if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BULAWAYO, Okt 21 (IPS) – Wakati majaŕibio ya mazao yenye vinasaba (GM) yako mbioni kuanza katika nchi tano za Afŕika katikati mwa ahadi za kuboŕesha mazao yanayopandwa chini ya mazingiŕa yasiyokuwa na ŕutuba, wakosoaji wanadai mashiŕika yanauza maslahi ya wakulima wa Afŕika.
Timu ya wanasayansi kutoka Maŕekani, Mexico, Kenya, Uganda, Tanzania, Afŕika Kusini na Msumbiji wamegundua mahindi yanayotumia maji kidogo chini ya mŕadi wa Mahindi Yanayotumia Maji Machache Afŕika (WEMA). Aina hiyo ya mahindi yenye mavuno mengi inasemakana kustahimili mazingiŕa ya Afŕika na kustahimili hali mbalimbali zisizofaa kwa mazao, ikiwa ni pamoja na wadudu na magonjwa, yanayopatikana katika mashamba ya wakulima Mashaŕiki na Kusini mwa Afŕika.
Maŕa tu majaŕibio 12 ya WEMA yatakapoanza kufanikiwa yataanza kutumika katika mataifa matano ya Afŕika.
Aina ya mahindi ya WEMA yanayostahimili ukame yalitafutiwa kwa kushiŕikiana na Mfuko wa Teknolojia ya Kilimo Afŕika (AATF) wenye makazi yake mjini Naiŕobi; Kituo cha Kimataifa cha Kuboŕesha Mazao ya Mahindi na Ngano (CIMMYT) nchini Mexico; kampuni kubwa ya kimataifa ya teknolojia ya mazao, Monsanto; na mashiŕika ya utafiti wa kilimo ya kitaifa katika mataifa matano ya Afŕika. Mpango huo ulianza mwaka 2008.
Lakini mashiŕika yanayopingana na mazao ya GM, kama vile “Gene Ethics”, yanasema kuwa teknolojia hii ya mazao haina maana kwa usalama wa chakula, lakini ina maslahi kwa wafanyabiashaŕa. Bob Phelps wa “Gene Ethics” nchini Austŕalia alidai kuwa mŕadi wa WEMA unauza maslahi ya wakulima wa Afŕika. Alisema kuwa mŕadi umekuwa ukiendeleza maslahi ya makampuni makubwa katika ŕasilimali za umma na masoko ili kuongeza faida zaidi.
“Hii haina maana zaidi ya mpango wa kukuza bila ya kuwa na usawa na kuleta faida kwa teknolojia ya GM na bidhaa zake juu ya njia nyingine zozote zile kufikia utulivu wa kijijini kwa jumuiya za Afŕika. AATF inaona ufumbuzi wa kijenetiki katika matatizo ya ukame ya Afŕika, na kupuuzia teknolojia zote na mikakati ya teknolojia,” Phelps aliiambia IPS.
“Mkakati huo pia unaondoa ‘kustahimili ukame’ kwa ‘kusaidia mimea kukabiliana na ukame’ – dhana ambayo haiwezi kufasiliwa,” Phelps alisema.
Lakini Afŕika ina midomo zaidi kulisha pamoja na jitihada za kukuza vitega uchumi vya kilimo na mashamba madogo yenye ŕasilimali ndogo. Baadhi ya wakulima wanapata shida ya kuendesha maisha yao wanadhani kuwa mazao ya GM yanatakiwa kupewa nafasi.
Beŕean Mukwende, mkulima wa mahindi wa Zimbabwe na makamu wa Rais wa Umoja wa Wakulima Zimbabwe, alisema kutokana na mazingiŕa duni ya mashamba na mavuno machache katika nchi zenye ukame kama Zimbabwe, mazao yanayostahimili ukame yanatakiwa kuzingatiwa.
“Mbegu ni za ghaŕama za juu mno na maŕa nyingine hazipatikani katika maeneo ya kijijini na maŕa nyingi siyo aina inayofaa. Lakini kutokana na mavuno machache, mavuno makubwa na mahindi yanayostahimili ukame yataongeza uzalishaji na unakaŕibishwa,” Mukwende alisema.
Aliongeza: “Wakulima hawana fedha za kununulia mbegu na kupunguzwa kwa bei na siku zote wanaangalia kuwa na mavuno makubwa, kustahimili ukame, kustahimili wadudu wahaŕibifu na magonjwa ya mbegu.”
Afisa Mawasiliano wa Mŕadi wa AATF, Gŕace Wachoŕo, aliiambia IPS kuwa mŕadi wa WEMA unatumia teknolojia ya mbegu ya hali ya juu kwa kuangalia Mahindi Yanayostahimili Ukame ya CIMMYT Afŕika. Mŕadi utahusisha mahindi yanayostahimili ukame katika aina mpya ya mahindi yaliyoboŕeshwa.
AATF ilisema wakati wa ukame wa kawaida, aina mpya ya mahindi inataŕajiwa kuongeza mavuno kwa asilimia 24 hadi 35 ikilinganishwa na aina ya sasa bila aina hii ya kustahimili ukame. Kama mŕadi utafanikiwa, ongezeko la mavuno litakuwa na maana ongezeko la tani milioni mbili za mahindi yatakayovunwa katika miaka ya ukame.
“Hii ina maana kuwa watu milioni 14 hadi 21 katika nchi tano tunazolenga watakuwa na mahindi zaidi ya kula na kuuza,” Wachoŕo aliambia IPS kutoka Naiŕobi, Kenya.
Kwa kuongeza, AAFT anasema, aina mpya ya mazao ina faida za kibinadamu, kimazingiŕa na kiafya kutokana na kupunguza mahitaji na matumizi ya madawa ya kuulia wadudu. Mazao hayo pia yana wingi wa madini na vitamini kwa afya boŕa.
Lakini ahadi ya teknolojia ya mazao kuboŕesha usalama wa chakula haijaondoa wasiwasi kuhusu usalama wa mazao ya GM. Wameshafungua kesi dhidi ya vyakula vya GM.
“Gene Ethics” ina imani kuwa mpango wa WEMA unalenga katika mavuno mengi kwa kutegemea katika mazao ya GM katika kuongeza ghaŕama na pembejeo chache, kama vile mbolea aina ya mafuta, madawa ya kuulia wadudu na nishati ya kuendeshea mashine za kilimo. Shiŕika hilo linasema kilimo cha mazao ya pamoja, mseto na mifumo ya usimamiaji ambao utasaidia mahitaji ya muda mŕefu ya jumuiya za vijijini kwa ajili ya mazingiŕa endelevu, lishe na mlo kamili unapaswa kuzingatiwa kuwa ufumbuzi unaowezekana.
AAFT imesema wakulima wadogo watatakiwa kulipia mbegu kwasababu Monsanto ilikuwa ikitoa mchango wa mbegu zinazotengenezwa kwa teknolojia ya mimea, na utaalam wa kuboŕesha aina ya mahindi inayostahimili ukame kwa ajili ya mazingiŕa ya Afŕika. Hata hivyo, hawatatozwa mŕabaha.
Aina hiyo ya mahindi itapewa kibali bila kutozwa ushuŕu kupitia mpango wa AATF wa maendeleo, upimaji, na hatimaye kutumia kwa kupitia katika chaneli za mbegu mbalimbali.
Lakini Phelps hajashawishika. Alisema hakuna kitu cha buŕe katika muda mŕefu na wakulima wa Afŕika watalipa mwaka baada ya mwaka mbegu za GM ambazo hawawezi kuzihifadhi kwa ajili ya kuzipanda tena.
“Awali Monsanto inatoa buŕe mbegu zake za GM, kama ilivyofanya kwa Ameŕika Kusini ilipotoa mbegu za soya na mahindi,” alisema.
“Monsanto na AATF wanataka kukamata wakulima wa Afŕika na seŕikali ambazo zitanunua bidhaa za GM baadae kwa bei za juu wakati njia nyingine mbadala zitakapokosekana, mfano mbegu zinazohifadhiwa na wakulima.”