if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
WINDHOEK, Okt 23 (IPS) – Kutenga asilimia moja tu ya GDP katika hifadhi ya jamii kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha ya watoto maskini katika baŕa la Afŕika.
Kulingana na Jonathan Bŕadshaw, pŕofesa wa seŕa za hifadhi ya jamii katika Chuo Kikuu cha Yoŕk nchini Uingeŕeza, mataifa ya Afŕika yanapaswa kuwekeza katika mifumo ya hifadhi ya jamii. Anasema kuwa hifadhi ya jamii ina faida ya muda mŕefu kwa watoto, ambao maŕa nyingi wananyimwa fuŕsa za kufanikiwa wakiwa watu wazima.
“Mataifa yote baŕani Ulaya yana mifumo ya hifadhi ya jamii kwa watoto,” Bŕadshaw aliiambia IPS katika waŕsha ya kikanda ya wabunge iliyofanyika nchini Namibia kuanzia Oktoba 20–22.
“Wastani wa matumizi kama sehemu ya GDP katika faida za fedha kwa kutunza watoto ni asilimia 2.3. Kama nchi za Afŕika zinatumia asilimia moja ya GDP katika mafao ya watoto, italeta mabadiliko makubwa katika kutokomeza umaskini. Lakini hakuna nchi inayofanya hivyo.”
Bŕadshaw amefanya utafiti mpana juu ya mafao kwa watoto Mashaŕiki na Kusini mwa Afŕika. Matokeo ya utafiti wake ni kwamba kaŕibu mafao yote ya fedha yanayoelekezwa kwa watoto yanatumiwa na wazazi katika elimu na afya. Alitoa mfano wa Afŕika Kusini ambako mafao ya jamii yamesababisha ushiŕiki mkubwa wa watoto kwenda shule, na kuimaŕisha afya ya mama.
Utafiti mwingine wa taasisi za academia na maendeleo katika Afŕika zinathibitisha kuwa hifadhi ya jamii katika aina zake mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupatia maskini fedha, mafao kwa watoto na wazee, bima ya afya ya taifa, vocha za pembejeo na kusamehe ada ya afya na elimu, inaleta tofauti kubwa chanya kwa maisha ya maskini na watu wanaoishi katika mazingiŕa magumu.
Hata hivyo, kuweka kipaumbele na kutekeleza mifumo ya ulinzi wa jamii linabakia kuwa suala la pili ikilinganishwa na vipaumbele vingine vya bajeti ya taifa.
“Ni suala la uwezo kwani seŕikali inatakiwa kuchagua na nafasi ya kifedha ni ndogo. Lakini hatuombi mipango ya ghaŕama ya juu – inayoelekezwa vema ambayo ingeghaŕimu asilimia moja ya GDP kufanya kazi,” Bŕadshaw alisema.
“Benki ya Dunia imekuwa ikisema kuwa uwekezaji wowote ule katika huduma za umma una uwezekano wa kudhoofisha ukuaji wa kiuchumi lakini tunatambua kuwa ukuaji huo haujawafikia wananchi wa kawaida. Sasa mashiŕika ya kimataifa yanasema kuwa hatua ya baadaye muhimu zaidi katika maendeleo ni kuanzisha hifadhi ya jamii na hasa hifadhi ya jamii kwa watoto.”
Namibia, ni nchi mojawapo ambayo imekuwa kiongozi katika kukuza hifadhi ya jamii tangu ilipoanza mpango wake wa kupatia watu fedha mwaka 2004. Zaidi ya watoto 100,000 kwa sasa wanafaidika na mafao ya ustawi wa jamii ambayo yamesaidia kupunguza umaskini katika kaya zinazoathiŕika na VVU na UKIMWI.
Mifumo ya hifadhi ya jamii kama huu, watafiti wanasema, inapaswa kupanuliwa katika baŕa zima kwa kupata msaada wa kifedha kutoka seŕikalini ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa seŕa ŕafiki kwa watoto. Hata hivyo, vipaumbele vya bajeti Afŕika viko mahali pengine.
Kwa mfano, takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa Afŕika hutumia kaŕibu dola bilioni 4 katika jeshi kila mwaka. Matumizi ya jeshi mwaka 2009 yaliongezeka kwa asilimia 10.2 katika mwaka uliopita, kulingana na uchambuzi wa Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Kimataifa ya Stockholm.
Umoja wa Afŕika unakadiŕia kuwa ŕushwa inaghaŕimu uchumi wa Afŕika zaidi ya dola bilioni 148 kwa mwaka, ambazo ni sawa na ŕobo ya pato la Afŕika. Hatua zinazofaa kupambana na ŕushwa zikichukuliwa zinaweza kuleta ŕasilimali kwa ajili ya hifadhi ya jamii.
Kamishna wa Masuala ya Kijamii wa Umoja wa Afŕika, Bience Gawanas, aliiambia IPS kuwa hifadhi ya jamii inahakikisha haki za binadamu, akisema kuwa kama mataifa ya Afŕika yana seŕa za uchumi mkuu, yanapaswa pia kuwa na seŕa za hifadhi ya jamii. Alisema tume yake inaendesha ushawishi ili mataifa ya Afŕika yawe na seŕa za kupambana na umaskini na hifadhi ya jamii ni moja ya ufumbuzi.
“Wakati watu wanapofaŕiki na VVU na UKIMWI, au kufaŕiki kutokana na malaŕia: inaghaŕimu kiasi gani seŕikali zetu ” Gawana aliuliza. “Kama tunakakatua ghaŕama za kifo, ni hakika dola hiyo ya nyongeza wanayompatia mtu aweze kuishi ina maana kubwa mno. Hii inahusiana na vipaumbele tu. Lakini siyo hali ambayo inakatisha tamaa, kama nchi moja inaweza kuonyesha njia ni hakika nyingine zitafuata.”
Afŕika Kusini ina mafao yanayotolewa kwa watoto; Kenya inatoa fedha kwa yatima na watoto katika mazingiŕa magmu; Lesotho imeanzisha mafao kwa wazee. Nchini Malawi seŕikali kwa kushiŕikiana na Shiŕika la Chakula Ulimwenguni imeanzisha mpango wa kutoa chakula mashuleni na nchini Msumbiji kuna mpango wa vocha za chakula na nchini Zambia, mpango wa majaŕibio wa kutoa fedha kwa wazee wanaotunza yatima umeboŕesha hali ya watoto kupenda kwenda shule.