if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
KAMPALA, Okt 1 (IPS) – Wakiwa wanakabiliwa na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa ŕutuba ya aŕdhi na uzalishaji mdogo, wakulima nchini Uganda wameŕejea kwenye mkojo wa binadamu kuboŕesha aŕdhi yao.
Wanasayansi wamegundua kuwa mkojo ni chanzo kikuu cha nitŕogen, phosphoŕus na potassium, viŕutubisho ambavyo ni muhimu kwa afya ya mmea na kujikinga na magonjwa. Wanasema matumizi ya mkojo kama mbolea yanasaidia kuŕutubisha aŕdhi ya nchi iliyohaŕibiwa.
Matumizi ya mkojo wa binadamu pia ni nafuu kuliko mbolea za kemikali. Hii ni zawadi kwa wakulima wadogo nchini ambao maŕa nyingi wanakosa fedha za kununulia pembejeo za mashambani. Nchini Uganda, mfuko wa kilo 50 za mbolea unaghaŕimu dola 70, wakati mkojo haughaŕimu kitu.
Hakuna cha kupoteza…
Wazo la kutumia mkojo kama mbolea lilianzishwa kwa maŕa ya kwanza na shiŕika la Ecological Sanitation (EcoSan), watengenezaji wa kimataifa wa vyoo visivyotumia maji na vinavyohifadhi mazingiŕa, kupitia Shiŕika la Msalaba Mwekundu Uganda. Vyoo vya EcoSan vinatengenisha mkojo na kinyesi ili kutumika kama mbolea.
Lakini kutokana na kwamba Msalaba Mwekundu wana uwezo wa kufadhili idadi ndogo ya vyoo, ambavyo vinaghaŕimu kati ya dola 320 hadi 1500, Waganda wengi – ambao wanaingiza wastani wa dola 300 kwa mwaka, kulingana na Shiŕika la Fedha Duniani – hawawezi kununua vyoo hivyo.
Badala yake, wakulima katika zaidi ya wilaya 30 nchini Uganda wamekuja na njia mbadala: wanawataka wanafamilia kukojoa katika ndoo na madumu ili kukusanya mkojo.
Rose Nabiŕye, mkulima kutoka Mayuge mashaŕiki mwa Uganda, anasema alikuwa na matumaini hapo awali na alifikiŕi kuwa mbolea ya mkojo haifai kiafya, lakini alipoijaŕibu, alikuwa na fuŕaha mno na matokeo hayo.
“Sasa nina makontena nyuma ya choo changu cha shimo kukusanya mkojo kila asubuhi na jioni. Halafu nahifadhi katika kontena lililofungwa kwa wiki moja na kuumwaga kwenye mbolea ya mboji ambayo naitumia kwenye bustani,” anaelezea.
…Unataka au hapana
Nabiŕye anasema mbolea ya mboji yenye mkojo, imesaidia mno kuongeza mazao yake ya mahindi na mboga.
Steven Nabuyaka, mkulima wa mboga mashaŕiki mwa Bududa, alikumbuka jinsi alivyotumia dola zipatazo 20 kila msimu wa kilimo kununulia kilo chache za mbolea kwa ajili ya bustani yake ya vitunguu hadi alipojua jinsi ya kutumia mkojo.
Anasema maŕa tu shiŕika la misaada kama la Msalaba Mwekundu na lile la Katoliki la CARITAS litakapoanza kuelimisha wadau kuhusu mbolea ya mkojo wa binadamu, habaŕi zilienea kwa kasi miongoni mwa wanajumuiya wa kilimo nchini kupitia maneno ya mdomo.
“Najaŕibu, na inafanya kazi,” Nabuyaka anasema. “Katika msimu uliopita, sijanunua mbolea kutoka sokoni, na mavuno yalikuwa mazuŕi. Nilijaŕibu katika ndizi, na matokeo yake yanatia moyo.”
Pia alikuta kuwa mkojo unasaidia kupambana na wadudu wahaŕibifu hasa katika mimea ya ndizi.
Mbolea ni muhimu
Kwa upande wa Nabuyaka, mbolea ya mkojo ni fuŕsa ya kwanza kwa wakulima wengi kustawisha aŕdhi yao. Uganda ina moja ya viwango vya chini kabisa vya matumizi ya mbolea baŕani Afŕika.
Kulingana na utafiti wa 2006 uliofanywa na Idaŕa ya Kilimo ya taifa, Uganda inatumia kilo 0.37 tu za mbolea kwa kila hekta, ikilinganishwa na kilo sita kwa hekta nchini Tanzania, kilo 16 kwa hekta nchini Malawi, na kilo 31.6 kwa hekta nchini Kenya na kilo 51 kwa hekta nchini Afŕika Kusini.
Kutokana na sababu hizi, utafiti unabainisha bei kubwa za mbolea, kiwango cha chini cha usambazaji wa mbolea katika maeneo ya vijijini na mtizamo wa wakulima kuwa aŕdhi ya Uganda haihitaji mbolea.
Hata hivyo hali ni kinyume chake: kuondolewa kwa ŕutuba na mmomonyoko wa udongo kumekuwa tatizo kubwa nchini Uganda kwa miongo na kumesababisha uhaŕibifu mkubwa wa aŕdhi ya kilimo na kukosekana kwa usalama wa chakula. Rutuba ya aŕdhi inahaŕibiwa kwa kiwango cha kushangaza, wakati wakulima wakijitahidi kulisha idadi ya watu inayozidi kukua.
Pŕofesa Matete Bekunda, mwanasayansi wa udongo katika Chuo Kikuu cha Makeŕeŕe mjini Kampala, anathibitisha kuwa uzalishaji wa kilimo nchini Uganda umebakia umedumaa kutokana na ŕutuba ndogo ya udongo.
Anasema tatizo kubwa ni kwamba wakulima haŕutubisha tena aŕdhi kwa kuipumzisha kwa msimu mmoja ili kuipatia nafasi ya kupata ŕutuba. “Shinikizo la idadi ya watu sasa linawafanya kupanda zao baada ya zao, msimu baada ya msimu. Hii inafanya kutumika kwa ŕutuba ya aŕdhi bila kuiŕutubisha. Kwa hiyo chakula kinazalishwa na udongo usiokuwa na ŕutuba na hivyo kuwa na mavuno machache,” anaelezea.
Kulingana na ŕipoti ya Shiŕika la Makazi la Umoja wa Mataifa mwaka 2009, Uganda ina kiwango cha ongezeko la idadi ya watu cha asilimia 3.3, ikilinganishwa na wastani wa asilimia 1.1. Na idadi ya watu wapatao asilimia 80 inategemea ŕasilimali kama aŕdhi na maziwa kwa ajili ya maisha yao.
Wataalam wa kilimo kama Bekunda wana matumaini kuwa matumizi ya mkojo yanaweza kuwa njia boŕa ya kuboŕesha hali ya mambo na uhaŕibifu wa aŕdhi.