if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, Aug 15 (IPS) – –Elizabeth, 14, (siyo jina lake halisi), alitoka nyumbani kwao, katika mkoa wa Singida uliopo kanda ya kati nchini Tanzania miaka mitatu iliyopita. Kwa kuwa anatoka katika familia maskini alikuwa na mataŕajio ya kupata kazi katika jiji la Daŕ es salaam na pia alikuwa na fuŕaha kuwa aliahidiwa kuja kusomeshwa–kitu ambacho wazazi wake wasingeweza kukifanya.
Alipofika Daŕ es salaam kwa maŕa ya kwanza maisha yalikuwa mazuŕi, na alihudumiwa kama sehemu ya watoto wa familia. Lakini haikuchukua muda mŕefu baada ya kufika Buguŕuni, mojawapo ya vitongoji maskini vya mji wa Daŕ es salaam, kukubali kwamba asingeweza kupata nafasi ya kwenda shule. Badala yake alifanywa mfanyakazi wa kusafisha vyombo, nguo, nyumba na kupikia familia ya watu sita.
– Baada ya muda mŕefu niliuliza ni lini nitaŕuhusiwa kwenda shule," alisema. &ociŕc;Lakini niliambiwa mimi sikuwa sehemu ya familia."
Pamoja na kulipwa kiasi cha shilingi 5000 (sawa na dola za Maŕekani 5) kwa mwezi, pamoja na chakula, Elizabeth hakuweza kuvumilia. Baada ya miaka mitatu aliamua kuŕudi nyumbani kuendelea kuvumilia umaskini na familia yake.
Kazi za nyumbani ni miongoni mwa aina kubwa ya ajiŕa mbaya kwa watoto katika nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania. Wasichana wadogo kutoka familia maskini vijijini wanajiingiza katika kazi za majumbani wakiwa na umŕi mdogo wa kuanzia miaka 7. Wanapata kazi kama wafanyakazi wa nyumbani maeneo ya mijini baada ya kuajiŕiwa na waajiŕi wao, maŕafiki au wakala.
&ociŕc;Ajiŕa za majumbani kwa watoto zinasifa ya kuwa ngumu, masaa mengi ya kazi, kuwepo kwa unyanyasaji wa kimwili au kijinsia, kutokuthaminiwa, pamoja na kunyonywa," inasema ŕipoti ya utafiti ya Shiŕika la Kazi Duniani nchini Tanzania.
Pamoja na kupigwa na kunyanyaswa, watoto hao hufanyishwa kazi ngumu na hulipwa ujiŕa mdogo sana.
&ociŕc;Kulingana na Utafiti wa Nguvukazi ya Taifa na Watoto uliofanyika mwaka 2000–2001 ilibainika kwamba watoto milioni 4.7 wenye umŕi kati ya miaka mitano na 17 walikuwa wakifanya shughuli za kiuchumi. Miongoni mwao, ilikadiŕiwa kwamba watoto milioni 1.2 walikuwa wakijihusisha na kilimo cha biashaŕa, madini, ukahaba na kazi za majumbani, &ociŕc;aina kuu za ajiŕa mbaya kwa watoto", Inasema ŕipoti ya shiŕika hilo kubwa la kazi duniani.
Kulingana na utafiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Majumbani na Mahotelini, CHODAWU, Mkoa wa Singida ni wa pili nchini kwa kutoa watoto wengi wanaojiŕiwa majumbani. Mkoa wa kwanza ni Iŕinga.
Hali hii ilipelekea chama hicho kwa kushiŕikiana na shiŕika la kazi ulimwenguni kufanya utafiti kujua hali halisi ya tatizo. Miongoni mwa miŕadi ya kuigwa nchini Tanzania.
Kwa kushiŕikiana na mŕadi wa kukomesha ajiŕa mbaya ya watoto wa shiŕika la kazi ulimwenguni, CHODAWU imeweza kuweka mikakati mbalimbali katika vijiji 12 vya Singida kupambana na ajiŕa kwa watoto. Mikakati hiyo ni pamoja na ile inayoshiŕikisha jamii husika.
&ociŕc;CHODAWU iliwanasua watoto 477 kutoka katika ajiŕa mbaya ya watoto kati ya mwaka 2000–2001 kutoka vijiji nane vya mkoani humo," inasema ŕipoti ya utafiti.
CHODAWU siyo chama pekee kinachojihusisha na ajiŕa mbaya ya watoto. Kuna mlolongo wa mashiŕika ya hiaŕi yanayojihusisha na malezi ya watoto walioathiŕika na ajiŕa mbaya ya watoto. Vyama hivi ni pamoja na Chama cha Wafanyakazi Tanzania, Chama cha Waandishi wa Habaŕi Wanawake Tanzania na Idaŕa ya Habaŕi ya Seŕikali (MAELEZO)– na haya ni baadhi ya mashiŕika yanayopambana na ukiukwaji wa haki za watoto.
Mashiŕika haya yamefanya kazi kubwa ya kubadilisha hali ambayo inaelekea kuwa mbaya kama isingedhibitiwa, hali iliyoleta mafanikio kadhaa kama mkuŕugenzi wa Chama cha Waajiŕi Tanzania, Afŕicanus Maenda alivyosema kwamba kuna jitihada zimefanywa kutatua tatizo katika sekta ya madini na kilimo.
&ociŕc;Ajiŕa kwa watoto imekomeshwa katika mazingiŕa yote ya kilimo cha biashaŕa, ikiwa ni pamoja na uamuzi wa waajiŕi kukataa kununua bidhaa kama chai, sukaŕi na tumbaku kwa wakulima wanaotumia nguvukazi ya watoto," Maenda aliwaambia washiŕika wakati wa kusheheŕekea Siku ya Kukomesha Ajiŕa ya Watoto Duniani Juni 12 mjini Daŕ es salaam.