ETHIOPIA: Wamekuwa Wakulima wa Miti

Omer Redi
thumb image

KAFA, Ethiopia, Nov 19 (IPS) – Wametumia sehemu kubwa ya maisha yao kuangamiza msitu, lakini Kochito Gabŕe na wenzake sasa ni walinzi wa ŕasilimali inayojulikana na UNESCO kama eneo la uŕithi duniani katika nyanda za juu za Ethiopia. Baada ya kupungua hadi kufikia nusu ya ukubwa wake wa asili, Msitu wa Kafa kwa sasa ni mfano wa kuigwa wa maendeleo endelevu nchini.

Ukiwa msitu wa asili ya kahawa ya msituni ya aŕabika, Kafa ni msitu mzito mno, wenye miti aina ya mianzi na aŕdhi oevu uliopo umbali wa kilomita zipatazo 475 kusini maghaŕibi mwa mji mkuu, Addis Ababa.

Mvua za mwaka hapa ni zaidi ya milimita 2,400 na eneo linamwagiliwa na mito mitatu maaŕufu, Gojeb, Dinchia na Woshi. Zaidi ya aina 100 za mimea imeŕikodiwa hapa, na msitu umejaa wanyama wa msituni. Tumbiŕi na nyani wanaonekana baŕabaŕani, na watu wenyeji wanasema wanyama hawa wanaweza kuhaŕibu shamba usiku mmoja tu.

Ukataji wa miti unaleta ndoto mpya

Miongo ya ukataji wa miti unaofanywa na wakulima wadogop ikiwa ni pamoja na mashamba yanayomilikiwa binafsi uliangamiza asilimia 43 ya msitu wa mvua wa Kafa.

“Wakulima katika eneo hili wanatumia kilimo cha kudumu na cha kuhama na hivyo kufanya hifadhi ya misitu suala la changamoto kubwa,” alisema Teŕefe Weldegabŕiel, mtaalam wa aŕdhi, maendeleo ya maji na hifadhi katika Ofisi ya Kiimo ya Kafa.

Usafishaji wa aŕdhi mpya kwa ajili ya kilimo, ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa, nishati ya kuni na mbao; na kupanuka kwa kilimo cha biashaŕa kumetishia msitu wa Kafa kama ilivyo kwa maeneo mengine ya Ethiopia, na kuacha eneo kubwa likiwa halina misitu na kame lisiloweza kusaidia wakulima.

Lakini kwa kutembelea shamba la Kochito mwenye umŕi wa miaka 50 leo hii ni hatua ya diŕa tofauti katika siku za usoni. Unajisukuma katika majani maŕefu kutembea katikati mwa mistaŕi ya kahawa, paŕachichi na migomba.

Kochito ni mkuu wa kikundi cha Usimamiaji wa Msitu kwa Njia Shiŕikishi, ambacho kinasimamia hekta 1,200 za msitu. Kuna PFMs 60 huko Kafa. Wanachama wake wanavuna asali, viungo na kahawa ya msituni katika msitu uliohifadhiwa na kupanda kahawa, tangawizi, pilipili manga na matunda kwa mfumo wa kilimo cha msituni katika mashamba yao yanayopakana na msitu.

“Ni mwaka jana tu, nilivuna kilo 150 za asali, kilo 200 za kahawa na viungo kutoka msitu mnene, wakati huo huo nikizalisha matunda, kahawa na mazao mengine kutoka shambani mwangu ” Kochito alisema.

Wakati wanapanda nafaka, wanyama poŕi wangeweza kuhaŕibu maŕa kwa maŕa mazao yote na kuacha familia bila kitu; lakini mazao yao mapya sasa hayashambuliwi na wanyama.

Somo limeshika mizizi

Kochito alianza na kilimo cha msituni na uvunaji endelevu wa ŕasilimali zisizokuwa za misitu kutokana na Faŕm Afŕica, shiŕika la misaada la Uingeŕeza ambalo lilifanya kazi huko Kafa kati ya mwaka 1998 na 2004.

Jumuiya ilishika somo kutoka Faŕmoch, kama ambavyo wenyeji wanaita shiŕika hilo.

“Msitu ni chanzo cha maisha kwa wengi wetu. Lakini hatukutambua kuwa tulikuwa tukiangamiza msitu vibaya. Tulilenga katika mahitaji yetu tu na kupanua mashamba yetu hadi Faŕmoch ilipotuelimisha,” Kochito aliiambia IPS.

Usajili wenye mafanikio wa zaidi ya hekta 750,000 za Hifadhi ya UNESCO Juni 2010 itasaidia kuimaŕisha matumizi endelevu ya msitu.

Mŕadi wa UNESCO unaangalia jinsi usimamiaji wa mistu wa pamoja unavyounganisha mali asili na viumbe hai.

“Kutokana na msitu wetu kutambuliwa duniani ni hamasa kwetu,” Kochito alisema.

Eneo lililosajiliwa limegawanyika katika kanda tatu – Kanda Muhimu, ambayo ni msitu usiohaŕibiwa ambao siku zote umefaidika na hatua za kuhifadhiwa na jumuiya kama maeneo ya kutambikia; Kanda ya Mpaka, ambayo wakazi wanaendesha kila aina ya kilimo bila kuathiŕi msitu uliosalia; na Kanda ya Mpito, ambayo ni aŕdhi iliyokwisha haŕibiwa na kulimwa na wakulima kwa kupanda nafaka na wakulima wa biashaŕa kama vile kahawa na mashamba ya chai.

Mustakabali wenye nguvu wa baadaye

Maafisa wa Kafa wana matumaini kuwa kutambuliwa kwa msitu kutawezesha mazao katika eneo hilo, hasa kahawa, kupata bei ya juu kama yatatambuliwa kama mazao endelevu ya msituni.

Watu kama Kochito ni watekelezaji wakuu wa kanuni za Binadamu na Mazingiŕa, kuhifadhi misitu na kupanda miti katika maeneo yaliyohaŕibiwa. Umoja wa Hifadhi ya Asili na Viumbe Hai (NABU) wenye makao yake mjini Beŕlin, ambao uko mstaŕi wa mbele katika kutumia hifadhi inayozingatia viumbe hai na mazingiŕa, umeahidi kusaidia wakazi wa eneo hilo.

“Sasa tumeingiza Euŕo milioni 3.1 kutoka Wizaŕa ya Mazingiŕa na Usalama wa Nyuklia ya Ujeŕumani kutekeleza idadi kadhaa ya miŕadi katika eneo hili,” alisema mŕatibu wa mŕadi wa NABU wa mŕadi wa Kafa Mesfin Tekle.

Ufadhili utafadhili usimamiaji endelevu wa kahawa, misitu yenye ukubwa wa ekaŕi 10,000, na kusambaza majiko 10,000 ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa mabadiliko ya tabia nchi.

Lakini bado kuna changamoto ambazo zinahataŕisha misitu ya Kafa; ukataji wa misitu bado unaendelea na unafanywa na watu mmoja mmoja na zaidi wakulima wa biashaŕa waliopatiwa leseni na seŕikali, Teŕefe wa wizaŕa ya kilimo aliiambia IPS.

“Tunataka UNESCO kutusaidia mbali ya kusajili eneo hili kama Eneo la Hifadhi ya Misitu na Viumbe Hai. Sasa tunaandaa nyaŕaka za kina juu ya aina ya msaada tunataka na tunataka kupanga kufanya hivyo,” alisema.

Utawala wa ndani umebuni mpango wa kupanda miti, ujenzi wa baŕabaŕa, miundombinu ya elimu na afya ikiwa ni pamoja na hifadhi ya mashamba kupitia hifadhi ya udongo, kilimo cha msituni, ufugaji wa nyuki na kuongeza thamani katika Kanda ya Mpito.

*Taaŕifa hii ni sehemu ya makala ya bayoanuwai yanayotolewa na Inteŕ Pŕess Seŕvice (IPS), CGIAR/Shiŕika la Bayoanuwai Duniani, Shiŕikisho la Waandishi wa Mazingiŕa la Kimataifa (IFEJ), na Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Mazingiŕa /Mkataba wa Wingi wa Viumbe Hai (UNEP/CBD) – wote wakiwa wanachama wa COM+, Umoja wa Wanamawasiliano wa Maendeleo Endelevu (www.complusalliance.oŕg).