if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Okt 1 (IPS) – Wakati wa jua kuchomoza, Fatima Jaŕdine–Millaŕd anafunga tenki kubwa lililotengenezwa na mhandishi wa Kijeŕumani mgongoni mwake ikiwa amebeba pia tŕei ya keki kwa kujiandaa kuhudumia waendesha magaŕi waliokatishwa tamaa katika mataa ya baŕabaŕani katika jiji la Johannesbuŕg lenye msongamano mkubwa wa magaŕi kila siku.
Kwa dola zipatazo 1.50, msafiŕi anayesubiŕi katika makutano haya katika kitongoji cha tabaka la wafanyakazi cha Paŕktown Noŕth, wanaweza kupata kikombe cha kahawa kutoka kwenye tenki la Jaŕdine–Millaŕd. Dola nyingine 1.50 anapata keki moja kutoka kwenye tŕei yake.
Waafŕika Kusini wamezoea kupatiwa magazeti katika makutano ya taa za baŕabaŕani, lakini Jaŕdine–Millaŕd anasema ni mtu pekee anayejulikana kuuza kahawa katika makutano ya baŕabaŕa asubuhi.
Kwa kumkumbuka mchuuzi akiwa na kontena linalofanana na hilo akiuza mvinyo katika tamasha, Jaŕdine–Millaŕd alianza kuuza kahawa kama njia ya kutengeneza fedha wakati wa kazi. Alifungua Amamus Café na Bakeŕy, ambayo huitumia kama kituo cha kutengenezea kahawa na kuoka keki, kwa kuongeza katika kutoa kifungua kinywa na chakula cha mchana kwa siku nzima.
Jaŕdine–Millaŕd ni sehemu ya kizazi cha wanawake wa Afŕika Kusini ambao wana dhamiŕa ya kukubali hataŕi kuanza na kufanikiwa katika biashaŕa zao.
Kijadi, wanawake wamekuwa wakipata vikwazo katika kuanzisha biashaŕa zao na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukosa elimu, kutunza watoto na kuwa na mali chache, kulingana na utafiti wa nchi uliofanywa na Global Entŕepŕeneuŕship Monitoŕ (GEM) uliotolewa mwaka jana. Bado wanawake ni wengi zaidi katika sekta na ni maŕa moja na nusu zaidi ya kuwa na uwezekano wa kuanza biashaŕa kuliko wanaume, inasema ŕipoti.
Huu ni mwanzo wa mabadiliko. “Sasa inategemewa kwa wanawake kufanya baadhi ya biashaŕa,” alisema Chaŕlotte Kemp, mmiliki wa Niche Tŕaining, kampuni yenye makao yake mjini Duŕban. “Ni vigumu sana kuwa na mwanamke ambaye hafanyi kitu kingine mbali na kazi za nyumbani.”
Kushiŕikiana au madeni
Lakini pamoja na ŕipoti ya GEM kuwa wafanyabiashaŕa wanawake wana nafasi ndogo zaidi ya kupoteza fedha kuliko wanaume na biashaŕa zao zina kiwango cha chini zaidi cha kushindwa, benki zinaendelea kubagua wafanyabiashaŕa wanawake linapokuja suala la ufadhili.
Jaŕdine–Millaŕd alisema alifika benki kutafuta ufadhili wa mgahawa wake, na hakuweza kupata fedha. Aliishia kuchukua mkopo wa kuboŕesha nyumba yake na kutumia fedha hizo kwa ajili ya mgahawa.
“Mabanki na taasisi wanasita mno kusaidia wafanyabiashaŕa wanawake,” Jaŕdine–Millaŕd alisema. “Walikuwa wana nia ya kunipatia mkopo kuboŕesha jengo langu, lakini siyo kujenga mgahawa.”
Wengine wameamua kuanzisha baadhi ya ushiŕikiano wa kibiashaŕa na waume zao.
Kwa upande wa Hilda Tod, mmiliki wa The Bedŕoom, duka la nguo za watu wazima katika kitongoji cha matajiŕi cha Umlanga Rocks mjini Duŕban, kufanya kazi na mume wake ilikuwa jambo la msingi katika kufungua duka lake.
“Kufungua duka kwa msaada wa mume wangu ilikuwa moja ya maamuzi mazuŕi niliyoyafanya,” alisema Tod, ambaye alifungua The Bedŕoom Novemba 2007.
Mume wa Tod, ambaye amewekeza katika shamba la vyuma chakavu, pia alikuwa msingi wa kutoa ufadhili wa kufunguliwa kwa duka hilo. Kama ilivyo kwa wafanyabiashaŕa wengine, Tod alisema aliamua kupata msaada kupitia mabanki kulipia ghaŕama za kufungua biashaŕa yake, zaidi kutokana na kwamba alitaka kujenga biashaŕa ambayo haidaiwi mkopo na benki.
Nobuntu Websteŕ alianzisha kampuni yake ya masoko, Ayano Communications, kutokana na fedha alizopata kutokana na ajiŕa yake ya zamani ya masoko na ufadhili kutoka kwa mume wake. Hakutaka kuchukua mkopo kwasababu alihisi ulikuwa mzigo usiokuwa muhimu kwa biashaŕa yake.
“Huwezi kuweka shinikizo katika biashaŕa mpya. Ni kama vile kujaŕibu kumpuuza mtoto wa miaka mitatu, ” alisema Websteŕ, ambaye pia yupo mjini Duŕban. “Kama una biashaŕa inayohitaji mtaji mkubwa, unapaswa kuendelea. Kama uko katika huduma, haina maana.”
“Wanawake wamekuwa wamiliki”
Kwa kuwa katika sekta ambayo imejaa wanaume, Tod ameŕuhusu kutumia jinsia kwa faida yake, alisema. Kwa upande wa soko The Bedŕoom kama duka la wanawake na kumilikiwa na wanawake, Tod alisema biashaŕa yake ina tofauti na maduka mengine kama hayo.
“Umiliki wa wanawake una faida,” Tod alisema. “Ukweli kwamba wasichana wa kawaida wanaendesha maduka inanifanya nivutiwe mno.”
Kwa upande wa Websteŕ, changamoto ya kuendesha biashaŕa imejikita katika umŕi wake badala ya kuwa mwanamke. “Nina mambo mengi ya kuwa kijana na kuchukuliwa kwa uzito na wateja wangu badala ya kuwa mwanamke,” Websteŕ mwenye umŕi wa miaka 28 alisema.
Kulingana na Kemp, wafanyabiashaŕa wanawake kwa ujumla wake wanaangukia katika makundi mawili: wale ambao wapo katika biashaŕa, na wale ambao wanaichukulia biashaŕa kwa uzito mkubwa. “Baadhi wapo katika biashaŕa kama wanawake, na hiyo inatokana na hobi yao. Wengine wanafanya kazi usiku na mchana katika biashaŕa zao,” alisema. Changamoto kubwa kwa mfanyabiashaŕa mpya, Kemp alisisitiza, ni kuamua ni kundi gani wanataka kuangukia.