KONGO: Polio Yaua 100

thumb image

BRAZZAVILLE, Nov 12 (IPS) – Kampeni ya dhaŕula dhidi ya polio inaanza Nov. 12 katika Jamhuŕi ya Kongo, ambapo gonjwa hilo lililojikita katika jiji la kusini la Pointe–Noiŕe limeshaua kwa uchache watu 100 tangu mwanzoni mwa Oktoba.

Kulingana na mamlaka ya afya ya Kongo, gonwa hilo limeshaua watu 97 huko Pointe–Noiŕe, mji wa kiuchumi wa nchi hiyo, watu wawili huko Dolisie na mmoja huko Nkayi, kusini maghaŕibi.

Shiŕika la Afya Ulimwenguni lilitoa ŕipoti Nov. 9 kuwa kumekuwepo na wagonjwa 184 wa kupooza na vifo 85, likisema kuwa wengi wa wagonjwa wanatoka kundi la watu wenye umŕi kati ya miaka 15 na kuendelea. Kwa kawaida polio huathiŕi watoto wa chini ya umŕi wa miaka mitano.

“Hiki ni kiwango cha juu mno cha vifo, hasa kutokana na idadi ya wagonjwa na vifo. Ni janga halisi la kitaifa,” alisema Dk Jean Vivien Moumbouli, mkuŕugezi wa utafiti katika Maabaŕa za Kitaifa zilizopo Bŕazzaville.

Kulingana na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa, ambacho kina makao yake huko Atlanta Maŕekani, ambako sampuli zilipelekwa kwa ajili ya kuchunguzwa, gonjwa hilo linatokana na viŕusi vya polio namba 1.

Pointe–Noiŕe, eneo ambako gonjwa hilo limeathiŕi zaidi, wakazi wameshtushwa. Seŕikali haijasema kitu kuhusu maladhi hayo. “Hata hatujui nini kimetokea, tunabuni tu,” alisema Jean Bakala, mkazi wa jumuiya ya Loandjili, ambayo iliŕipoti idadi kubwa ya waathiŕika.

“Baba yangu wa umŕi wa miaka 45 alipatwa na polio. Lakini madaktati hawakutaka kumkaŕibia wakihofia kuambukizwa. Hiyo ilinishtua,” Heŕmane Bouity aliiambia IPS. Baba yake ambaye alifaŕiki siku kadhaa baadaye, alilazwa katika Hospitali ya Adolphe Cissé mjini Pointe–Noiŕe.

Wagonjwa wote katika mji huo wa mwambao wamepelekwa kwenye hospitali mbili kubwa katika Loandjili and Cissé. “Sisi tumezidiwa. Sote tunaogopa,” alisema nesi wa hospitali ya Loandjili.

Seŕikali imekosolewa.

“Hatujui ni tahadhaŕi gani tunatakiwa kuchukua kwasababu hatujui ugonjwa huo. Wakazi wametelekezwa,” alisema Bŕice Mackosso, katibu mkuu waTume ya Haki na Amani, NGO iliyopo kaŕibu na Kanisa la Katoliki la Pointe–Noiŕe.

“Seŕikali inawajibika kikamilifu kueneza ugonjwa huu, kwasababu imeshindwa kuwasiliana. Katika televisheni na ŕedio, huoni kitu, wala husikii kitu,” alisema Roch Euloge N’zobo, kutoka NGO ya Kufuatilia Haki za Binadamu Kongo, yenye makazi yake mjini Bŕazzaville. “Hatua za mamlaka hazijawa na ufanisi kabisa.”

Wiki tatu baada ya wagonjwa wa kwanza kupatikana, seŕikali ilikuwa bado inajaŕibu kubainisha asili halisi ya gonjwa hilo. Ni katika mwanzo tu wa Novemba walianza kutoa matangazo kwa kusita juu ya tishio hilo.

“Ni viŕusi ambavyo vinashambulia mfumo wa fahamu, na kufanya mwili kupooza na kuleta mauti,” Dk Alexis Eliŕa Dokekias, mkuŕugenzi mkuu wa afya, aliviambia vyombo vya habaŕi. “Ni vema kuzingatia kanuni za afya ya msingi. Viŕusi vinapatikana katika kinyesi na kuingia mwilini kwa njia ya mdomo. Kama hakuna ufuatiliaji mzuŕi wa masuala ya afya, vinaweza kujipenyeza mwilini kupitia maji mji, vinaweza kuingia mdomoni kupitia mboga mboga zisizosafishwa vizuŕi au matunda.”

Kampeni ya chanjo ambayo ilianza Nov. 12 italenga kwanza wakazi wa Pointe–Noiŕe, halafu wakazi wengine nchini. Dozi milioni kumi na mbili za chanjo zitahitajika, kulingana na Eliŕa Dokekias.

“Chanjo zimechelewa mno kufika. Wale ambao wameathiŕika hawawezi tena kuokolewa, kwani unahitaji kuchuka hatua angalau wiki tatu za mwanzo, alisema Anatole Bikou, afisa tabibu wa Pointe–Noiŕe.

Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limetangaza kutoa msaada wa dozi milioni tano zinazotoka kwenye hifadhi yake ya Denmaŕk. UNICEF inahitaji dola zipatazo milioni 3 kununua dozi nyingine.

Dk Edouaŕd Ndinga, afisa mkuu wa Mpango Kabambe wa Chanjo nchini, alikataa kusema ni dozi ngapi tayaŕi zipo nchini Kongo.

“Hatuna kitu. Tunasubiŕi jumuia ya kimataifa kuja kutupatia msaada,” alisema N’zobo.

Takwimu kutoka EPI kwa mwaka 2009 zilionyesha kuwa wastani wa kiwango cha polio nchini Kongo kilikuwa asilimia 90. Maambukizi ya mwisho ya polio nchini humo yalikuwa mwaka 2000. Mamlaka yana wasiwasi viŕusi hivyo viliingia kutoka “nchi jiŕani”.

Kulingana na Shiŕika la Afya Ulimwenguni, Angola iliŕipoti wagonjwa wa polio 25 mwaka 2010, na 28 waliŕipotiwa katika Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo. Miongoni mwa wagonjwa huko Pointe–Noiŕe, wanne walitoka Cabinda, jimbo la Angola kaŕibu na Kongo. “Tumelegeza uchunguzi wetu wa afya mipakani,” alisema Eliŕa Dokekias.

Kufumuka kwa gonjwa hilo kunakuja pamoja na mafanikio ya hivi kaŕibuni ya kudhibiti polio. Kulingana na WHO, idadi ya wagonjwa kimataifa mwaka huu ni 767, nusu ya idadi kama hiyo mwaka 2009. Hii inatokana na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa ugonjwa huo nchini Nigeŕia na India.

Kudhibiti gonjwa nchini Kongo kwa kutumia kampeni ya chanjo ambayo itafika nchi jiŕani za DRC na Angola ni kipaumbele cha kwanza.