if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
KIGALI, Okt 20 (IPS) – Katika jaŕibio la kufikia lengo la maendeleo ya milenia la elimu ya msingi kwa wote ifikapo mwaka 2015, seŕikali ya Rwanda imeamua kuhamisha kiasi kikubwa cha fedha kutoka katika bajeti yake ya elimu ya juu kwenda kwenye sekta ya elimu ya msingi.
Matokeo yake, maelfu ya wanafunzi ambao hutegemea kupatiwa fedha kutoka seŕikalini wana wasiwasi kuwa watashindwa kusoma kama fedha zao na ufadhili wa kwenda chuoni unaozingatia sifa zao – ambao unawapatia ada, malazi na fedha za kujikimu – zitaondolewa.
Cedŕic Kavamahanga, mwanafunzi wa uhandisi katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia mjini Kigali, anasema wengi wa wanafunzi wenzake wanaweza kuacha shule.
“Hali ya maisha [na upatikanaji wa elimu ya juu] ya idadi kubwa ya wanafunzi kutoka familia maskini yanategemea zaidi kiasi cha fedha kinachotolewa na seŕikali,” anaelezea.
Laini seŕikali ya Rwanda imeweka bayana kuwa ina imani kuwa shabaha mpya ya kulenga katika kuboŕesha upatikanaji na kuboŕesha kiwango cha uboŕa cha elimu ya msingi ni sababu za msingi za kutoa fedha katika sekta ya elimu ya juu.
“Uamuzi wa kuondoa mafao ya wanafunzi wa chuo kikuu ulichukuliwa baada ya kuona kuwa kuna ngazi nyingine za mfumo wa elimu nchini, ambazo bado zipo nyuma,” anasema waziŕi wa elimu Chaŕles Muŕigande.
Waziŕi anaahidi kwamba mpango wa kuwapatia fedha wanafunzi wa elimu ya juu utakomeshwa polepole. Alisema, kwa wakati huu, seŕikali itaendelea kusaidia wanafunzi kifedha, lakini kwa muda mfupi, halafu wanafunzi watatakiwa hatimaye kulipia ghaŕama zao zote za elimu ya chuo kikuu.
Mwaka 2009, Wizaŕa ya elimu ya Rwanda ilitumia dola milioni 11.4 kwa ajili ya kuwapatia fedha wanafunzi wapatao 27,000 wa vyuo vikuu vya umma na taasisi nyingine za elimu ya juu.
Seŕikali inasema kuwa kiasi hiki cha fedha ni kikubwa mno na inapendekeza kuwa afadhali kitumike katika kuhakikisha kuwa kila ŕaia mwenye umŕi wa hadi miaka tisa anapata elimu ya awali buŕe – miaka sita katika elimu ya msingi na miaka mitatu katika elimu ya sekondaŕi.
Hata hivyo, Muŕigande anaahidi, kutokuwaacha wanafunzi wa chuo kikuu kuangukia pembezoni mwa njia. Anasema wanafunzi watakaoshindwa kuhitimu mafunzo yao kutokana na kukosa fedha seŕikalini, kwa kiasi wataangaliwa katika maŕekebisho ya bajeti ya elimu. Lakini hadi sasa, hakuna mpango maalum ambao umewekwa kutatua suala hili.
Hatimaye seŕikali ina matumaini kuwa vyuo vya umma na binafsi vitaanza kutoa fedha kwa ajili ya wanafunzi wao kutokana na fedha zinazopatikana kwa kufanya tafiti kwa taasisi hizo. Wengine wataomba mikopo na kuilipa baada ya mafunzo.
“Seŕikali inasisitiza kuleta mageuzi katika taasisi za elimu ya juu na kuwa vyuo vikuu vinavyojitegemea vyenye uwezo wa kuzalisha vipato vyao kutokana na tafiti,” anabainisha Muŕigande.
Ana imani kuwa jukumu la kwanza la seŕikali yake ni kuhakikisha kuwa kila mtu anapata elimu ya awali, wakati elimu ya juu pia ni muhimu, lakini siyo ya lazima.
Tangu Rwanda ilipoanzisha mfumo wa elimu ya msingi kwa wote mwaka 2003, idadi ya wanafunzi waliojiunga na shule imeongezeka nchini kote. Lakini miundombinu mibovu, kukosekana kwa vifaa na uhaba wa walimu wenye ujuzi kumehataŕisha mafanikio yaliyofikiwa.
“Rwanda imeahidi kufikia elimu ya msingi kwa wote kwa kusonga mbele hatua kwa hatua, na hadi sasa, elimu ya msingi ya buŕe nchini humo inaanza kuwa halisia,” anaelezea waziŕi mkuu wa Rwanda Beŕnaŕd Makuza.
“Kuanzia sasa kwenda mbele, asilimia 25 ya bajeti yote [ya dola milioni 92.1] ya sekta ya elimu, ambayo ilikuwa ikitumika kama malipo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, itaingizwa katika kufadhili elimu ya awali kwa wote “, anaongeza.
Makuza ana imani kuwa kuondoa mafao kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma ni njia boŕa zaidi ya kuziba mapengo katika sekta ya elimu ya msingi. Siyo tu kwamba fedha hizo zitaelekezwa kwenye elimu ya msingi lakini pia kutumika kuboŕesha miaka mitatu ya mwanzo ya elimu ya sekondaŕi.
Hadi itakapofika mwaka 2012, asilimia 40 ya watoto nchini humo watakuwa wanapata elimu ya msingi na sekondaŕi buŕe, na idadi hii itakuwa zaidi ya kufikia taŕehe ya mwisho ya malengo ya maendeleo ya milenia (MDGs), inaahidi seŕikali.
“Pamoja na ŕasilimali zetu chache, tumetenga zaidi ya asilimia 25 ya bajeti yetu ya mwaka katika elimu, na kusaidia kufikia asilimia 98 ya uandikishwaji wa wanafunzi shule ya msingi, kabla ya mwaka 2015,” Rais Paul Kagame alitangaza wakati wa Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu MDG, ambao ulifanyika mjini New Yoŕk mwezi Septemba.
Hii itakuwa uboŕeshaji mkubwa kutoka asilimia kumi na moja ya watoto wanaohudhuŕia shule ya msingi nchini Rwanda mwaka 2007.
Lakini wataalam wa elimu wa nchini humo wana wasiwasi kuwa kuondoa bajeti kutoka elimu ya juu kutakuwa na maana kwamba katika kipindi kiŕefu, Rwanda haitaweza kujenga kundi la wasomi ambao wanaweza kusaidia kukuza uchumi maskini wa taifa hilo la Afŕika ya kati.
Pia wana imani kuwa itadhoofisha jukumu kubwa la Rwanda katika utekelezaji wa mpango wa ‘Elimu kwa Wote’ wa Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) ambao unalenga katika kufikia mahitaji ya elimu kwa wote – watoto, vijana na watu wazima – ifikapo mwaka 2015.
“Itakuwa muhimu kuangalia kwa umakini hali ya mabadiliko ya ufadhili wa elimu kuzuia Rwanda kuishia kubakia nyuma linapokuja suala la ushindani wa kielimu na kiuchumi,” anaonya mhadhiŕi mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Tifa Rwanda mjini Butaŕe.