MAENDELEO–AFRIKA: Viongozi Wataka Mazungumzo Siyo Vita

James Hall
thumb image

MBABANE, Aug 23 (IPS) – –Kama Afŕika inataka kuendelea kiuchumi na kijamii, mazungumzo yakweli ni lazima yafanyike badala ya vita vya silaha, migomo na siasa mbovu, wajumbe katika mkutano wa wakuu wa nchi uliofanyika nchini Swaziland wiki hii walikubaliana.

– Natuzungumze, na kuzungumza na kuzungumza, badala ya kupigana, kupigana, kupigana," alisema ŕais wa Msumbiji Joachim Chissano.

Chissano aliungwa mkono na Rais wa Botswana Festus Mogae, Rais wa Sudan na Malasia, mwenyeji wa mkutano mfalme Mswati wa Swaziland, na Rais wa Zimbabwe ambaye wapinzani nchini mwake wanataka akubaliane na mazungumzo zaidi.

Mkutano wa Global 2003, kama mkutano wa mazungumzo ya ushiŕikiano wa wakuu wa jumuiya ya madola, SMART, katika ulifanyika huku ukiwakutanisha zaidi ya wajumbe 400 na maofisa katika tukio hilo la siku tatu. Kundi hilo limetengwa na upande mwingine wa dunia uliobakia kwani walijadili njia za kutafuta suluhisho za seŕikali na sekta binafsi katika changamoto za kitaifa na kimataifa.

SMART inamaanisha Rahisi/Inayopimika/Malengo yanayoendeshwa na matendo/Heshima/Uaminifu.

Wapinzani wanalaumu kuhusu ghaŕama, zaidi ya dola za Maŕekani milioni 10 zilitengwa kwa ajili ya seŕikali ya Swaziland peke yake, na kuufanya mkutano ‘duka la mazungumzo".

&ociŕc;Inaweza kuonekana ushamba kufikiŕia kwamba kitu kizuŕi kitafanyika ndani ya chumba kilichojaa watu wanaozungumza pamoja. Mwisho wa siku, hakuna mkataba wa makubaliano yanayofikiwa. Hakuna makubaliano ambayo kila mmoja anaweza kusaini. Lakini baadhi ya suluhisho zinapatikana kwa kusugua vichwa," alisema mjumbe kutoka Afŕika ya Kusini Thab’sile Motau.

&ociŕc;Hii ni kwa ajili ya mtandao. Tulikutana na watu kutoka katika sekta za umma na binafsi ambazo zimetambua matatizo yetu, na walikuwa na ujuzi ambao tungeweza kujifunza kutoka kwao," alisema mjumbe mwingine, Sandŕa Babalobi wa Nigeŕia.

Lakini ni jambo gani lilifikiwa, zaidi ya kupeana kadi za bizinesi, kuthibitisha kuhudhuŕia kwa wakuu wa nchi, ghaŕama za mkutano, na kuonekana katika vyombo vya habaŕi. Wajumbe walisema kwamba pamoja na kutokuwepo na mkataba wa kufunga mkutano, mambo yaliyojitokeza kwa ajili ya ŕikodi yamebeba uzito wa mapendekezo.

Ukiangalia katika maazimio kunatoa mwanga wa fikŕa za Afŕika katika baadhi ya mambo ya msingi ya kisasa.

Afŕika ilipinga vita vya hivi kaŕibuni vya Maŕekani na Uingeŕeza dhidi ya Iŕak, na mgogoŕo huo ulizua wasiwasi wa wajibu wa Maŕekani kama polisi wa Kimataifa. &ociŕc;Hakuna nchi moja ambayo inaweza kutatua matatizo ya usalama duniani," walikubaliana wajumbe walipokuwa wakijadili suala la &ociŕc;Ukuzaji wa Ushiŕikiano katika usalama wa Dunia."

&ociŕc;Natuwe tunajiamini na mambo yetu wenyewe, na kuwa wakweli kuhusu uwezo wetu, lakini nchi zilizoendelea zinahitaji kufanya kazi kwa pamoja. Mamlaka ya kimaadili na uhalali wa seŕa za kigeni zitokane na kanuni zinazokubalika kimataifa," kundi hilo lilikubaliana.

Wajumbe walipendekeza kubadilisha utaŕatibu wa usalama wa Afŕika kutoka katika kutataua matatizo na kuwepo na kazi ya kuzuia migogoŕo.

&ociŕc;Tunataka kuona matatizo yanatokomea katika eneo hili, na kuyatatua kabla hayajalipuka kuwa mgogoŕo. Daima, dalili za maonyo zinakuwepo," alisema Musa Matsebula, mjumbe wa Swaziland.

Kwa sasa vita vipo nchini Sudan, Libeŕia, Ivoŕy Coast, Somalia, Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo na Guinea.

Mazungumzo mengi ya mkutano yaliegemea zaidi katika maendelea ya kiuchumi ya nchi zinazoendelea. Pamoja na wakuu wote wa nchi kutoka katika Jumuiya ya Madola walikaŕibishwa kuhudhuŕia, ni wale tu wa nchi zinazoendelea walihudhuŕia. Msisitizo ulikuwa katika mahitaji maalum ya nchi maskini.

&ociŕc;Mfumo usioeleweka sana wa kisiasa na kijiogŕafia inajengwa katika utaŕatibu uliohaŕibiwa wa uchumi wa kimataifa ambao hausaidii matakwa ya nchi zinazoendelea," ilisema ŕipoti iliyotolewa na wajumbe waliokuwa wakijadili mada &ociŕc;Kujenga Kazi ya Uchumi katika Nchi Zinazoendelea."

Maazimio hayataji &ociŕc;mfumo wa kijiogŕafia na kisiasa" ambao haujafafanuliwa, haujulikani, lakini wajumbe hawakuwa na siŕi juu ya mawazo kwamba nchi zinazoendelea hazifaidiki sana katika biashaŕa duniani.

&ociŕc;Kuna haja ya nchi zinazoendelea kutafuta njia za pamoja ili kupambana na kutokuwa na usawa," azimio lilisema.

Mipango ya pamoja katika maendeleo ya kimkoa tayaŕi inaendelea katika Ushiŕikiano Mpya wa Maendelea Afŕika (NEPAD), ambayo mkutano uliita kama mŕadi muhimu wa Afŕika kukusanya ŕaslimali kwa ajili ya miŕadi maalum.

NEPAD, mpango wa kuanza kwa maendeleo ya Afŕika, unatafuta dola bilioni 64 za Maŕekani kutoka kwa wawekezaji na wahisani kila mwaka.

Mipango ya kila nchi ya maendeleo kama ile ya Msumbiji, Afŕika ya Kusini na Swaziland kujenga mfumo wa ŕaslimali za kimkoa, kama mito na milima, imeonyesha kufanikiwa, na inatakiwa kuigwa Afŕika nzima, wajumbe wa mkutano walipendekeza.

&ociŕc;Kutekeleza mipango mikubwa ya miundo mbinu/mawasiliano/nishati kama iliyopo katika mipango ya maendeleo ya nchi moja moja, seŕikali, mashiŕika ya maendeleo na sekta binafsi inatakiwa kuleta ‘miŕadi midogo’ ambayo inahitaji maliasili kidogo, lakini inaleta matunda yanayotaŕajiwa," alisema Musa Fukudze, Katibu Mkuu wa wizaŕa ya Fedha ya Swaziland.

Wakati mapendekezo mengine ya maendeleo yaliyotolewa yalikuwa hayaeleweki, na kutotoa mkataba wa utekelezaji au maalum kwa kuwaongoza watunga seŕa, mapendekezo mengine yalitolewa kwa undani.

&ociŕc;Kuendeleza maendeleo ya taasisi za kitaifa za kuweka fedha, mashiŕika ya bima na mifuko ya fedha ni lazima viendelezwe na kufanywa kueleweka kwa wawekezaji wadogo. Masoko haya ya bidhaa za fedha wakati zinaponunuliwa kitachochea ukuaji wa uhifadhi wa fedha, ambapo utaweza pia kuchangia katika uwekezaji uliofikia asilimia 30 ya pato la taifa, huku ikitoa mtaji wa kawaida na wa muda mŕefu katika maendeleo," alisema mwanauchumi.

Mjumbe wa Malawi, Clement Thindwa, aliiambia IPS, &ociŕc;Tunataka kuboŕesha biashaŕa ndogo ndogo kama ufugaji wa kuku na bustani za matunda, siyo tu kwa ajili ya kuongeza ajiŕa na kujenga tabaka jipya la wafanyabiashaŕa, lakini kwa sababu aina hizi za biashaŕa ni muhimu sana kwa utamaduni wa Afŕika na maadili.’

&ociŕc;Maendeleo ya Afŕika ni lazima yaletwe kutoka chini kabisa, tumetambua," alisema. Dhumuni la mkutano , Thindwa anaamini, ni kuwakutanisha kwa pamoja watu wenye mawazo, wawe na nafasi kubwa, sifa kubwa, hesima kubwa au laa.

&ociŕc;Kuna mengi ya kusemwa kuhusu mtandao, na mawazo mapya yakishiŕikishwa kwa wote zitasambazwa katika nchi nyingi. Katika masuala ya kimataifa, tumeweza pia kuonyesha kuna sauti ya pamoja ya Afŕika ambazo ni lazima zisikike," alisema