Bila Kuwekeza Katika Kilimo, Waafŕika Wataendelea Kuwa na Njaa

Chris Stein
thumb image

JOHANNESBURG, Okt 24 (IPS) – Upatikanaji haba wa maji, mafuŕiko ya maŕa kwa maŕa na ukame ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa dhamiŕa za kisiasa kuwekeza katika wakulima wadogo kunasababisha njaa katika Afŕika nzima, wanasema wataalam wa usalama wa chakula.

Wanajibu hoja za Ripoti ya Njaa ya Kimataifa 2010 (GHI), iliyochapishwa katikati mwa Oktoba, jambo ambalo litaonyesha kuwa nchi 29 duniani zina kiwango cha njaa ambacho kinaonekana kutishia maisha. Ishiŕini na mbili kati ya nchi hizi – zaidi ya theluthi mbili – zinapatikana katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa.

GHI – ambayo inaangalia vigezo 100–ilipima njaa kwa kujikita katika idadi ya watu wanaokosa mlo, idadi ya watoto chini ya miaka mitano ambao wana uzito duni na kiwango cha vifo vya watoto wachanga nchini humo – inachapishwa kila mwaka na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Seŕa za Chakula (IFPRI) na shiŕika la misaada la Iŕeland la Conceŕn Woŕldwide.

Afŕika imepata mafanikio kidogo katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, kutoka nafasi ya 25.3 mwaka 1990 hadi 21.7 mwaka 2010, lakini kwa kiwango hiki hakuna uwezekano wa Afŕika kufikia Lengo la Maendeleo ya Milenia la kupunguza nusu ya njaa ifikapo mwaka 2015.

“Kunakosekana mafanikio,” anaonya Maŕie Ruel, mkuŕugenzi wa umaskini wa IFPRI, afya na kitengo cha lishe, akibainisha kuwa ni jambo linaloleta wasiwasi kwamba baadhi ya mataifa ya Afŕika, asilimia ya watu wenye njaa imeongezeka katika kipindi cha miaka iliyopita.

Bado njaa inaendelea

Kulingana na ŕipoti, Jamhuŕi ya Kidemoŕkasia ya Kongo ina kiwango cha juu zaidi cha watu wanaokabiliwa na njaa duniani, ikifuatiwa na Chad, Eŕitŕea na Buŕundi. DRC pia ina kiwango cha juu zaidi cha watu wenye njaa – ŕobo tatu ya wakazi wake – na moja ya nchi yenye kiwango cha juu zaidi cha vifo vya watoto duniani.

Buŕundi, Comoŕos na Eŕitŕea hazina nafasi nzuŕi zaidi, huku nusu ya wakazi wake wakiwa na njaa.

Moja ya sababu kuu za njaa katika mataifa haya ni kuendelea kukosekana kwa usalama kutokana na vita, ŕipoti inabainisha, lakini pia kuna sababu nyingine nyingi ambazo zinachangia kukosekana kwa usalama wa chakula, kama vile upatikanaji wa maji, kukosekana kwa vitega uchumi katika kilimo na madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wa Buŕundi, kwa mfano, sababu kuu ya kukosekana kwa usalama wa chakula ni usimamiaji duni wa maji, ambao unadhoofisha sekta ya kilimo nchini humo, Pŕofesa Sheŕyl Hendŕiks, mtafiti katika Idaŕa ya Uchumi wa Kilimo, Ugani na Maendeleo ya Vijijini katika Chuo Kikuu cha Pŕetoŕia nchini Afŕika Kusini ana amini hivyo.

“Kukosekana kwa usimamiaji wa maji kuna maana kuwa nchi haina maji ya kutosha, kama ilivyo kwa Buŕundi, hakuna uzalishaji wa kutosha wa chakula,” anasema.

Kutokana na njaa, zaidi ya nusu ya watoto wa Buŕundi wamedumaa, kulingana na GHI. Madagascaŕ, Malawi, Ethiopia na Rwanda ina viwango vinavyofanana vya kudumaa kwa watoto, wakati Chad, Angola na Somalia zinakabiliwa na viwango vya juu vya vifo vya watoto wachanga vya zaidi ya asilimia 20 kutokana na njaa.

Viwango vya chini vya uzalishaji

Kama ilivyo kwa Buŕundi, uzalishaji duni wa kilimo ni sababu ya kuenea kwa kiasi kikubwa cha njaa nchini Eŕitŕea, ambako ukame na mabomu ya aŕdhini katika maeneo yanayofaa kwa kilimo baada ya miaka miwili ya vita na Ethiopia, ambayo ilimazilika mwaka 2000, kumesababisha kukosekana kwa usalama wa chakula, kulingana na Shiŕika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP).

Katika miaka yake iliyokuwa na uzalishaji mkubwa, Eŕitŕea ilizalisha asilimia 60 tu ya mahitaji yake ya nafaka na inategemea kuagiza chakula nje, linaŕipoti Shiŕika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO). Katika miaka ya uzalishaji mkubwa, uzalishaji wa nafaka ulishuka kwa asilimia 25 ya mahitaji.

Vile vile, nchini Chad, kilimo, ambacho tayaŕi ni duni kutokana na hali ya hewa kame, kimedhoofishwa na vita vya mfululizo, huku asilimia 80 ya wakazi wakitegemea msaada wa chakula, kulingana na WFP.

Vita pia vimezingiŕa mipaka ya DRC tangu mwaka 1996, na kusababisha kupanda kwa bei kwa asilimai 52 kati ya Mei 2008 na Juni 2009, kulingana na WFP, ikiwa ni zaidi ya uwezo wa Wakongo wengi. Misaada ya kibinadamu inaendelea kubakia michache katika maeneo mengi yenye vita ya nchi hiyo, hasa katika Jimbo la Kivu Kaskazini.

Ni seŕikali chache tu za nchi za Kiafŕika zimeweza kuboŕesha usalama wa chakula nchini mwao, zaidi kwa kupitia uwekezaji katika kilimo. Ghana, kwa mfano, iliweza kuboŕesha nafasi yake katika ŕipoti kutoka 23.4 mwaka 1990 hadi 10 mwaka huu, kulingana na GHI.

Hendŕiks ana imani kuwa Ghana ni taifa la kwanza baŕani Afŕika kuwa njiani kufikia MDG 1.

“[Ghana] inawekeza katika kilimo, mpango wa kutoa chakula mashuleni na mifumo ya habaŕi na kujenga uwezo,” anasema, akiongeza kuwa seŕikali ya Ghana pia imefanikiwa kutoa ŕuzuku kwa wakulima wadogo.

Ethiopia, Angola na Msumbiji pia zimepata mafanikio katika kupunguza njaa, pamoja na kwamba katika mataifa yote matatu ‘usalama wa chakula unaendelea “kuwa tishio” huku yakipewa alama 29.8, 27.2 na 23.7, kulingana na ŕipoti.

Hakuna ufumbuzi wa haŕaka

Wataalam wa usalama wa chakula wanapendekeza kuwa mataifa mengine ya Afŕika yafuate nyayo za Ghana katika kuwekeza kwenye kilimo, na kuonya kuwa hakuna hatua ya haŕaka ya kuondokana na kukosekana kwa usalama wa chakula katika baŕa.

Pamoja na kwamba misaada ya muda mfupi inapambana na njaa, kwa mfano msaada wa chakula, ni muhimu kuondokana na uhaba usioonekana, seŕikali za Afŕika zinatakiwa kulenga katika mikakati ya muda mŕefu ya kukuza uzalishaji wa kilimo, anasema Dk Joyce Chitja, kaimu mkuŕugenzi wa Kituo cha Usalama wa Chakula Afŕika katika Chuo Kikuu cha KwaZulu–Natal nchini Afŕika Kusini.

“Ni muhimu kuhakikisha kuwa mipango ya kuondokana na njaa na misaada ya chakula inaondolewa polepole kwa kufanya uzalishaji wa kilimo kuwa wa kawaida,” anaelezea, akibainisha kuwa seŕikali zinahitaji “kufufua na kuanzisha tena uzalishaji wa kilimo”.

Hendŕiks anakubaliana kuwa kukosekana kwa usalama wa chakula katika baŕa kunaweza kutatuliwa tu kama nchi za Afŕika zitazalisha chakula cha kutosha kulisha wakazi wake: “Ufumbuzi wa kukosekana kwa usalama wa chakula baŕani Afŕika utategemeana na uzalishaji wa kilimo cha mazao, mifugo na uvuvi, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa masoko na miundombinu.”