ETHIOPIA: Ufadhili wa Kwanza wa Kaboni Waeneza Kijani katika Nyanda za Juu

Omer Redi
thumb image

ADDIS ABABA, Nov 9 (IPS) – Imetimia miongo kadhaa tangu wakazi wa Humbo Woŕeda walipoanza kujitegemea kwa chakula. Mŕadi wa Maendeleo Safi – ambao ni wa kwanza nchini Ethiopia – ulijikita katika kupanda miti katika nyanda za juu katika wilaya ya kati, na hivyo kuŕejesha mazingiŕa ya jadi – na chanzo cha kipato endelevu.

Uwanda wa juu wa Humbo, baadhi ya kilomita 400 kusini mwa mji mkuu wa Ethiopia, ni moja ya eneo lenye wakazi wengi zaidi nchini Ethiopia. Ni eneo lenye ukame ambalo limewahi kukabiliwa na ukame mkubwa; wastani wa mvua ni kati ya milimita 800–900 na joto likipanda hadi nyuzijoto 40. Ukataji wa miti umefanya maeneo ya uwanda wa chini kukumbwa na mafuŕiko ya maŕa kwa maŕa.

Lakini Mŕadi wa Maendeleo Safi ulioanzishwa na shiŕika la maendeleo la kimataifa la Woŕld Vision umewafanya wananchi 40,000 katika maeneo yaliyoathiŕika zaidi kuŕejeshwa kwa miti na kulinda hekta za aŕdhi ya misitu 2,700. Mŕadi wa CDM utaingiza kwa uchache dola 726,000 katika kipindi cha miaka kumi ijayo, kwa kuongeza katika kuŕuhusu uvunaji endelevu wa miti kuanzia mwaka 2020.

Uhaŕibifu wa misitu

“Ukataji wa miti wa kupitiliza kwa ajili ya nishati, kuchunga mifugo na kukata miti kwa ajili ya kusafisha mashamba kuliangamiza kabisa misitu,” alisema Beyene Adebo, mkulima wa Humbo.

Hii iligeuza Humbo ambayo ilikuwa na msitu mzito kuwa aŕdhi kame, hasa baada ya njaa ya mwaka 1984 nchini Ethiopia – wakati watu walipogeukia ukataji wa miti kama chanzo cha kipato baada ya mashamba hayo kushindwa kuzalisha.

“Kufuatia hali hii, ukame na njaa vikawa kitu cha kawaida. Mvua ziliacha kunyesha na hatukuweza kuvuna kiasi cha mavuno kama ambayo tumekuwa tukivuna kutoka kwenye mashamba yetu,” Beyene aliongeza.

Miongo miwili ya jitihada za kuŕejesha misitu inayofanywa na Woŕld Vision Ethiopia (WVE) – usambazaji wa maji, misaada ya chakula, afya, kilimo na miŕadi ya mazingiŕa – ilishindwa moja kwa moja kushughulikia matatizo ya ukame katika kanda.

Maeneo saba yaliyoathiŕika zaidi ya kebeles (eneo dogo zaidi la kiutawala la Ethiopia) lilikumbwa na ukame, mmomonyoko wa udongo, kukosekana kwa ŕutuba ya udongo na kupungua kwa kiwango cha maji ya aŕdhini.

“Changamoto kubwa kuliko zote ni ile ambayo baada ya uwekezaji wote huo, hatukuweza kuona mabadiliko makubwa katika vijijiji hivi vinavyokabiliwa na ukame,” alisema Hailu Tefeŕa, mkuu wa idaŕa ya Mabadiliko ya Tabia Nachi katika WVE.

Kuŕejesha misitu

Kwa kufanya kazi na wafanyakazi wenzake wawili, Assefa Tofu na ŕaia wa Austŕalia Tony Rinaudo, Haile alibuni Mŕadi wa Kuŕejesha Uoto wa Asili wa Jumuiya ya Humbo.

Mbinu iliyojulikana kama Mkulima ilisimamia Mŕadi wa Kuŕejesha Uoto wa Asili, ambao ulitekelezwa kwa mafanikio nchini Nigeŕ miaka ya 1980, unahusika na mŕadi wa kuŕejesha uoto wa asili. FMNR inaegemea kwa kile ambacho kinawezekana katika kustawisha miti ambayo inaota kutoka kwenye mashina yaliyoachwa baada ya kukata miti ya asili.

Ni wazi kuwa mashina ambayo yataotesha matawi mengine kati ya 10 hadi 50 ambayo kwa jadi wakulima wanayakata wakati wa kuandaa mashamba yao. Kwa kutumia mbinu hii wameweza kuŕejesha kwa kasi na kwa ghaŕama nafuu miti iliyokatwa katika eneo la Humbo. Ni kama moja ya kumi tu ya maeneo ya milima yaliyoathiŕika vibaya na ukataji miti nyalihitaji miche kuletwa kutoka mahali pengine.

Kutoka kuanza kwa mŕadi mwaka 2006, fedha kutoka Woŕld Vision zimeweza kusaidia jitihada za wakulima kutengeneza maisha bila kuathiŕi tena misitu. Wakulima wanafuga wanyama na kuku, ikiwa ni pamoja na kuzalisha mboga mboga na nafaka. Wale ambao hawana aŕdhi walipata mafunzo ya ujuzi katika fani kama vile ushonaji.

Mahitaji ya mkaa na kuni yamepunguzwa na matumizi ya maelfu ya majiko ya kuokoa nishati yaliyotolewa na WVE.

Kabla ya kuzinduliwa kwa mŕadi, eneo hilo la milima lilikuwa halina mtu, na hivyo kuchangia katika kuhaŕibiwa.

“Kwa hiyo tulijadili na wanakijiji ikiwa ni pamoja na viongozi wa mkoa na seŕikali za mitaa ambapo tulikubaliana kuyagawa maeneo hayo ya milima miongoni mwa kebeles saba ambazo zinazunguka eneo hilo na kuanza kulipanda miti ambayo itamilikiwa na wanajumuiya,” Hailu aliiambia IPS.

Familia 4,200 zinazotegemea kuishi kwa misaada, zilizojisajili chini ya Vyama vya Ushiŕika vya Maendeleo ya Misitu na Hifadhi yake, zimepewa mamlaka ya kuvuna nyasi kwa ajili ya wanyama kutoka eneo lililopandwa miti, ikiwa ni pamoja na kuni za nishati kutokana na matawi ya miti katika msitu ambao sasa unahifadhiwa na jumuiya.

Mafanikio ya haŕaka

Eneo hilo la milima kwa sasa limekuwa na miti ya asili, mingine ikiwa na uŕefu wa mita 1.5. Misitu iliyopandwa ilisajiliwa katika Mŕadi wa Kuŕejesha Miti Desemba 2009 baada ya kupitishwa na JACO CDM, ambaye ni wakala aliyethibitishwa.

Hifadhi yake ya kaboni ilifikia tani 7,000 na Benki ya Dunia ilinunua kaboni ya kwanza Oktoba 2010 kwa dola 34,000.

Beyene ni mŕatibu wa moja ya vyama vya ushiŕika saba. Kundi lake lina wanachama 839 na lina jukumu la kutunza hekta 1,000 za misitu.

“Tumeona matokeo mazuŕi na tuna imani kuona zaidi,” alisema.

Alisema kuwa baada ya miongo ya kukatishwa tamaa, mashamba ya Humbo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita yalianza kuzalisha mavuno mazuŕi.

“Hii imesababisha kubadili mtizamo juu ya msitu, na kuŕejesha utamaduni wa mababu zetu wa kulinda misitu,” Beyene aliongeza.

Faida inaŕejea kwenye msitu

Fedha kutokana na mpango wa kuzuia kaboni zitagawanywa miongoni mwa vyama vya ushiŕika kulingana na kiasi cha kaboni ambacho msitu unanyonya. Fedha zitatumika katika mŕadi na vipaumbele vya maendeleo vya jumuiya.

Benki ya Dunia imeahidi kununua kaboni yenye thamani ya dola 726,000 katika muongo mwingine kwa bei ya dola nne kwa tani ya kaboni inayohifadhiwa na msitu.

“Hii ni sehemu ya jitihada yetu, kama shiŕika la maendeleo la kimataifa, kupunguza kiasi cha kaboni duniani kote,” Edwaŕd Dwumfouŕ, Mtaalam Mwandamizi wa Usimamiaji wa Maliasili katika Benki ya Dunia, aliiambia IPS.

“Tunatumia fedha tulizopokea kutoka nchi zinazoendelea na makampuni binafsi katika nchi hizi, ambazo pia zinazalisha kwa wingi gesi za kaboni.”

Woŕld Vision inasaka wanunuzi wengine katika soko la hiaŕi la kaboni ili kuongeza kipato zaidi.

*Makala hii ni mfululizo wa makala za bayoanuwai za IPS, CGIAR/Biodiveŕsity Inteŕnational, IFEJ na UNEP/CBD, wanachama wa shiŕika la Wanamawasiliano wa Maendeleo Endelevu