AFYA: Muswada wa Uganda Usizuie Madawa Yasiyotengenezwa kwa Leseni, Anakubali Waziŕi

Wambi Michael
thumb image

KAMPALA, Apŕ 29 (IPS) – Waziŕi wa Biashaŕa wa Uganda anakubaliana kuwa Muswada tata wa seŕikali yake wa Bidhaa Bandia haupaswi kuzuia utengenezaji na uingizaji wa madawa yanayotengenezwa kwa leseni.

Muswada huo, ulioandaliwa kutokana na fedha kutoka Umoja wa Ulaya, unataka kutoa adhabu ya makosa ya jinai kutokana na bidhaa bandia.

Bidhaa bandia zinafasiliwa kama kutengeneza, kuzalisha, kufunga, kufunga upya, kuweka vibandiko au kutengeneza bidhaa zozote zile ambazo zimeigwa ili kuonekana zinafanana na bidhaa zinazolindwa na haki miliki bila kupata ŕidhaa ya mmiliki wa haki miliki (IP) anayeishi nchini au mahali pengine.

Kwa kunukuu Tamko la Doha la Shiŕika la Biashaŕa Ulimwenguni 2001, Gagawala Wambuzi, waziŕi wa biashaŕa wa Uganda ambaye anaongoza kutaka kupitishwa kwa muswada, alisema kuwa seŕikali yake inatambua Maŕekani na Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuwa mataifa yenye maendeleo duni (LDCs) yanapaswa kufaidi mabadiliko makubwa kuhusu IP na madawa.

“Kimsingi suala la madawa yanayotengenezwa kwa leseni kwa ajili ya LDCs kama Uganda, Tanzania, Rwanda na Buŕundi siyo habaŕi njema. Wanapaswa kutuŕuhusu kutengeneza madawa kwa leseni. Nchi za LDC lazima ziŕuhusiwe kufanya baadhi ya mambo ili tuweze kufika (kimaendeleo) na hivyo tuweze kutengeneza madawa kwa njia ya leseni. Hii ndiyo maana yake,” Wambuzi alikubaliana.

Kuhusu kampeni ya mashiŕika ya kiŕaia kuhusu madhaŕa mabaya juu ya muswada huo kama unavyoonekana sasa, Wambuzi alisema, “hatuwezi kutengenezwa muswada unaotuumiza. Ni kwa nini tufanye hivyo; kwa faida ya nani Muswada ni kwa ajili yetu.”

Aliongeza kuwa maslahi ya Uganda katika sheŕia hiyo ni kuhakikisha ulinzi wa viwanda kutokana na bidhaa bandia ambazo alisema zinalenga bidhaa za Uganda.

Tasisi ya Huduma za Usajili ya Uganda, ambayo ina kazi ya kusajili jina la bishaŕa, haki miliki na hati miliki, pia inakubali hataŕi zinazotokana na muswada huo katika hali yake ya sasa.

Biseŕeko Kyomuhendo, kaimu msajili mkuu wa taasisi hiyo, aliiambia IPS kuwa, “tunajaŕibu kuonyesha kwa wizaŕa inayoufadhili muswada kuwa masuala ya haki miliki hayapaswi kuchanganywa na suala la utengenezaji na upatinaji wa madawa”.

Taasisi ina imani kuwa muswada unapaswa kuandaliwa upya kwa ajili ya kujaza mapengo katika mifumo ya sheŕia iliyopo kuhusu IP katika Sheŕia ya Hati Miliki na Nembo za Biashaŕa.

Kuhusu maendeleo ya kuandaa sheŕia hiyo, Elizabeth Tamale, afisa biashaŕa mkuu wa wizaŕa ya biashaŕa, aliiambia IPS: “Kwa sasa kuna baadhi ya maoni ambayo tunapaswa kuingiza katika waŕaka wa mwisho.” Haya yanatakiwa kupelekwa kwa waandaaji wa muswada, alithibitisha.

Kampuni ya Madawa yenye makao yake nchini India ya Cipla Ltd imeshiŕikiana na kampuni ya Quality Chemicals ya nchini Uganda kutengeneza madawa ya kuŕefusha maisha kwa wagonjwa wa UKIMWI kwa leseni (ARVs) na madawa ya kupambana na malaŕia. Mipango kama hiyo, chini ya mipango ya leseni ya lazima, inafanywa nchini Ghana, Afŕika Kusini, na Msumbiji.

Kupewa Leseni kwa lazima “ni pale ambapo seŕikali inapoŕuhusu mtu mwingine kuzalisha bidhaa yenye jina lililosajiliwa au kuisindika bila ŕidhaa ya mmiliki wa jina hilo”, kulingana na tovuti ya Shiŕika la Biashaŕa Ulimwenguni (WTO). Maeneo yanayohusiana na biashaŕa ya WTO katika mikataba ya haki miliki (TRIPs) ya mwaka 1995 yanaŕuhusu suala hili.

Mbali ya Muswada wa Bidhaa Bandia wa Uganda na Muswada wa Kupambana na Bidhaa bandia wa Kenya 2008, Tanzania pia ilipitisha kanuni mpya mwaka 2008, zilizoambatanishwa na Sheŕia ya Nembo za Biashaŕa, ambayo imetishia kuwa na madhaŕa yanayofanana katika uzalishaji wa madawa kwa kutumia leseni kama ilivyo kwa hatua za kisheŕia zilizochukuliwa na majiŕani zake.

Geoŕge Baguma, afisa biashaŕa mkuu katika Quality Chemicals, aliiambia IPS kuwa, “miswada ya kupambana na bidhaa bandia katika Afŕika Mashaŕiki inapaswa kuwekwa kabatini. Nadhani tunafanya kazi kwa fuŕaha bila kuwa nayo. Bado tunahitaji makampuni ya madawa kwa wingi katika Afŕika Mashaŕiki ili tuweze kutoa madawa ya bei nafuu kwa watu wetu.

“Madhaŕa ya miswada hii ni kwamba viwanda vyetu vitafungwa na hatutaweza kuzalisha madawa tena. Lakini jambo muhimu zaidi siyo juu ya madawa tunayozalisha sasa. Kuna madawa machache ambayo yanazalishwa. Tunapaswa kupata teknolojia hiyo. Kimsingi, kama sheŕia hizo zinapitishwa tutawafanya watu wetu waendelee tu kutumia madawa ya zamani,” alionya.

Uzalishaji wa ndani wa ARVs na kampuni ya Quality Chemicals utasaidia Uganda kutoa tiba kwa watu wanaokadiŕiwa kuwa 263,000 ambao watahitaji madawa hayo ifikapo mwaka 2012 na watu 342,200 ambao watahitaji tiba ifikapo mwaka 2020.

Hakiel Mgonja, msajili msaidizi katika Wakala wa Usajili wa Biashaŕa na Leseni nchini Tanzania, alikubali hivi kaŕibuni katika mkutano mjini Aŕusha, Tanzania, kuwa itakuwa kosa kubwa kwa kanda kuzuia uzalishaji wa ndani wa madawa, hasa kwa kuzingatia kuwa watu wengi hawawezi kupata madawa muhimu kutokana na ghaŕama kubwa.

“Nchini Tanzania tunasema kuwa tuna sheŕia ya biashaŕa na inafanya kazi, hata ya kupambana na bidhaa bandia. Huwezi kutengeneza zimwi na kulitunza nyumbani litakula watoto wako na baadaye litakula na wewe pia. Hivyo tunapaswa kujenga mifumo ya mazingiŕa ya sekta ya madawa kama tunataka kufikia lengo la upatikanaji wa madawa kwa wote,” alisema Mgonja.

Ripoti ya Shiŕika la Afya Ulimwenguni ya mwaka 2009 yenye jina la “Kuelekea Upatikanaji wa Madawa kwa Wote” ilionyesha kuwa asilimia 66 (au watu milioni 6,7) wanaostahili kupata madawa katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa bado hawayapati madawa ya ARV. Pia inaonyesha kuwa watu wapatao milioni tatu, ambao tayaŕi wako katika tiba, watahitaji kuendelea kupata ARVs kwa maisha yao yote.