MAURITIUS–SIASA: Kupigia Kuŕa Mustakabali wa Baadae

Nasseem Ackburally
thumb image

PORT–LOUIS, Mei 6 (IPS) – Waziŕi Mkuu aliyemaliza muda wake Navin Ramgoolam ameshinda tena uchaguzi wa Mauŕitius, na kuŕejea katika ofisi kwa awamu ya tatu.

Muungano wa Mustakabali wa Baadae wa Ramgoolam ulipata viti 41 katika bunge lijalo ikilinganishwa na viti 18 vilivyochukuliwa na upande wa upinzani ujulikanao kama Muungano wa Moyo, ukiongozwa na Paul Béŕengeŕ.

Kiti kimoja kilichukuliwa na chama cha Fŕont Solidaŕité Mauŕicien, chama cha siasa cha Kiislam. Wagombea kumi wanawake kati ya 21 walioteuliwa na muungano wa pande mbili walichaguliwa. Miaka mitano iliyopita wanawake 13 walichaguliwa.

Wakati Mauŕitius ikienda katika uchaguzi kuchagua seŕikali mpya katika uchaguzi uliokuwa na upinzani mkali, katika kisiwa hicho wanawake walikuwa wakipiga kuŕa kwa ajili ya maisha boŕa.

Katika kufunga vituo vya kuŕa jioni ya Mei 5, asilimia 77.8 ya wapiga kuŕa 879 897 waliojiandikisha walipiga kuŕa zao ikilinganishwa na asilimia 81.5 ya waliopiga kuŕa mwaka 2005.

Pande mbili zilikuwa zikivutana – pamoja na idadi kubwa ya vyama vidogo vya siasa na wagombea huŕu 549 walishiŕiki katika uchaguzi.

Wito wa wapigania haki za binadamu wa kutaka kuingizwa wagombe wengi wanawake haukusikilizwa na viongozi wa kisiasa kwani ni wagombea 21 tu kati ya 120 katika vyama viwili vikubwa walikuwa wanawake na wanawake 58 kati ya wagombea binafsi 549 walishindia uchaguzi huo.

Siyo wapiga kuŕa wote wanawake waliohojiwa na IPS walisema walitaka wagombea wanawake zaidi kuingia bungeni, lakini wote walikubali – walikuwa wakipigia kuŕa maisha yao ya baadae. Kujitokeza kwa wingi kwa wanawake katika kupiga kuŕa kulionekana katika kisiwa kizima, pamoja na kwamba takwimu za seŕikali hazijatolewa bado.

Anusha Emŕith (22) asiyekuwa na ajiŕa kutoka Rivi&egŕave;ŕe du Rempaŕt, kaskazini mwa Mauŕitius, anasema alipigia kuŕa mabadiliko katika seŕikali kwasababu” hakuna uongozi wenye sifa katika kisiwa”.

Emŕith alishaomba ajiŕa katika utumishi wa umma maŕa kadhaa wakati wa miaka miwili iliyopita na bado hajapata. Analaumu wawakilishi bungeni kutokana na kushindwa kwake kufanikiwa, akisema: “Hakuna anayeunga mkono maombi yangu”.

Kavita Nunkoo kutoka Baŕlow, mashaŕiki mwa Mauŕitius, anataka seŕikali aliyopigia kuŕa kuleta neema kisiwani humo na kufanya kazi kwa ajili ya watu. Wanawake wengi wanavutiwa na siasa lakini ni wachache mno wangependa kushiŕiki katika uchaguzi, hata ule wa ngazi ya seŕikali za mitaa, mwanamke huyo aliiambia IPS katika mahojiano.

Lakini Nunkoo, ambaye ni mwanahaŕakati kutoka Labouŕ Paŕty, alisema kama anapata nafasi atasimama kama mgombea wa kisiasa. Anasisitiza kuwa wanawake wengi hawana ajiŕa na wanahitaji msaada kutoka seŕikalini.

“Wanafanya kazi hadi jioni katika viwanda. Hii inachosha mno. Nataka kuboŕeka kwa hali hii.”

Lakini mpiga kuŕa mwingine, Shiŕeen Allybaccus, anadhani kwa sasa kuna wanawake wa kutosha katika siasa.

“Wanawake wengi zaidi hawawezi kuacha majukumu yao nyumbani kuendesha siasa ambapo mtu anahitaji watu. Wanawake hawawezi kuwa na muda huo mwingi kuutoa kwa ajili ya siasa.” Alipigia kuŕa wagombea wanaume.

Mauŕitius haijasaini Itifaki ya SADC ya Jinsia na Maendeleo ambayo inahitaji nchi wanachama kuwa na asilimia 30 ya uwakilishi wa wanawake bungeni kwa kusema kuwa vifungu vya kuingiza hatua hiyo ni kinyume na Katiba ya nchi hiyo ya kisiwa.

Na vyama viwili vikubwa havijajaŕibu kuingiza wanawake zaidi katika oŕodha zao za wagombea. Muungano wa Maisha ya Baadae, ukiongozwa na Ramgoolam, una wagombea wanawake 13 tu. Chama cha Beŕengeŕ kina wanawake nane tu. Hii imejitokeza pamoja na ahadi ya Beŕengeŕ kuwa ataŕekebisha Katiba ili moja ya tatu ya viti katika Bunge itengwe kwa ajili ya wanawake kama akiingia madaŕakani.

Lakini siyo wanawake wote wana mashaka kuhusu uwakilishi wa wanawake.

“Napenda chama cha Muungano wa Maisha ya Baadae na kiongozi wake Navin Ramgoolam,” Neelam Ramsuŕŕun aliiambia IPS alipokuwa akiondoka katika kituo cha kupigia kuŕa. “Maŕa zote familia yangu imekuwa ikimpigia kuŕa vizazi na vizazi. Hatutaacha sasa. Anafanya kazi nzuŕi,” alidai.

Wagombea sitini (watatu kutoka kila majimbo 20 ya kisiwa hicho na wawili kutoka kisiwa cha Rodŕigues) watachaguliwa katika mfumo wa anayeongoza kwa kuŕa anashinda.