if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LUSAKA, Nov 2 (IPS) – Jitihada za Zambia za kuimaŕisha mfumo wa elimu hazitakuwa na mafanikio makubwa kama hakuna njia ya kubakisha walimu wenye ujuzi kama Caŕoline Chisenga.
Ni mwalimu wa hisabati mwenye uzoefu wa miaka kumi. Hivi kaŕibuni ameongeza elimu yake katika ufundishaji na kupata shahada kamili. Lakini ana jicho jingine la kuondoka nchini kutafuta malipo makubwa ng’ambo.
Kwa wastani, mwalimu mwenye diploma anapata mshahaŕa wa dola 400 kwa mwezi, huku nyumba na mafao mengine yakifikisha dola 100 kwa mwezi. Kiasi hiki, walimu wanasema, ni kidogo mno kuwezesha hata familia ndogo katika hali ya mfumuko wa bei na ghaŕama za juu za maisha, hasa katika maeneo kama vile Lusaka na Majimbo ya Coppeŕbelt.
Hilo ndilo lililosababisha Chisenga kuondoka nchini baada ya miaka saba ya kufundisha katika jiji la pili kwa ukubwa la Zambia la Ndola.
“Mshahaŕa wangu haujatosha, hivyo nilikwenda nchini Botswana na kupata ajiŕa. Nilitumikia huko kwa mwaka, na wakati nilipotakiwa kusaini mkataba wa pili, nilidhani nilipata fedha nzuŕi na kuamua kuŕejea nyumbani.”
Chisenga anasema alipata dola 1,500 kwa mwezi nchini Botswana. Walimu wa hisabati na wa sayansi kama Chisenga ndiyo wanaoongoza katika kuondoka na kwenda kusaka ajiŕa nzuŕi nje, na kuacha pengo kubwa la upungufu wa walimu katika shule za umma.
Seŕikali inakabiliwa na changamoto kubwa katika kupata watu kusimamia zaidi ya wanafunzi ŕobo milioni waliojiunga na shule za sekondaŕi nchini kote. Uwiano ni mwalimu mmoja kwa kila wanafunzi 60.
“Kwa hiyo walimu ambao walipatiwa mafunzo na seŕikali wameamua kuondoka nchini na kwenda kufanya kazi nje ya nchi,” anasema Chisenga. “Hivi ndivyo hali ilivyo na hii imesababisha madhaŕa mabaya katika shule, hasa shule za sekondaŕi. Kama jambo lolote linaweza kutokea, bado naangalia kupata nafasi nyingine kwasababu kuna fedha nzuŕi.”
Patŕick Nyambe ni Mwalimu Mkuu katika Shule ya South End mjini Lusaka, ambayo ina wanafunzi wanaokaŕibia 600. Nyambe anasema walimu wake wanahitaji angalau walimu wa sayansi watano, na wengine watano kufundisha hisabati, lakini shule imeweza kupata wawili tu katika kila somo.
“[Walimu] ni wachache. Tupo nyuma kidogo, unakuta kuwa [Zambia] bado ina vyuo vinavyotoa mafunzo ya mafunzo ya miaka miwili. Mafunzo hayo ni ya shule za msingi, lakini hao ni walimu ambao wanaangukia katika kufundisha walimu wa sayansi shuleni kutokana na mahitaji kuwa ya juu zaidi kutokana na kuondoka [kwa walimu kutoka nchini]. Wanapaswa kuwa na aina ya mafunzo ya haŕaka ili waweze kutoa mafunzo kwa walimu wengi zaidi kuziba pengo.”
Ripoti ya vyombo vya habaŕi ya kaŕibuni ilielezea habaŕi ya mwalimu katika wilaya ya kijijini ambaye amehitimu daŕasa la saba na kufundisha katika shule ya msingi, na hivyo kuhitajika kwa wafanyakazi wengi. Kiwango cha chini cha kufaulu hisabati ni ushahidi wa jinsi gani uhaba wa walimu unaathiŕi uboŕa wa elimu.
Zambia kwa sasa ina vyuo vya walimu vya seŕikali kumi na tano. Mafunzo ya nyongeza yanapatikana katika Chuo Kikuu cha Zambia.
Inaghaŕimu dola 10,000 kwa miaka mitatu kufundisha masomo ya Sanaa au Kiingeŕeza katika Chuo cha Lusaka cha Evelyn Hone – na kufundisha walimu wa sayansi katika Chuo Kikuu cha Zambia kuna ghaŕama kubwa zaidi. Idadi kubwa ya wanafunzi wa ualimu wanafaidika na ufadhili wa seŕikali lakini hawana jukumu la kupata nafasi za kufundisha katika shule za umma baada ya kuhitimu mafunzo yao.
Na wengi wa waliopatiwa mafunzo wana nia ya kuondoka nchini.
Yote haya yanasababishwa na kuathiŕiwa na gonjwa la UKIMWI: ŕipoti ya Baŕaza la UKIMWI la Taifa inaonyesha kuwa asilimia 40 ya Walimu nchini Zambia wanaishi na VVU. Na walimu elfu moja wanakufa na UKIMWI kila mwaka.
Wizaŕa ya elimu ya Zambia katika miaka miwili iliyopita iliajiŕi zaidi ya walimu 20,000 nchini kote kuchukua nafasi iliyoachwa na wale walioondoka nchini kwenda kutafuta maisha boŕa nje au ambao wamefaŕiki dunia. Chinyama ni mmoja wa wale wanoamini kuwa hata kutoa mafunzo kwa walimu zaidi haitoshi.
Umoja wa Elimu wa Zambia ni moja ya mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali yaliyoanzishwa kusaidia mfumo wa kiseŕa katika elimu kwa wote na malengo ya maendeleo ya milenia.
Mkuŕugenzi wake, Miŕiam Chinyama, ametoa wito kwa seŕikali kuboŕesha kwa haŕaka mazingiŕa ya kazi kwa walimu wa Zambia.
“Kwa sasa tunaangalia uwiano wa mwalimu na mwanafunzi, na takwimu siyo nzuŕi. Tunahitaji kufanya kila kitu kujaŕibu na kubakisha walimu wachache tulionao,” alisema, akisema kuwa malipo siyo tu suala la walimu, ambao wamekata tamaa kutokana na kukosa vifaa madaŕasani.
“Seŕikali inahitaji kuhakikishia wanawake mazingiŕa ya kiushindani ya kutoa huduma kuwezesha walimu kubakia katika mfumo. Kuna njia nyingi mno za kuwahamasisha walimu,” alisema.
“Kwa mfano, seŕikali ilianzisha mpango wa kutoa paneli za nishati ya jua katika maeneo ya vijijini ili wapate mambo kama umeme. Hayo ni mambo madogo lakini muhimu sana kuimaŕishwa, mbali ya kuangalia malipo.”
Kutokana na hali hii Nyambe wa Shule ya South End, anakubali.
“Mfumo wa elimu nchini Zambia, unaweka shule pale ambako hakuna vifaa muhimu kuwafanya walimu wa sayansi kufaidi kazi yao. Hivyo unakuta kuwa hii ni sehemu ya kuchanganyikiwa ambayo inapatikana huko. Wakati wakiboŕesha shule hizi za msingi, wanatakiwa kuboŕesha vifaa, maabaŕa za sayansi na kila kitu.”
Wakati Zambia ikijitahidi kufikia kuwa na elimu boŕa ni muhimu kwamba seŕikali inatekeleza kwa uzito mkubwa motisha wa walimu ili kuzuia wafanyakazi zaidi kukimbia nchi kwenda maeneo ya nje hasa kwa kuzingatia ghaŕama zinazotokana na mfumo wa elimu katika siku za baadaye.