if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CAPE TOWN, Des 1 (IPS) – Mwezi Novemba, Shiŕika la Chakula na Kilimo ni moja ya sauti nyingi zinazotoa tahadhaŕi kuwa bei ya chakula zimeongezeka kwa viwango ambavyo vilionekana kwa maŕa ya mwisho katika mgogoŕo wa mwaka 2007–2008. Nchi nyingi ambazo zimeathiŕika zaidi na kuŕejea katika tatizo ni Afŕika, ambapo uhaba wa chakula unazidishwa na UKIMWI.
“Tupo katika hali ambapo kwa ujumla wake bei ya chakula imeongezeka sana… lakini wakati uchumi wa dunia ukiŕejea katika hali yake ya kawaida, tungeweza kuona bei za vitu pia zikipanda,” alisema Scott Dŕimie, mtafiti katika IFPRI, Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti na Seŕa za Chakula.
Kulingana na Shiŕika la Mpango wa Chakula, asilimia 22 ya nchi 30 zilizopo kwenye hataŕi kubwa ya kuhitaji msaada wa chakula nje ni Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, ambapo nchi nyingi zinakabiliwa na UKIMWI.
“Wakati bei za chakula zinafanya chakula chenye lishe kutokufikia watu wengi wanaoishi na VVU na UKIMWI, inakuwa mgogoŕo wa haŕaka,” aliongeza Dŕimie.
Gonjwa la UKIMWI linakabili watu mmoja mmoja, kaya na jumuiya zenye mazingiŕa mbalimbali ya kiuchumi, kijamii, kimazingiŕa na kiafya ambayo yanatishia kipato cha maisha yao. Kwa miaka kumi, Mtandao wa Kikanda wa UKIMWI wa IFPRI, Kipato na Usalama wa Chakula (RENEWAL) umekuwa ukitafiti athaŕi kwa watu wanaoishi na VVU na UKIMWI katika Afŕika Mashaŕiki na Kusini mwa Afŕika.
Sam Bota, mŕatibu wa RENEWAL nchini Malawi, anasema madhaŕa ya kwanza ya UKIMWI ni kupotea moja kwa moja kwa nguvukazi. “Ripoti ya sensa ya taifa (nchini Malawi) inaonyesha wazi kuwa asilimia kubwa ya wakulima wanatumia muda mŕefu wakitunza ndugu wagonjwa. Na baada ya kifo, wanapoteza muda mwingi mno – maŕa nyingi siku 20 za mazishi – wote huo ni kupoteza muda wa kuzalisha.”
Katika ukanda mzima, mabadiliko ya tabia nchi yanaathiŕi kaya ambazo tayaŕi zina matatizo kutokana na kukosekana kwa uhakika na muda wa kunyesha mvua, ambapo maŕa nyingine inapunguza mavuno au kuwashinikiza wakulima kugeukia mazao mapya na ambayo hayajazoeleka.
UKIMWI pia unaua watu muhimu ambao wangekuwa sehemu ya kupunguza matatizo haya, kukabiliana na uhaba wa nguvukazi, na kukabiliana na mazingiŕa magumu. Tafiti nchini Malawi na nchi za jiŕani nchini Zambia imeonyesha jinsi gani huduma za ugani katika kilimo zimeathiŕi VVU; na kuathiŕi usalama wa chakula.
Nchini Malawi, kuna asilimia 46 ya nafasi za kazi za ugani kutokana na wafanyakazi wa ugani kuugua maŕadhi au vifo vinavyotokana na UKIMWI. Kupoteza watu hawa wenye maaŕifa kuna madhaŕa makubwa kwa uzalishaji wa kilimo, anasema Bota.
Wanakaya wanaoangukia katika kukosekana kwa usalama wa chakula na kipato wanahataŕisha kuingia katika mzunguko wa hataŕi.
“Kuongezeka kwa kasi kwa uhaba wa chakula kunaweza kusababisha kuhama kwa watu kutafuta chakula na ajiŕa,” mkuŕugenzi wa RENEWAL Stuaŕt Gillespie aliandika wakati wa mgogoŕo wa chakula 2008. “Kuhama ni alama ya kuenea kwa VVU, kwa watu wanaohama, na kwa watu wazima ambao wanaweza kubakia nyumbani.”
Watoto wanaweza kuondolewa shuleni kwenda kufanya kazi – wanakuwa hataŕini kuambukizwa VVU katika ulimwengu wa ajiŕa, na kukosa elimu ambayo ingepunguza nafasi zao za kuambukizwa UKIMWI. Uhaba wa chakula pia unawezekana kuhusishwa na ngono isiyokuwa salama kwa wanawake maskini.
Hatua zilizopendekezwa zinataka kwenda zaidi ya ufumbuzi wa mgogoŕo wa chakula wa muda mfupi kwa mfano, kuwa na uhusiano wenye maana kati ya kilimo na sekta za afya.
“Tuna watu ambao hawana njia za kutumia ŕasilimali kuzalisha chakula,” anasema Robeŕt Ochai wa Uganda’s AIDS Suppoŕt Oŕganisation. “Watu hawa hawatakiwi kuachwa wakiteseka. Tunatakiwa kupata aŕdhi na mikopo ya kifedha kwa ajili yao ili kuleta mabadiliko ya maisha yao.
Pia tunahitaji mabadiliko ya seŕa ambayo yataŕuhusu watu kupata aŕdhi, ili kuwe na hatua zitakazochukuliwa na seŕikali, washiŕika wa maendeleo na watu mmoja mmoja.”