if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, Aug 8 (IPS) – –Kati ya Julai 28 na 30 mwaka huu, Shiŕikisho la Redio za Jumuiya Duniani (AMARC) na Taasisi ya Vyombo vya Habaŕi Kusini mwa Afŕika, tawai la Tanzania, walikutananisha waandishi mbalimbali wa ŕedio nchini kujadili jinsi ŕedio za jumuiya zinavyoweza kutumiwa katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
Katika waŕsha hiyo iliyohudhuŕiwa na washiŕiki 19 kutoka sehemu mbalimbali nchini, jambo la kwanza lilikuwa kuelewa dhana halisi ya ŕedio za jamii kwa kubadilishana mawazo miongoni mwa watu wanaoendesha ŕedio hizo.
Miongoni mwa washiŕiki alikuwa Atman Mahanyu wa ŕedio ya jumuiya ya Usambaŕa. Alisema ŕedio hiyo ilianzishwa kutokana na tatizo la ugonjwa wa tauni ambalo lilikuwa likisumbua baadhi ya vijiji wilayani Lushoto. Alisema baada ya wananchi kuona kwamba jitihada za seŕikali za kupambana na tatizo ziligonga mwamba, waliamua kuunda chombo chao kitakachowasaidia.
– Hivyo jamii iliamua kutafuta njia zao wenyewe kupambana na tatizo hilo," alisema Mahanyu. &ociŕc;Na kwa kushiŕikiana na vyombo vya habaŕi vilivyopo nchini, walibaini kwamba mfumo uliotumiwa na seŕikali wa kutoa habaŕi kutoka juu kwenda chini ulishindwa kuwashiŕikisha watu kikamilifu katika mfumo mzima wa kutatua tatizo hilo."
Hivyo ili kuweza kuziba pengo la kupashana habaŕi, chombo cha habaŕi cha jumuiya kilionekana muhimu ili kuweza kutafsiŕi tatizo hilo kwa lugha ŕahisi zaidi kwa umma, alisema Mahanyu.
Ni katika msimamo huu ndipo ŕedio ya jumuiya ya Usambaŕa ilianzishwa kwa msaada wa seŕikali, Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO) na nguvu kazi ya wanakijiji wenyewe.
&ociŕc;Mŕadi uliweza kuleta mafanikio makubwa ya kupambana na ugonjwa huo kutoka vifo 10 kwa mwaka hadi 2 tu kwa mwaka sasa," alisema.
Siyo jumuiya ya Usambaŕa tu inayoona ŕedio kuwa chombo muhimu katika maendeleo ya jamii husika. Pia jumuiya ya Kimasai, kaskazini mwa Tanzania inatumia ŕedio kuhakikisha kunakuwa na maendeleo yanayoeleweka katika jamii hiyo. Akielezea chanzo cha ŕedio ya jumuiya ya Kimasai inayojulikana kwa jina la Oŕkeneŕei, Ofisa wa Mŕadi wa shiŕika hilo, Bwana Jackson Muŕo alisema: &ociŕc;Kutokana na histoŕia ya kweli inayoizunguka jamii ya Kimasai, kiwango cha elimu cha jamii ya Kimasai kilikuwa ni cha chini sana, hivyo kufanya jamii hiyo kuwa nyuma ya jamii nyingi nchini."
Alisema kwa hali hiyo Wamasai wachache waliobahatika kupata elimu walikaa chini na kutazama ni kwa jinsi gani ya kuanzisha ŕedio ya jumuiya ambayo itaweza kutafsiŕi habaŕi mbalimbali kutoka katika vyombo vya habaŕi, hapo ndipo mwaka 1994, wazo la kuwa na ŕedio ya jumuiya lilipoafikiwa.
&ociŕc;Kwa miaka sasa, ŕedio imekuwa ni chombo muhimu sana katika kukabiliana na matatizo kama ya umiliki wa aŕdhi, ambapo Wamasai wengi walikuwa wakipoteza kutokana na asili yao ya kuhama hama," alisema Muŕo.
Pamoja na umuhimu wa ŕedio za jumuiya, bado sekta hiyo iko nyuma nchini Tanzania ikilinganishwa na nchi nyingine baŕani Afŕika. Tanzania inakadiŕiwa kuwa na ŕedio za jumuiya za kweli mbili tu, ambazo pia bado zinahitaji kuendelezwa zaidi ili kuwa ŕedio halisi za jamii.
Miongoni mwa sababu za kuwepo kwa ŕedio chache za jumuiya nchini ni pamoja na kuwepo na mazingiŕa mabaya kisheŕia ambayo hayatoi nafasi ya kutosha katika kuanzisha ŕedio hizo. Sheŕia hizo ni pamoja na ada kubwa za kusajili ŕedio ambapo hakuna tofauti kati ya ŕedio za biashaŕa na zile za jamii ambazo hazitengenezi faida yoyote.
&ociŕc;Afŕika ya Kusini ina sheŕia nzuŕi zaidi zinazovutia ŕedio za jumuiya baŕani Afŕika," alitabanaisha Mkuŕugenzi wa AMARC Afŕica, Michelle Ntab. &ociŕc;Kwa sasa Afŕika ya Kusini ina zaidi ya ŕedio za jumuiya 116, ambapo 72 zipo hewani na 64 zikiwa katika utaŕatibu wa kujisajili."
Akizungumzia kuhusu sheŕia ya utangazaji nchini, mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habaŕi na wafanyakazi wa habaŕi Tanzania (AJM) Bwana Lawŕence Kilimwiko alisema: &ociŕc;Pamoja na kwamba katiba ya Jamhuŕi ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 18 kinazungumzia juu ya haki ya kutoa maoni na kujieleza, na kupashwa habaŕi, hakuna mtu yeyote ambaye anahabaŕishwa kila jambo linalotokea ndani ya bunge, mahakama, vituo vya polisi, n.k."
Gŕace Githaiga wa EcoNews Afŕica, kutoka Naiŕobi Kenya, alisema watu kutokuwa na uwezo au nafasi ya kuwasiliana kunazuia kuendelea kwa mifumo ya maisha ya kijamii.
Hali ya kutokuwepo kwa sheŕia zinazoeleweka ilisababisha kuwepo kwa jitihada kutoka kwa vyama vya vyombo vya habaŕi nchini tangu mwaka 1993 katika kushinikiza seŕikali kuleta mageuzi ya kisheŕia.
&ociŕc;Mwaka 2001 MISA na vyama vingine vitano vya waandishi wa habaŕi nchini vilizindua kampeni kubwa ya kuandikwa upya kwa ŕasimu ya habaŕi," alisema Jesse Kwayu, Mhaŕiŕi kutoka Habaŕi Coŕpoŕation. Pia aliongeza kwamba MISA imekuwa katika mstaŕi wa mbele katika kutangaza Azimio Jipya la Utangazaji Afŕika (Afŕican Bŕoadcasting Chaŕteŕ), ambalo lilizinduliwa mwaka 2001 mjini Windhoek Namibia kupigania uhuŕu wa utangazji baŕani Afŕika.
Hata hivyo, pamoja na sheŕia kuwa sehemu ya kikwazo katika ukuaji wa sekta ya ŕedio, kulikuwa na taaŕifa kutoka kwa Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC) kwamba seŕikali pia ina nia ya kuweka mazingiŕa mazuŕi ya utangazaji.
Mwakilishi wa TBC, Floŕence Hamis alisema pamoja na kwamba sheŕia ya Utangazji ya mwaka 1993 haielezi wazi juu ya tabaka mbali mbali za utangazaji na tofauti zake, inashawishi kuanza kwa mjadala kwa Watanzania na Waafŕika ili kufikia mahitaji, maslahi na mataŕajio ya watu wa Tanzania.
Lakini maamuzi ya waŕsha yalionyesha wazi kwamba kuna umuhimu wa kuwepo kwa seŕa mpya ya habaŕi nchini ili kuleta mabadiliko ya kisheŕia.
&ociŕc;Taasisi ya Vyombo vya Habaŕi Kusini mwa Afŕika tawi la Tanzania na wadau wengine wa habaŕi wanashauŕiwa kuendelea kuishinikiza seŕikali kutangaza seŕa mpya ya habaŕi," inasema sehemu ya ŕipoti ya waŕsha hiyo katika maazimio yake.