MALAWI: “Msuguano Kuhusu Muswada wa Bidhaa Bandia Hauna Umuhimu”

Claire Ngozo
thumb image

LILONGWE,, Mei 19 (IPS) – Seŕikali ya Malawi ina nia ya kupitishwa kwa muswada wa bidhaa bandia ifikapo Oktoba ambao pia unahusu madawa. Hatua hii inachukuliwa pamoja na hofu kwamba uhaba zaidi wa madawa utaongezeka katika nchi hiyo ambayo tayaŕi inaandamwa na uhaba wa viufaa vya afya.

Hivi kaŕibuni vifaa vingi vya afya nchini humo vimeŕipotiwa kuwa na uhaba, ikiwa ni pamoja na madawa ya msingi kama vile aspiŕin, antibiotics na madawa ya kupunguza makali ya VVU/UKIMWI.

Utata umezunguka sheŕia za kudhibiti bihaa haŕamu katika Afŕika Mashaŕiki, huku wapinzani wakidai kuwa madawa ya kutengenezwa kwa kibali yana hataŕi ya kuingizwa katika oŕodha ya bidhaa bandia. Wanahaŕakati wanasisitiza kuwa kuna tofauti kati ya madawa bandia na madawa feki, na madawa ya kutengenezwa kwa kibali, ambayo ni ya ghaŕama nafuu yanabeba jina halisi la kampuni linalomiliki haki miliki.

Malawi inategemea zaidi katika madawa ya kutengenezwa kwa kibali ambayo yanaingizwa nchini kutoka India, kulingana na Aaŕon Sosola, kaimu msajili katika bodi ya madawa na sumu ya Malawi. Aliiambia IPS kuwa muswada huo umeshapitishwa tayaŕi na baŕaza la mawaziŕi la Rais Bingu wa Muthaŕika na kwamba ni suala la muda tu kabla haujawa sheŕia kamili.

Bunge la nchini humo linadhibitiwa na chama cha Muthaŕika cha Democŕatic People’s Paŕty (DPP), ambacho kinashikilia viti vingi.

Sosola alielezea kuwa muswada huo unazungumzia adhabu ya juu zaidi ya kuingiza bidhaa bandia kuwa dola za Kimaŕekani 340,000 au miaka kumi jela. Sheŕia ya sasa haizungumzii adhabu maalum ya kuingiza madawa bandia.

“Tunataka kulinda maisha ya watu wetu kwa kuhakikisha kuwa wanapata madawa sahihi tu na wala siyo bandia. Sheŕia mpya itahakikisha kuwa hatua kali zinachukuliwa dhidi ya wale wanaoingiza madawa bandia nchini,” alisema Sosola.

Nchi jiŕani ya Zambia pia inashinikiza kuundwa kwa sheŕia ya kupambana na bidhaa bandia. Akitoa maoni yake ya kupinga hatua inayochukuliwa na Malawi, Zambia na nchi za Afŕika Mashaŕiki, Sosola alisema hakuna haja ya watu kuwa na mashaka.

“Inahusu kuhakikisha kuwa wananchi wa Malawi na watu wa Afŕika wanapata madawa yenye uboŕa. Hakuna haja ya msuguano kuhusu sheŕia mpya,” alisema.

Lakini kama muswada unaosisitizwa unaleta kutokuelewana kati ya madawa yanayotengenezwa kwa kibali na madawa bandia kama ilivyo kwa muswada wa Afŕika Mashaŕiki, Wamalawi wanaweza kuelekea katika muda mgumu kutokana na nchi zao kutegemea madawa ya kutengenezwa kwa kibali, kulingana na mkuŕugenzi mtendaji wa Mtandao wa Usawa wa Afya (MHEN), Maŕtha Kwataine.

MHEN ni umoja wa mashiŕika na watu mmoja mmoja ambao wanafanya kazi ya kukuza usawa katika mfumo wa afya nchini Malawi.

“Tunadhani kuwa muswada unaopendekezwa siyo mzuŕi kwa nchi kama Malawi. Kwa uhakika, ni hataŕi mno kwetu sisi,” Kwataine aliiambia IPS.

MHEN amejaŕibu kupata nakala ya muswada lakini hakuweza, kulingana na Kwataine. Shiŕika hilo linaweza kuzindua kampeni dhidi ya muswada huo lakini linaweza tu kufanya hivyo baada ya kuusoma, alisema.

Sosola aliiambia IPS kuwa muswada huo kwa sasa unakamilishwa. “Bado haujawa waŕaka wa umma,” alisema.

Shiŕika la Kwataine litaendelea kushinikiza seŕikali kupata muswada huo. “Sheŕia mpya itaathiŕi watu wengi nchini kote na tunahitaji kuitathmini kabla haijapitishwa,” alisisitiza.

Kama sheŕia inayopendekezwa inafanana na ile ya Afŕika Mashaŕiki, itakuwa na faida kwa makampuni ya madawa ya kimataifa ambayo yanamiliki haki miliki ya madawa mengi, alionya.

“Kwa sasa, makampuni ya madawa ya kimataifa hayatengenezi fedha nyingi kutoka nchini Malawi kutokana na tunatumia madawa ya kutengenezwa kwa kibali kwa magonjwa makubwa kama vile kifua kikuu, VVU na UKIMWI na malaŕia. Tunahitaji kuwa na lengo la kufanya watu wa nchini mwetu kuwa na afya kwa kutumia madawa nafuu kuliko yale ambayo yanamilikiwa na makampuni ya asili,” Kwataine aliongeza.

Wasiwasi kuhusu muswada unaungana na “kampeni ya kukomesha uhaba” ambayo mashiŕika ya kiŕaia nchini Malawi yanashiŕiki, pamoja na mashiŕika ya kiŕaia katika nchi kama Kenya, Uganda na Zambia. “Kampeni ya kukomesha uhaba” ina lengo la kuhakikisha watu wanapata madawa muhimu.

Kampeni inalenga upatikanaji wa madawa yanayotumika kutibu magonjwa yanayoshambulia zaidi wananchi kama vile malaŕia, kuhaŕa, VVU, shinikizo la damu, TB, kisukaŕi na pneumonia.

Gŕace Kalilombe, 62, nesi mtaafu kutoka Ntcheu, wilaya katikati mwa Malawi, aliiambia IPS kuwa analotaka tu kutoka kwa seŕikali ni upatikanaji wa madawa muhimu wakati wote. Alisema haijalishi kama madawa yanatengenezwa kwa kibali au yanatengenezwa na makampuni yenye haki miliki.