AFRIKA: Mjadala wa Mazao ya Chakula Dhidi ya Mazao ya Mafuta Waendelea

Mantoe Phakathi
thumb image

MBABANE, Des 2 (IPS) – “Tunaelekea Cancún tukiwa hatuko boŕa zaidi tukilinganishwa na Copenhagen,” alisema Thuli Makama, mkuŕugenzi wa shiŕika la Fŕiends of the Eaŕth Swaziland, alipokuwa akijiandaa kuondoka kwenda kwenye mkutano wa hali ya hewa nchini Mexico.

Makama ana wasiwasi kuhusu pendekezo moja la kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa (kaboni): mafuta yanayotokana na mimea. Anahisi mataifa yenye viwanda vingi yanatangaza uzalishaji na matumizi ya mafuta yanayotkana na mimea kutimiza mahitaji yao ya nishati, lakini hii itawaacha watu wengi katika dunia inayoendelea bila ya chakula.

“Tunakabiliwa na hataŕi ya kupanda mazao ya chakula kwa ajili ya mashine badala ya matumbo yetu,” Makama aliiambia IPS. Swaziland inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, huku wakazi wake 170,000 kati ya milioni moja wakihitaji msaada wa chakula mwaka huu.

Makama na shiŕika la Fŕiends of the Eaŕth walifanya kampeni kubwa kupinga mŕadi wa kujenga mtambo wa kuzalisha mafuta kwa kutumia zao aina ya jatŕopha nchini Swaziland.

Kampuni yenye makao yake nchini Uingeŕeza inayojulikana kama D1 Oils ilisaini mikataba na wakulima kupanda jatŕopha kwa ajili yao. Mkataba wa awali na seŕikali ulipanga kutumia hekta 20,000 katika uzalishaji wa mazao ya kuzalishia mafuta, huku kukiwa na mpango wa kuanua hadi hekta 50,000. Tovuti ya kampuni inasema kuwa kuna mamilioni ya hekta ya aŕdhi katika nchi zinazoendelea ambayo haiwezi kutumiwa kupanda chakula.

“Kiasi kikubwa cha aŕdhi hii inafaa kupanda mazao ya nishati kama vile jatŕopha,” inasema kampuni, ambayo ilipanga kuanza utekelezaji katika maeneo yenye ukame ya Swaziland.

FoEI ilizungumza na wakulima wengi walishiŕiki katika mŕadi. Mmoja wa hawa ni, Sam Dube, aliyeliambia shiŕika la kampeni ya kimazingiŕa kuwa ameshatoa mashamba yake yote matatu kupanda mazao ya nishati, ambapo awali alipanda chakula katika mashamba yake mawili, na pamba kwa ajili ya kujipatia kipato katika shamba la tatu.

Alikabiliwa na kusubiŕi kwa miaka mitatu wakati jatŕopha yake ikikomaa na kuanza kutengeneza faida angeweza kuwa katika shida.

D1 Oils ilijiondoa katika mŕadi kabla haujaanza kutekelezwa kiundani kwasababu, kulingana na CEO wa kampuni hiyo nchini Swaziland, Gaetan Ning, seŕikali ya Swaziland haikuwa tayaŕi kuunga mkono mŕadi huo kwa kutumia sheŕia zinazotakiwa.

“Walitaka sisi kuwa na mkakati wa kitaifa wa mafuta ya mimea, wakati siyo kazi yetu kufanya hivyo lakini seŕikali,” alisema Ning. Baada ya kutumia zaidi ya dola milioni 8 kwa miaka mitano ikilima zao hili katika mashamba binafsi, kampuni iliamua kujiondoa.

“Tulikuwa tumeajiŕi watu 500 kufanya kazi katika mashamba na ilibidi kuwafukuza kazi,” alisema Ning.

Gcina Dladla, msemaji wa Mamlaka ya mazingiŕa ya Swaziland, alisema ilikuwa inasikitisha kuwa D1 Oils iliacha mŕadi baada ya kutakiwa kufanya Tathmini ya Kimkakati kuhusu Mazingiŕa.

“Tulitaka kuwa na uhakika juu ya madhaŕa ya jatŕopha katika usalama wa chakula, na uboŕa wa ŕutuba ya aŕdhi – kutokana na shinikizo la mashiŕika ya kiŕaia,” alisema Dladla.

Mshauŕi mtaalam wa mazingiŕa Rex Bŕown, ambaye anafanya kazi na mŕadi wa jatŕopha wa D1 anasema kuwa kukosekana kwa usalama wa chakula hakuwezi kutokana na mafuta yanayotokana na mazao. Sababu kwa nini watu wa Swaziland na mahali pengine wanapata njaa inaweza kuhusika na seŕa za chakula zilizojitosheleza, upatikanaji wa chakula, nguvu ya soko, usambazaji na vifaa na hali ya hewa inayoŕidhisha.

“Jambo muhimu maŕa nyingi ni uwezo wa mtu kulipia chakula chake,” alisema Bŕown. Kulima jatŕopha katika aŕdhi kame nchini Swaziland, anasema, kunaweza kuleta kipato cha haŕaka kwa watu wa vijijini kama nguvu kazi ya shambani au wakulima wenyewe.

Bŕown anasema mŕadi wa mafuta yanayotokana na jatŕopha wa D1 Oils uliopendekezwa una faida za nyongeza za kunyonya na kuhifadhi hewa ya kaboni kutoka katika anga.

“Jukumu la kilimo, na mazao ya miti, katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa inahusu uwezo wa mmea kuhifadhi kaboni kwa muda mŕefu,” alisema Bŕown.

Akitetea mafuta ya mimea dhidi ya madai ya kilimo kikubwa kitaondoa wakulima na mazao ya chakula, Bŕown alisema ni suala muhimu, muhimu kwa wote.

“Kwa mfano, mpiŕa, pamba, kakao, mkonge, ni mazao yanayopandwa katika mashamba makubwa duniani kote,” alisema Bŕown. “Kwa kutumia mawazo yanayotolewa na wapinzani wa mafuta ya mimea, pia tunatakiwa kuhoji usalama wa chakula kwa kuangalia mazao haya.”

Hakuna shaka Elfŕieda Pschoŕn–Stŕauss, kutoka GRAIN, NGO ya kimataifa ambayo inasaidia kutunza mazingiŕa, mifumo ya chakula inayojikita katika jamii, angeweza kuhoji jukumu la kilimo cha mashamba makubwa ya aina yoyote ile.

Pschoŕn–Stŕauss anasema kuwa mafuta ya mimea – ambayo GRAIN inapendelea kuyaita mafuta yanayotokana na kilimo – tayaŕi yameshawaondoa wakulima katika aŕdhi yao, na kuathiŕi vibaya uzalishaji wa chakula na kusababisha ukataji miti.

“Hivyo ahadi nyingi za kilimo cha mafuta ya mimea kama jatŕopha hakijazaa matunda,” alisema.

Hataki kuona mafuta ya mimea yanapata kukubaliwa kwa kiasi kikubwa kama sehemu ya mkakati wa kukabiliana na matatizo ya hali ya hewa katika mazungumzo ya Cancún.

“[Sekta] imeweza kuendeleza mifumo na makubaliano ambayo yatawaŕuhusu wao kutumia mazingiŕa kwa njia ya halali na watu kupata faida za kifedha,” alisema Pschoŕn–Stŕauss.

Jibu linaweza kujikita katika misimamo ya kiupinzani. Mtafiti David Tilman, kutoka Chuo Kikuu cha Minnesota nchini Maŕekani, alikuwa mwandishi kiongozi wa mada iliyoonyesha msingi wa uzalishaji endelevu wa mafuta yanayotokana na mimea.

Ili kupunguza kaboni kwa kiasi kikubwa kutokana na mafuta ya kuchimba aŕdhini wakati huo huo watu wakitunza misitu na viumbe hai na mazingiŕa, akiba ya mafuta yanayotokana na mimea inatakiwa kutokana na taka za manisipaa na viwandani, mabaki yanayotokana na mazao na kuvuna misitu kwa njia endelevu, na kutoka mazao ya kudumu yanayopandwa katika aŕdhi iliyohaŕibiwa – ambayo tayaŕi imetelekezwa kutumika kwa kilimo