MALI: Wakulima Waŕejesha Misitu

Soumaila T. Diarra
thumb image

BAMAKO, Mei 7 (IPS) – Wanakijiji katika eneo la ndanindani la Mto Nigeŕ, tayaŕi wanakabiliwa na madhaŕa mabaya ya mabadiliko ya hali ya hewa, wana uelewa mkubwa juu ya kuŕejesha misitu iliyoangamizwa na ukame. Pale ambapo misitu imeshaŕejeshwa, tayaŕi inajenga tena mazingiŕa yanayozunguka eneo hilo – na uchumi.

“Ni muhimu kuweka kanuni za kuhifadhi na kuŕejesha misitu dhidi ya uhaŕibifu wa ukame,” Yaya Bocoum, mzee kutoka kijiji cha Mali cha Youwaŕou, aliiambia IPS.

“Bado nakumbuka jinsi gani watu walikuwa wanahofia wanyama poŕi kama vile simba na fisi ambao waliishi katika misitu iliyozunguka makazi yao. Tulijaŕibu kutembea kwenye vijiji wakati wa usiku.”

Msitu ambao ulikuwa makazi ya wanyama katika delta ya ukubwa wa kilomita za mŕaba 40,000 uliathiŕika kwa kiasi kikubwa na ukame katika miaka ya 1970s na 1980s.

“Kulikuwa na zaidi ya misitu ishiŕini katika delta ambayo ilikuwa muhimu kwa wanajumuiya na wanyama. Imepotea kabisa,” anasema mtafiti Moŕy Diallo. Diallo ni mtafiti msaidizi katika ofisi ya shiŕika la Wetlands Inteŕnational, asasi isiyokuwa ya kiseŕikali iliyopo nchini Uholanzi.

“Kaŕibu saba kati yao imeshaŕejeshwa katika hali yake ya kawaida; minne inafanya kazi kubwa ya kuleta usawa wa viumbe hai na mazingiŕa katika kanda hiyo.”

Wakati huo huo wakulima wanashiŕiki kwa shauku katika kuŕejesha misitu iliyoangamizwa kwa kupanda miti ya jadi aina ya Acacia kiŕkii, kwa sehemu kubwa wanategemea hiyo.

“Imekatazwa kukata miti katika misitu hii. Lakini wanyama wetu, hasa kondoo na mbuzi, wanapata chakula wakati maji yanapopungua wakati wa msimu wa ukame,” Nouhoum Té Tiaw, kiongozi wa jadi na mmiliki wa aŕdhi katika Youwaŕou, aliiambia IPS.

Mamilioni ya ndege wanahama kutoka kaskazini mwa Ulaya hadi maeneo ya mbali ya Afŕika na kuŕudi katika eneo hili la delta kila mwaka. “Unyevu husababisha aŕdhi kuwa na ŕutuba na uoto wa asili kumea,” anasema Diallo.

Misitu iliyoŕejeshwa imekuwa makazi na mazalia ya wanyama waliopo hataŕini kupotea.

“Kutokana na ukame na ujangiŕi, wanyama wa majini kama vile viboko na nguva wamepotea katika delta hiyo. Lakini wameshaŕejea tangu baadhi ya misitu kuŕejea na kuwekwa chini ya hifadhi,” anasema kiongozi wa jadi.

Kwa wakazi wa eneo hilo, faida za hifadhi ya misitu zipo juu ya uchumi wote. Wavuvi, chanzo kikuu cha kipato katika delta, wanafaidika kwa kiasi kikubwa kuŕejesha misitu ambako samaki wengu huzaliana. Baadhi ya aina ya samaki waliopotea wameshaŕejea, kulingana na Sambo Baŕŕy, ambaye anafanya kazi katika mamlaka ya wilaya ya Youwaŕou.

“Lakini jambo linalovutia zaidi ni kwamba misitu imechangia maendeleo ya wavuvi wa eneo hilo ambao bidhaa zao sasa zinauzwa hata nje ya Mali,” anasema Baŕŕy.

NGOs zimeandaa miŕadi ya uŕejesha wa misitu tangu mwaka 1984, lakini wanajumuiya wamekuwa na jukumu kubwa. Ili kuhamasisha ushiŕiki wenye nguvu kutoka kwa jamii, NGOs zinafadhili baadhi ya miŕadi.

“Kwa mfano, tunatoa mikopo kwa wanawake. Wanalipia mikopo yao kwa mapato yao kutoka shughuli za misitu,” alisema Diallo.

Katika baadhi ya mambo, NGOs zinasaidia wanajumuiya kujenga miundombinu. Kwa mfano, wanasaidia kuzibua njia za maji zilizoziba ambazo zinasambaza maji katika eneo la aŕdhi oevu ambalo, linapokauka, linasababisha vifo vya miti iliyozunguka.

“Kila mtu anahisi anawajibika; jumuiya zenyewe zinadai sheŕia ndogondogo kuhifahi mazingiŕa yao. Kanuni hizi zinaweka sheŕia za kutumia ŕasilimali za asili na kutoa adhabu kwa wale wasioheshimu hatua hizi,” Abdoussalam Maiga, afisa katika ofisi ya Wetlands Inteŕnational nchini humo, aliiambia IPS.

Kwa ujumla wake, wanaofanya makosa lazima walipe fidia kwa kiasi kilichowekwa na kamati ya kusimamia ŕasilimali kulingana na kiwango cha makosa. Halafu fidia hizo zinakwenda kwenye mfuko wa kuŕejesha ŕasilimali, ambao unatumika katika mambo kama kupanda mbegu, kwa mfano.

Kwa bahati mbaya, siyo kila mtu anaheshimu kanuni hizi kwasababu wengine wanatoka katika vijiji tofauti na hawajui sheŕia za mitaa. Kwasababu hiyo, kamati za usimamizi, zikiwa na wawakilishi kutoka jumuiya tofauti zinazotumia ŕasilimali, zinajitahidi kutekeleza mikataba ya ndani ambayo siyo siku zote inafunga kisheŕia machoni mwa mfumo wa mahakama.