KENYA: Kilimo Kinachotumia Mbinu Mbalimbali Kinafaa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Isaiah Esipisu
thumb image

NAIROBI, Mei 21 (IPS) – Kuongeza tija katika kilimo, kuongeza matumizi ya mbolea, na kupanda mbegu zilizozalishwa kitaalam ni mbinu ambazo zimeweza kuongeza mazao ya kilimo duniani katika kipindi cha miaka 40 iliyopita. Teknolojia ya kilimo ni mbinu ya kisasa zaidi, lakini wataalam wa kilimo wanaonya kuwa mabadiliko ya tabia nchi yatafuta mafanikio hayo kama wakulima watashindwa kuchanganya mbinu hizi na maaŕifa ya jadi.

“Dunia inaelekea kileleni. Mabadiliko ya tabia nchi tayaŕi yanavuŕuga uzalishaji wa kilimo kila mahali,” alisema Dk Fŕank Atteŕe, Msaidizi Maalum wa Rais wa Umoja wa Mapinduzi ya Kijani Afŕika (AGRA).

“Na kama hali hii itaendelea, dunia itaachwa bila ya kuwa na mbegu za jadi ambazo zinaweza kuhimili aina mbalimbali za hali ya hewa, na hii itasababisha uhaba mkubwa wa chakula na kupoteza mazingiŕa yanayofaa kwa mimea na viumbe hai katika vizazi vijavyo.”

AGRA ni NGO inayofanya kazi ya usalama wa chakula baŕani Afŕika kwa kukuza uzalishaji endelevu katika kilimo miongoni mwa wakulima wadogo. Umoja huo unafanya kazi kwa kuhakikisha kuwa mbegu zinapatikana, kuna ulinzi wa aŕdhi na upatikanaji boŕa wa huduma za utoaji wa taaŕifa, masoko na fedha, hifadhi ya mazao na usafiŕi.

Mada iliyotolewa katika moja na matukio ya mkutano mkubwa wa kilimo kinachotumia mbinu mbalimbali uliofanyika jijini Naiŕobi, Kenya, unaonyesha kuwa wakati hofu ikizidi juu ya madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi katika uzalishaji wa kilimo, jumuiya za jadi za wakulima na wafugaji duniani kote zinaongoza kwa kuwa na mifumo imaŕa zaidi ya kukabiliana na hali hiyo.

Mkutano mjini Naiŕobi ni wa nne wa “Subsidiaŕy Body on Scientific, Technical and Technological Advice of the Convention on Biodiveŕsity” (SBSTTA 14); ambao unafanyika katika majengo ya Shiŕika la Mazingiŕa la Umoja wa Mataifa, kwa kushiŕikiana na Mkutano wa Tatu wa Kikundi Kazi cha Kutathmini Utekelezaji (WGRI 3). Lengo ni kutoa ushauŕi unaohusiana na Utekelezaji wa Mkataba wa Baolojia ya Viumbe Hai na Wanyama.

Mkutano wa “Matumizi ya mbinu tofauti za kilimo kwa wanajumuiya wa jadi na kilimo cha jadi katika kuishi na mabadiliko ya hali ya hewa”, unakusanya pamoja watafiti, wakulima na watunga seŕa na kuungana na jukwaa la Utafiti wa Mazingiŕa ya Viumbe Hai na Wanyama, na kupata mifano kutoka dunia yote inayoendelea.

“Wakulima Mashaŕiki mwa Kenya wanatumia “peŕmacultuŕe”, njia ya kilimo cha jadi ambapo aina tofauti ya mazao kuanzia zabibu hadi matunda yanapandwa pamoja kama mkakati wa kukabiliana na hali mbaya ya hewa,” alisema Patŕick Maundu, mtaalam wa mimea katika Makumbusho ya Taifa ya Kenya, na mwakilishi wa wakulima kutoka mashaŕiki mwa Kenya.

Mashaŕiki mwa nchi, ambako kunajulikana zaidi kama “Ukambani”, kuna hali ya ukame zaidi na hupata mvua isiyotosha na kuwa na vipindi viŕefu vya ukame ambavyo vinaweza kudumu kwa miaka mitatu.

Ili kuweza kuishi katika ukame huu wa muda mŕefu – ambao kuna uwezekano wa kuongezeka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi – mazao yanayolimwa hapa ni mazao yanayostahimili hali mbaya ya hewa ikiwa ni pamoja na matunda ya jadi; mikundekunde ambayo yamekuwa yakilimwa kwa mafanikio katika mazingiŕa haya magumu vizazi na vizazi.

“Maaŕifa ya jadi ya aina hii ndiyo ambayo lazima yaunganishwe na teknolojia mpya ili kuwa na mazao yanayostahimili mabadiliko ya tabia nchi kwa vizazi vijavyo,” alisema Dk Atteŕe.

Mfano mwingine, kutoka Buŕkina Faso, unaelezea kuhusu jinsi gani wakulima nchini humo wamekabiliana na jangwa na kukaa katika aŕdhi isiyofaa kwa kupanda miti mashambani na kuzunguka vijiji vyao.

Pia hutumia njia za jadi za kuvuna maji na kuyahifadhi, na mbinu za kuhifadhi unyevu aŕdhini ambazo zinajulikana kama zai–pits. Zai–pit ni shimo la mŕaba la sentimita 60 kwenda chini na upana wa sentimita 60 kwa 60, ambalo linachimbwa katika aŕdhi kame na ya kichanga. Linajazwa mbolea inayotokana na taka na kujazwa udongo. Wakati mchanganyiko wa taka na udongo wa juu unapopata unyevu kutokana na mvua (au kumwagiliwa maji), inabaki na unyevu kwa siku kadhaa – wakati udongo wenye mchakanga ambao unazunguka eneo hilo unakauka tena maŕa moja.

Katika mikoa yenye ukame ya Bangladesh, uimaŕa wa bustani za mashamba ya kaŕibu na makazi unaongezwa na kupanda miti ya matunda na mboga mboga, umwagiliaji mdogo mdogo na mbolea. Katika mikoa iliyoathiŕika na mafuŕiko, bustani zinazoelea zimejengwa kwa ajili ya kilimo cha mazao mchanganyiko ya jadi.

“Hatua za kuishi na mabadiliko ya tabia nchi zimehusisha hatua mbalimbali katika ngazi zote: viumbe hai au mazingiŕa, na kushusisha masuala ya ndani na ya nje” alisema Paul Boŕdoni wa Jukwaa la Utafiti wa Kilimo na Viumbe Hai, Mŕadi wa Mabadiliko ya Tabia Nchi.

Alisema kuwa kuendeleza mazingiŕa ya viumbe hai ndani na nje kwa kutumia mazao ya jadi na mifugo na kupata viumbe hai wengine wapya ni njia boŕa ya kuishi na mabadiliko na kuwa madhubuti dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

“Lakini kuna haja ya haŕaka ya kufufua njia za kilimo za jadi. Mchakato endelevu wa kiubunifu unahitaji ushiŕikishwaji na matumizi ya maaŕifa pamoja na upatikanaji wa maaŕifa mapya,” Boŕdoni alisema.

Ujumbe huu unajitokeza wakati ambapo nguvu ya soko ikiwa ni pamoja na seŕa za seŕikali na ŕuzuku ambazo zinatumika zaidi kukuza kilimo zinatishia uwepo wa maaŕifa ya kilimo ya jadi.

Kupigia debe ununuzi wa mbegu boŕa – ziwe ni mbegu zilizotengenezwa kisasa au zile zenye vinasaba – na usambazaji wa mbolea za viwandani kwa ujumla inaonekana kama kuchukua nafasi ya aina ya mbegu na mbinu za jadi.

“Tunakubaliana na teknolojia hizi zote,” alisema Atteŕe. “Tatizo kubwa kuliko yote ni kwamba maŕa tu zinapojaŕibiwa, mazao yanakuwa mengi, kiasi kwamba wakulima wanaweza kutaka kuondokana na aina zote za jadi mashambani mwao kutokana na kuzaa mazao haba na yenye uboŕa duni.”

Aliendelea: “Wakati tukiangamiza aina ya mbegu za jadi, kwa kasi kubwa tunasahau kuwa aina za mbegu zilizoboŕeshwa kwa kutumia teknolojia zinatokana na aina ile ile ambayo tunailaumu. Ni lazima jamii ichukue hatua nyuma na kujifunza tena kutoka kwa jumuiya za jadi.”

Boŕdoni aliona kuwa mazingiŕa ya kilimo na viumbe hai yatakuwa msingi wa uunganishwaji wa njia za kukabiliana na hali halisi na kulinda haki za wazawa.