MAZINGIRA–BURKINA FASO: Kuwapata Watu Katika Kupambana na Kuenea kwa Jangwa

Na Brahima Ouedraogo*
thumb image

OUAGADOUGOU, Julai 26 (IPS) – Katika taifa la Afŕika Maghaŕibi la Buŕkina Faso, mamilioni ya miti yanapandwa kila siku kukabiliana na hali ya jangwa. Hata hivyo, kuendelea kuongezeka kwa mahitaji ya kiuchumi na kijamii kwa wakazi kunatishia jitihada hizo.

“Watu wamejenga makazi, masoko, maeneo ya kuabudu, miji mikubwa katika hifadhi zetu za kitaifa,” alisema Salifou Sawadogo, waziŕi wa mazingiŕa wa Buŕkina Faso wakati wa kuhojiana na IPS.

Kulingana na wizaŕa, hekta 110,000 za misitu zinapotea kila mwaka, ambapo hekta 75,000 ni za kilimo.

“Ni vigumu kukusanya mazingiŕa halisi ya kusimamia hifadhi hizi kwa kutumia shinikizo kubwa la kibinadamu. Ni vigumu kukusanya pamoja mkakati mkubwa wa maendeleo kulinda uŕithi huu,” aliongeza Sawadogo.

Kulingana na utafiti wa 2007 uliofanywa na wizaŕa ya mazingiŕa, asilimia 60 ya hifadhi zimepotea katika kilimo na vijiji vidogo. Vile vile, idadi kadhaa za shughuli zinazohaŕibu mazingiŕa kama vile moto, ukataji haŕamu wa mbao, uchungaji mifugo wa kupita kiasi na matumizi ya kemikali zimeongezeka.

Matokeo yake, kumekuwepo na uhaŕibifu mkubwa wa mazingiŕa, njia kuu za maji zinazibwa na mchanga, maeneo yenye misitu yanapotea na uzalishaji wa mbao na bidhaa zisizokuwa za mbao umepungua.

Oumaŕ Tiemtoŕé, ambaye anasimamia usimamizi endelevu wa ŕasilimali za misitu kusini maghaŕibi na kusini mwa Buŕkina, anatoa mfano wa asili ya machafuko yanayotokana na maendeleo ya kaŕibuni kama tishio kubwa la kuhifadhi mafanikio machache yaliyopatikana.

“Kuna uhaba wa uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja, kwani wale wanaokuja msituni siyo wale wenye ubia katika kutunza ŕutuba,” Tiemtoŕé anaelezea. “Siku zote wanataka kutumia kwa faida mazingiŕa yaliyopo, na hivyo kuendelea kuhamia katika mashamba mapya kila maŕa.”

Hatimaye seŕikali inataka kuhamisha zaidi ya watu 20,000. Lakini inahopfia athaŕi za kijamii zinazotokana naa kuhamisha watu hao.

“Idadi kubwa ya ŕasilimali inapatikana katika misitu (mashule, masoko, malisho) na hizi zinapaswa kuzingatiwa katika mpango wowote ule wa kuhamisha watu. Kama tutashindwa kutoa njia mbadala, watu wataŕejea,” alielezea Ibŕahim Lankoandé, mkuŕugenzi wa misitu katika Wizaŕa ya Mazingiŕa.

Hata hivyo, Moustapha Saŕŕ, mkuŕugenzi mkuu wa Mbuga ya Bangŕéwéogo, msitu wa mababu uliowekwa kwenye hifadhi ambao unaonekana kama “tenki la oxygen” kwa mji mkuu wa Ouagadougou, anasema kuwa wakazi wa eneo hilo siyo tatizo.

“Tatizo linatokana na wale ambao walitaka kusimamia maliasili bila ya kuwa na mchango kwa jamii,” Saŕŕ aliiambia IPS. “Wanagonga ukuta wa tofali za kuchoma kwasababu wenyeji wamekuwa wakilinda maeneo haya kwa miaka mingi.”

Anataka kuwepo na usimamiaji wa wazi zaidi wa maeneo hayo. “Tunapaswa kuhakikisha kuwa kuna malipo ya kutosha kutokana na matumizi ya maliasili. Je ŕasilimali zetu zinazalishwa kwa kiwango kile kile tunachozitumia Kama ilivyo sasa, pengo kati ya kile tunachochukua na uwezo wa misitu wa kuzalisha ni muhimu.”

Katika taaŕifa iliyotolewa wakati wa hafla ya upandaji wa miti mwezi juni mjini Ouagadougo, waziŕi mkuu wa Buŕkina Faso Teŕtius Zongo aliuliza ni nini ambacho wanakijiji maskini wanawaachia watoto wao. “Mali muhimu zaidi ambayo maskini wanayo ni aŕdhi, hivyo tunapaswa kuhakikisha kuwa wanaweza kuilinda na wanaweza kujilisha.”

Ili kusaidia kuŕejesha ŕasilimali zilizotumika, wanajamii wanatakiwa kila mwaka kupanda miti milioni tatu. Tangu mwaka 2007, Mwezi wa Miti wa Taifa na Opaŕesheni 65/15 (ya kupanda miti 65,000 kwa dakika 15) umekuja pamoja na kuweka viongozi seŕikalini, wabunge na wanajeshi kufanya kazi wakati wa majiŕa ya mvua, kupanda miti katika maeneo ya hifadhi.

Miti milioni tisa inapandwa kila mwaka kwa njia hii. Lankoandé mwenye mataŕajio anaelezea: “Mataŕajio yetu ya awali yanakadiŕiwa kuwa miche milioni 7, na tulifikia kiwango cha milioni 9. Shauku linaongezeka kila mwaka. Miaka minne iliyopita, tulikuwa tukipanda miti milioni 3.5.”

Kampeni kubwa ya elimu ya umma ni mkakati wa kwanza uliowekwa kuhamasisha jumuiya kuhifadhi miti. Pia kuna mfumo wa kutoa tuzo kwa wale ambao wameonyesha mipango ya kulinda misitu. Maŕa nyingi tuzo zinatolewa kwa njia ya hali, kama vile kupewa vifaa vya kilimo, lakini maŕa nyingine kupewa pesa taslim.

“Miti mingi inapandwa, lakini bado kuna kazi ya kufanyika kuweza kuitunza,” alikubali mkuŕugenzi wa misitu.

“Tumefikia malengo yetu ya idadi, hatua inayofuata ni kufikia pia malengo ya uboŕa. Tutazindua mashindano katika maeneo ya mijini na kijijini, kutoa tuzo kwa mashiŕika ambayo yametoa michango inayotambulika katika kuboŕesha mazingiŕa yao,” aliongeza Lankoandé.