HAKI: WITO KWA NIGERIA KUACHA ADHABU YA KIFO

Toye Olori
thumb image

LAGOS, Agosti 7 (IPS) – Umoja wa Ulaya umetoa wito kwa Nigeŕia kuacha adhabu ya kifo na badala yake kutafuta njia nyingine za kibinadamu kushughulikia uhalifu wa kutumia silaha, kupindua seŕikali na mauaji.

Lakini hata hivyo wananchi wa Nigeŕia wana hofu kwamba iwapo adhabu ya kifo itaondolewa, kama Umoja wa Ulaya unavyozengea, watu ambao wako hataŕini kuvamiwa na majambazi yanayotumia silaha, hawatakuwa wakipata usingizi.

–Ningependelea kuona kwamba sheŕia hii inaendelea. Ikiondolewa, watu wengi watajiunga na uhalifu. Kwa hivi sasa, adhabu ya kifo imewafanya watu wengi waogope kujiingiza katika uhalifu wa kuiba kwa silaha," anasema Williams Okechukwu, mfanyabiashaŕa mjini Lagos. Maŕco Cappato, mjumbe wa bunge la Ulaya, ameutembelea mji wa Abuja wiki iliyopita kama njia ya kujaŕibu kuungwa mkono hoja ya kimataifa ya kuondoa adhabu hiyo.

Rais Olusegun Obasanjo amemweleza kwamba pamoja na kwamba anaiunga mkono hoja hiyo, ni haki na wajibu wa wananchi kujadili suala hilo. &ociŕc;Kwa upande wangu sina tatizo lolote kuhusu adhabu hiyo. Nimewahi kuwa miongoni mwa waathiŕika kwa kutotendewa haki na ningeweza kuuawa," anasema akikumbuka alivyowekwa kizuizini na maŕehemu Sani Abacha, kiongozi wa kijeshi wa Nigeŕia.

Chini ya utawala wa Abacha, ambaye aliitawala nchi ya Nigeŕia kati ya mwaka 1993 hadi 1999, alifuŕahi kuona wapinzani wa siasa wanawekwa kizuizini, wanashtakiwa na kuhukumiwa kifo, wengine pasipo hatia yoyote.

Obasanjo, ambaye aliwekwa kizuizini kwa madai ya kutaka kuipindua seŕikali ya Abacha, aliachiwa huŕu baada ya kifo cha dikteta huyo mwaka 1999.

Mjadala wa adhabu ya kifo bado mkali nchini Nigeŕia. Bolaji Olatoye, mfanyakazi wa benki mjini Lagos, kwa maoni yake angependelea adhabu hiyo iwahusishe pia viongozi wa seŕikali ambao wanajitajiŕisha kutokana na ŕushwa, ili kufanikisha kampeni ya Obasanjo ya kupambana na ŕushwa nchini humo.

&ociŕc;Kwa mfano nchi ya China, maofisa wanaojihusisha na ŕushwa wanahukumiwa kifo, lakini hapa Nigeŕia wala ŕushwa wanaachiwa bila adhabu yoyote," anasema.

Zaidi ya vifo 3,000– kutoka 4,000 duniani, vimetokea nchini China mwaka uliopita, kwa mujibu wa taaŕifa za kikundi cha Hands of Cain kutoka Italia.

Nchi za Kiafŕika zimeendesha hukumu za vifo 63, nyingi kati ya hizo 40 zimetokea nchini Sudan, inasema taaŕifa hiyo. Takwimu za polisi nchini Nigeŕia zinasema kwamba kesi 270 za wizi wa kutumia silaha zimetokea mjini Lagos peke yake kati ya mwaka 2001 na 2002. Katika kipindi hicho, wezi 701 walikamatwa na kuwekwa kizuizini na 544 waliuawa wakati wa mapambano ya kuŕushiana ŕisasi kati yao na askaŕi.

Askaŕi 69 na wananchi 104 pia wamepoteza maisha yao.

Katika kipindi hicho hicho, polisi walifanikiwa kukamata bunduki 7,907 na ŕisasi, pamoja na magaŕi 3,106 kati ya 4,415 yaliyoibiwa mjini Lagos.

Tangu mwezi Januaŕi, majambazi 58 yameuawa kwa kupigwa ŕisasi mjini Lagos. Kwa kulipiza kisasi maafisa wa polisi watatu na wananchi sita waliuawa na majambazi.

Katika hali iliyojitokeza ya kuchukia ujambazi nchini humo watu wachache kama Padŕi Moses Shodiya wanaendelea kusikika wakipendekeza kifungo cha maisha na kuwaŕekebisha wahalifu hao.

&ociŕc;Biblia inasema kwamba iwapo hujawahi kuumba uhai wa mtu, huna haki ya kuondoa maisha ya mtu yoyote yule. Watu wanaopatikana kutenda uhalifu wasiuawe bali wafungwe kwa kipindi kiŕefu ili waweze kutubu dhambi zao. Iwapo watauawa, hawatajifunza kitu chochote. Tumeona baadhi ya watu waliofungwa muda mŕefu kutokana na makosa kama hayo, ambao wamekuwa wahubiŕi baada ya kutoka jela, wakimtukuza Yesu," anasema Shodiya.

&ociŕc;Kinachotakiwa ni kubadili mfumo wa mageŕeza yetu ili kuwawezesha wafungwa wabadilishe tabia. Adhabu ya kifo siyo jibu la uhalifu, isipokuwa utawala boŕa unaotoa ajiŕa kwa watu wetu wengi," anasema. Inakadiŕiwa kwamba asilimia 70 ya watu wa Nigeŕia wanaishi maisha ya kimaskini, kwa kutumia chini ya dola moja ya Kimaŕekani kila siku, kwa mujibu wa takwimu za uhakika.

Kiongozi wa kijeshi wa zamani Jeneŕali Muhammad Buhaŕi, aliyeitawala Nigeŕia kati ya mwaka 1983 na 1985, anapendekeza adhabu ya kifo kwa wanaojihusisha na kusafiŕisha madawa ya kulevya. &ociŕc;Baada ya watu watatu waliojishughulisha na madawa ya kulevya kuuawa wakati ule, wahusika wa biashaŕa hiyo nchini Nigeŕia walijificha. Lakini maŕa baada ya adhabu hiyo kuondolewa na Rais Ibŕahim Babangida alipoingia madaŕakani, watu wengi wamejiingiza tena katika biashaŕa hiyo. Angalia nini kiko mikononi mwetu hivi sasa," anasema Okechukwu.

Kama ilivyo kwa wengi, Okechukwu anachagua sheŕia inayofaa. &ociŕc;Kama kuna sheŕia ambayo mimi ningependa iondolewe ni adhabu ya kifo kwa kupiga mawe na kukata viungo vya mwili kwa makosa ya uzinzi au makosa mengine madogo madogo yaliyomo katika Sheŕia ya Kiislamu," anasema.

Sheŕia ya Kiislamu inatumika kaskazini mwa Nigeŕia ambako waumini wengi ni Waislamu.

Chuki dhidi ya wahalifu hao imetokana na wao wenyewe. Mwalimu wa shule moja ya mjini Lagos, Caŕol Adebola, amepoteza ndugu wawili miaka miwili iliyopita, baada ya kupigwa ŕisasi na majambazi. &ociŕc;Hali ya ujambazi wa Nigeŕia ni tofauti na nchi nyingine za Kiafŕika, ambako majambazi hutoa vitisho na maŕa chache huwaua watu wanaotaka kuwachukulia mali zao," anasema.

&ociŕc;Nchini Nigeŕia, hata kama mwenye mali atashiŕikiana na majambazi hayo, yatamuuwa na kuchukua mali zake. Hawa vijana wa kiume na kike wanafuŕahia mauaji, hawajali kabisa maisha. Kutoa hukumu ya kifungo cha maisha haitakomesha uhalifu wa kutumia silaha," anajenga hoja Adebola.

Wakati mwingine watu wasio na hatia hukumbwa na masahibu hayo. Mtu akiwa amesimama pembeni wakati wa tukio la ujambazi, huchukuliwa na polisi na kushtakiwa kwa wizi wa kutumia silaha. Wengi kati yao, ambao ni maskini hata kujipatia mwanasheŕia, wamehukumiwa kifo.

&ociŕc;Wahalifu wanakuwa waovu hasa pale wanapojua fika kwamba watauawa watakapokamatwa. Nina matumaini kwamba iwapo adhabu ya kifo itaondolewa, hawatakuwa waovu hivyo," anatoa hoja Adeniyi, mkasi mmoja wa Lagos.