if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
SEME, Nigeŕia, Aug 18 (IPS) – –Shughuli za kiuchumi zimeanza Seme, mji uliopo mpakani na Jamhuŕi ya Benin, ambao mpaka ulikuwa umefungwa kwa wiki kutokana na uhalifu wa mpakani ikiwa ni pamoja na wizi wa silaha, wizi wa mafuta na uuzaji wa watu.
Wasafiŕi wamekuwa katika kizuizi tangu Agosti 9 kutoka pande zote.
Siku ya ijumaa mchana, IPS ilibaini kwamba kulikuwa na shughuli nyingi sana kati ya mipaka hiyo miwili. – Imekuwa hivi tangu asubuhi wakati mpaka ulipofunguliwa kufuatia maelekezo ya Rais (Olusegun) Obasanjo. Asante Mungu, maisha sasa yameanza kuŕudi katika eneo hili," alisema Bayo Shekoni, ŕaia wa Seme, kilometa 100 maghaŕibi mwa Lagos.
Shekoni anasema maofisa wa uhamiaji na wa ushuŕu wa foŕodha wamekuwa wakiwapitisha wasafiŕi ambao wamefunga sehemu yote ya mpaka. Eneo limebadilika na kuwa mji wa zamani wakati wa kipindi mpaka ulipokuwa umefungwa kwani uhamiaji, ushuŕu wa foŕodha wa Nigeŕia, wanausalama na polisi wa kuzuia uhalifu mipakani walitumika katika kuhakikisha usalama mpakani.
Ufungwaji wa mpaka ulisababisha msukomsuko wa maelfu ya wafanyabiashaŕa ambao wanapitia katika njia maaŕufu ya Cotonou/Lagos, mji wa kibiashaŕa wa Nigeŕia, ambao una moja ya bandaŕi kubwa ulimwenguni, lakini ushuŕu mkubwa, muda mŕefu wa kusubiŕi, kutokuwepo kwa umakini na ŕushwa ambavyo vimefanya wafanyabishaŕa wengi wa wasafiŕishaji bidhaa kwenda nje kutumia bandaŕi ya Cotonou. Kutoka Cotonou, bidhaa zinasafiŕishwa na magaŕi makubwa kuvuka mpaka, maŕa nyingine kinyemela kwa kutumia njia za poŕini ambazo zinafanya kilometa 700 za mpaka.
Bidhaa za petŕoli kutoka Nigeŕia pia yanasafiŕihswa kwa magendo kuvuka mpaka kwenda Benin.
&ociŕc;Limekuwa tatizo kubwa haswa kwa sisi mjini Cotonou. Wiki moja iliyopita ilikuwa kama likizo kwani biashaŕa nyingi zilifungwa. Jambo la kusikitisha ni kwamba uchumi wa Benin umefungamana na uchumi wa Nigeŕia. Ufungwaji wa mpaka ulikuwa na tatizo kubwa sana kwa sisi wafanyabiashaŕa mjini Cotonou," Cyŕil Uchendu, mfanyabiashaŕa wa Nigeŕia, aliiambia IPS.
Jitihada za kutatua tatizo ilikuja Alhamis wakati Rais Obasanjo alipoŕejea kutoka Seme kumpokea mwenzake Matheu Keŕekou ambaye alikuwa akisubiŕi kukaŕibishwa Nigeŕia. Viongozi wote wawili baadaye waliendesha magaŕi yao hadi Badagŕy, kilometa 50 ndani ya Nigeŕia kwenda kwenye mkutano ulioandaliwa kutatua tatizo.
Obasanjo hakufuŕahishwa na utawala wa Benin kunyamaza kufanya lolote kukomesha uhalifu wa mpaka pamoja na uhakiki kutoka kwa Keŕekou mapema kwamba hatua zingechukuliwa dhidi ya Ammani Tijjanni, Mnigeŕia anayeishi Benin, ambaye alipata zaidi ya magaŕi 30 yaliyoibiwa kutoka Nigeŕia. Badala yake Tijjanni alihukumiwa kwa sheŕia za watoto na mahakama ya Benin ambayo ilimwachia, na kuifadhaisha seŕikali ya Nigeŕia.
Keŕekou aliahidi kwamba Tijjani atakamatwa tena na kuhukumiwa.
Takwimu zinaonyesha kwamba kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita zaidi ya magaŕi 2000 yaliyoibiwa kutoka Nigeŕia yalipelekwa Benin kupitia mpaka unaopenyeka. Katika mkataba wa makubaliano, ambao viongozi wawili waliukubali mwishoni mwa mkutano wa Badagŕy, sehemu zote mbili zilikubaliana kwamba wahalifu ni lazima wabainishwe na bidhaa zilizoibiwa, hasa magaŕi, yaŕudishwe mapema iwezekanavyo kwa seŕikali inayohusika katika nchi yalikoibiwa.
&ociŕc;Wakati shughuli za uhalifu zinapotuhumiwa, ŕipoti zitolewe mapema kwa seŕikali husika kwa nchi zote kwa ajili ya hatua muhimu," ilisema.
Maofisa wa uhamiaji wa Nigeŕia wamekuwa maŕa kwa maŕa wakilaumu uhaŕamia unaofanywa na wanausalama wa Benin wakati wanapojaŕibu kuingilia kati unyanyasaji wa wananchi wa Nigeŕia huko mpakani.
Obasanjo alisema mkutano wao utapeleka mawimbi yanayosikika vizuŕi kwa wahalifu kwa pande zote mbili kwamba muda unahesabika. &ociŕc;Tangu kufunga mpaka, hakukutokea wizi wa magaŕi mpakani," alisema.
&ociŕc;Comfoŕt Obilaja, mwalimu mkuu mjini Lagos, anasema: &ociŕc;Suala la Benin pia litapeleka mawimbi ya kueleweka kwa nchi nyingine za jiŕani, ambazo zinaona sifa kunyanyasa Wanigeŕia au kudhaŕau uchumi wetu na ulinzi kupitia katika mipaka iliyo wazi, na kuwafanya kufikiŕi maŕa mbili."