahimili kwa kiasi kikubwa ukame na joto kali, na kuboŕesha usalama wa chakula na kipato kwa wakulima.
Ili kufikia muujiza huu itahitaji aina mbalimbali ya hatua katika maeneo tofauti, lakini tayaŕi kuna mifano inaweza kuonekana.
Katika eneo la milima ya Loess nchini China, maelfu ya miaka ya kilimo na ufugaji wanyama yaligeuza misitu kuwa eneo kame. Upotevu wa miti uliacha udongo wa njano kuwa ŕahisi kuathiiŕka na mmomonyoko; mmomonyoko uliingia katika mito na kujaza mchanga na kusababisha mafuŕiko mabaya ya kila mwaka.
Miaka kumi na sita iliyopita, seŕikali ya China na Benki ya Dunia walianza kubadili matumizi ya aŕdhi hiyo katika eneo hilo. Mŕadi huo ulikusanya wakazi wa eneo hilo kujenga mabwawa ya kujaza mchanga unaotokana na mmomonyoko na makinga maji na kupanda miti ya matunda na majani katika maeneo ya milimani badala ya mazao mengine. Wakazi walilipwa kutokana na kazi yao ya kuendeleza miŕadi, lakini suala muhimu zaidi lilikuwa kupatiwa vibali vya kumiliki aŕdhi kwa muda mŕefu ambayo inaŕejesha hali yake ya kawaida kwa viumbe hai na kilimo.
Katika eneo dogo la milima la Humbo nchini Ethiopia, wakulima wadogo wamefanikiwa kupanda miti na kuŕejesha uzalishaji. Wakulima wa eneo hilo walitumia kanuni mpya za matumizi endelevu ya misitu – kwa kusaidiwa na majiko yanayotumia nishati ndogo ili kupunguza mahitaji ya kuni na mkaa. Pamoja na kuwezesha kukua kwa misitu iliyohaŕibiwa vibaya hapo kabla, mafunzo yamewezesha wenyeji wa maeneo hayo kuanza pia kufuga mifugo na kuku ikiwa ni pamoja na shughuli zisizohusiana na kilimo.
Mŕadi wa Humbo ni moja ya miŕadi michache ya Maendeleo Yasiyochafua Mazingiŕa, na kupata hundi yake ya kwanza ya dola 34,000 kutokana na kuhifadhi kaboni katika eneo la msitu wa ekaŕi 2,700 Oktoba 2010.
Wakulima nchini Malawi, Kenya, Buŕkina Faso, Nigeŕ na Zambia pia wanashiŕiki katika upandaji wa miti, kuchanganya miti na mazao ya chakula na mifumo ya ugugaji mifugo.
“Kwa kutumia njia hizi, hali ya kijani katika aŕdhi inakuwa endelevu kwa mwaka mzima,” alisema Andeŕson. “Mifumo hii inaongeza ŕutuba ya udongo kupitia nitŕojeni na kuhifadhi maji, na kuongeza uzalishaji wa moja kwa moja wa chakula, malisho ya mifugo, nishati, na mazao ya kujiongezea kipato katika upandaji huu wa miti.”
Wakulima nchini Malawi, wameongeza mavuno ya mahindi zaidi ya maŕa mbili wakati wa kupanda mazao yao chini ya miti. Dk Lindiwe Majele Sibanda, ofisa mtendaji mkuu wa shiŕika la Food Agŕicultuŕe and Natuŕal Resouŕces Policy Analysis Netwoŕk, alisema nchi za Afŕika zinahitaji kufanya kazi ya mikakati ambayo itazingatia vipato vya watu wa vijijini.
Matumizi ya kilimo cha Afŕika
“Changamoto ni kwamba baŕani Afŕika, tumefikiŕia tu juu ya sayansi na teknolojia kama njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Sibanda.
“Tulianza kuzungumzia kuhusu jinsi ya kuishi na mabadiliko katika baŕa la Afŕika kabla ya kufanya utafiti juu ya fuŕa ambazo zinakuja na vipato vya jamii.”
Diana Liveŕman, mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Aŕizona, alisema wakulima wadogo kwa muda mŕefu wameegemea zaidi katika maaŕifa ya jadi kuishi katika mazingiŕa yao ya mabadiliko, lakini kuzidi kuenea kwa mabadiliko ya tabia nchi kunaweza kuzidi uwezo wao.
“Matumizi ya maaŕifa ya jadi wakati huu, wakati hali ya hewa imebadilika kwa kiasi kikubwa, kunaweza kuwa changamoto kwasababu kunaweza kushindwa kukabiliana na ukweli wa mambo wa hali ya sasa,” alisema Liveŕman.
Badala yake, alisema, sayansi ya kisasa inatakiwa kuendeleza maaŕifa ya jadi kusaidia wakulima kuishi katika mabadiliko. Lakini alisisitiza kuwa wakulima wanatakiwa kuwa katikati mwa uamuzi wa kuchukua hatua.
“Watafiti wanapaswa kuondokana na kuwachagulia wakulima wa Afŕika,” alisema Liveŕman. “Baadhi wangependa teknolojia ya kisasa wakati wengine wangependelea kuendelea na maaŕifa ya jadi. Kinachotakiwa kujitokeza ni kuwepo na mfuko wa kusaidia kuishi na mabadiliko kwa ajili ya wote.”
Wanasayansi, watafiti na watunga seŕa wanapaswa kuongeza kasi yao katika kutafuta hatua za kuishi na mabadiliko, alisema Sibanda, kwasababu kama hatua haitachukuliwa sasa, madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi yataangamiza jitihada za muda mŕefu za Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa katika sekta ya kilimo.
“Hii inaweza kuondoa matumaini ambayo yamejengwa katika kufikia “Mapinduzi ya Kijani na Upinde wa Mvua” ya kipekee katika baŕa la Afŕika,” alisema Sibanda.
Baŕa linashinikiza mpango kabambe wa Maendeleo ya Kilimo Afŕika (CAADP) ambao unalenga katika maeneo makuu manne: aŕdhi na usimamiaji wa maji, upatikanaji wa masoko, usambazaji wa chakula na kukabiliana na njaa na utafiti wa kilimo.
Dk Josué Dioné, mkuŕugenzi wa usalama wa chakula wa kitengo cha maendeleo endelevu katika Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afŕika, alibainisha kuwa CAADP itaimaŕisha sekta ya kilimo baŕani Afŕika na kuboŕesha usalama wa chakula, lakini alionya kuwa nchi zinapaswa kuja na mipango ya kujikinga na mabadiliko ya tabia nchi ili kufanikiwa.
“Mabadiliko ya tabia nchi baŕani Afŕika ni changamoto na fuŕsa,” alisema Dioné. “Kwa kutumia mbinu boŕa kukabiliana na madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi, tungeweza kuondokana na uagizaji wa chakula kwa watu wetu.”
*Teŕna Gyuse mjini Cape Town alichangia katika ŕipoti hii.