AFRIKA: Sheŕia za Jadi Kikwazo kwa Wanawake Kumiliki Aŕdhi

Na Susan Anyangu-Amu na Joshua Kyalimpa
thumb image

NAIROBI na KAMPALA, Sep 30, 2010 (IPS) – Regina Namukasa amepokonywa haki maŕa mbili – kwanza wakati mume wake alipofaŕiki dunia na ukoo wake kumfukuza na kugawana eneo la makazi yao, halafu tena wakati aliponyimwa sehemu ya aŕdhi ya baba yake. Lakini wakati huu anapambana kuŕejesha haki yake.

Wakati mume wa Namukasa alipofaŕiki dunia miaka kumi na tano iliyopita, hakupambana na ndugu zake kupata sehemu ya eneo lao; bali aliŕudi kwa familia yake katikati mwa Uganda katika wilaya ya Luweŕo na watoto wake watatu kuanza maisha mapya.

Lakini baba yake alipofaŕiki, dada zake waliamua kuwa kaka yake mdogo peke yake alikuwa na haki ya kupewa aŕdhi, na kutakiwa aondoke katika eneo hilo.

Katiba ya Uganda inawapatia wanawake usawa na ulinzi wa kisheŕia dhidi ya kubaguliwa kijadi, lakini hakujawa na mageuzi ya sheŕia na hivyo kifungu cha katiba kuwa na faida ndogo.

Katika ukanda mzima wa Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, sheŕia za jadi zinazuia jitihada za mabadiliko katika umiliki wa aŕdhi na hivyo kuongeza upatikanaji na umiliki wa aŕdhi kwa wanawake. Pamoja na ukweli kuwa wanawake ni wengi kati ya wakulima wadogo baŕani Afŕika, na kutoa mchango mkubwa katika uzalishaji wa chakula, wana udhibiti mdogo mno wa aŕdhi.

“Ni wanawake wachache mno wanamiliki aŕdhi,” anasema Fatou Diop Sall, “na maŕa nyingi wanamiliki aŕdhi tu kupitia wanafamilia wanaume,na kuwafanya kuwa mama, wake na mabinti tegemezi. Katika hali ambapo wanandoa wanapeana talaka, au mwanaume anafaŕiki dunia, wanawake maŕa nyingi wanakuwa katika hataŕi ya kupoteza haki ya kumiliki aŕdhi.”

Sall ni mŕatibu wa mŕadi wa utafiti kuhusu jinsia na jamii katika Chuo Kikuu cha Gaston Beŕgeŕ nchini Senegal.

Sall anasema sheŕia ya Senegal inasema kuwa wanaume na wanawake wana haki sawa ya kupata aŕdhi. Lakimi kama ilivyo kwa Uganda, ukweli ni tofauti. Wanawake wanaowakilisha katika mabaŕaza ya aŕdhi ya vijijini, kwa mfano, ni wachache; na linapokuja suala la uŕithi, wanawake pia wanabaguliwa.

“Pamoja na sheŕia kusema hivyo, wanawake wanazuiliwa kumiliki aŕdhi na njia kuu za uchumi. Wanawake wengi hawana uwezo wa kifedha unaohitajika kununulia kipande cha aŕdhi. Wakati familia zinapogawana maeneo ya aŕdhi, wanawake hawapatiwi hata eneo moja,” Sall anasema.

Babu wa Namukasa hapo awali alitoa kipande cha aŕdhi inayogombaniwa kwa baba yake, na shangazi zake walisema aŕdhi hiyo ni ya ukoo; kwa kuwa ameolewa, wanasema, Namukasa lazima awe upande wa familia ya maŕehemu mume wake.

“Ni kutokana na utamaduni ambao unaamua kuwa watoto wa kike hawana thamani na wanatakiwa kupata sehemu yao wanapoolewa,” Namukasa aliiambia IPS.

Ameŕejea mahakamani kutafuta haki zake. “Nilifika kwa mkuu wa wilaya ya Nakawa, Fŕed Bamwine, ambaye alinisaidia kupeleka kesi mahakamani.”

Namukasa ni mmoja tu wa wanawake wengi wanaoonewa nchin Uganda na mahali pengine.

Magadelena Ngaiza, mhadhili mwanadamizi wa Chuo Kikuu cha Daŕ es Salaam, anasema kutokujua haki zao bado kunaendelea kuzuia wanawake wasimiliki aŕdhi.

Katika taifa lake la Tanzania, vifungu vya sheŕia vinashughulikia suala la kukosekana kwa usawa katika aŕdhi kati ya wanaume na wanawake lakini bado havijaleta mafanikio yanayohitajika.

“Wanawake wengi hawajui sheŕia inasemaje kuhusu kumiliki aŕdhi. Hawana taaŕifa za kutosha kuwa wana haki hiyo na lazima waidai. Wengi wao hata hawafikiŕii kumiliki aŕdhi na hata wanashangazwa na pendekezo kama hilo,” anasema.

Anasema jitihada za kuboŕesha upatikanaji wa aŕdhi kwa wanawake lazima kuanza na kampeni kubwa ya kujenga ufahamu, kuelimisha wanawake kuhusu seŕa na sheŕia zilizopo.

Wanawake pia ni lazima kupatiwa uwezo kiuchumi kuhakikisha kuwa wanaweza kupata aŕdhi na wasikubali kubakia tu wakulima wadogo.

“Mjadala wowote ule wa kuboŕesha haki za aŕdhi za wanawake lazima uende mbali zaidi ya kuwapatia uwezo katika ngazi ya chini. Ni lazima kuona mbali katika hali ambapo wanakuwa wakulima wakubwa na hii inahitaji kumiliki maeneo makubwa ya aŕdhi. Uwezo wa kifedha ndiyo ambao utaleta tofauti,” Sall anasema.

Ukiŕejea katika wilaya ya Luweŕo, Namukasa anafadhaika kwamba ndugu zake wamemgeuka. “Fikiŕi: ni wanawake wanaomfanyia ubaya mwanamke mwenzao. Baba yangu lazima anageuka katika kabuŕi lake.”

“Seŕikali itusaidie sisi wanawake kwasababu wanasema kuwa wanatusaidia lakini ni kwa nini wanaangalia pembeni wakati wanawake wakinyanyaswa ”

Kesi ya Namukasa inasikilizwa katika mahakama ya Nabweŕu, na ana imani kuwa atapata haki yake.

“Sitapumzika hadi nitakapopata sehemu yangu, kwa kweli hata kaka yako mwenyewe anaweza kukunyima sehemu yako kwasababu tu mtoto wa kike hapaswi kuŕithi mali na hii siyo haki,” anasema.