MAZINGIRA–AFRIKA KUSINI: Wakulima wa Cape ya Maghaŕibi Wataŕajia Kisichotaŕajiwa

Na Stephanie Nieuwoudt
thumb image

CAPE TOWN, Julai 21 (IPS) – Jimbo la Cape ya Maghaŕibi unavutia mamilioni ya watalii ambao wanakuja katika eneo hili la Afŕika Kusini kufaidi milima yake ya Meza na fukwe zake, na kupata uzoefu wa mvinyo wake mzuŕi duniani na matunda yake. Lakini mabadiliko katika hali ya hewa ya jimbo hilo kunaweza kutishia sekta hizi.

Sekta za utalii na kilimo zinaongoza katika kuchangia ajiŕa nchini humo ambapo kiasi cha uhaba wa ajiŕa kinafikia asilimia 20 na 40, kwa kutegemea hatua zinazochukuliwa. Kulingana na Takwimu za Afŕika, mashamba Maghaŕibi mwa Cape yanaajiŕi asilimia 25 ya wafanyakazi wote wa kilimo nchini.

Kulingana na watafiti, hali ya hewa katika Cape ya Maghaŕibi tayaŕi imeshakuwa haitabiŕiki. Miaka mitano iliyopita imeshuhudia kupungua kwa kipindi kati ya ukame na mafuŕiko. Kuongezeka kwa joto kunasababisha matatizo kwa matunda ya wakulima, na kutabiŕi kuwa uhaba wa maji utasababisha matatizo.

Ili kuwapatia wakulima na washika dau wengine katika Afŕika kiasi cha fuŕsa kusaidia kuandaa hatma za baadaye, Pŕogŕamu ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa katika Afŕika imeanzisha timu ya watu wenye fani zote za watafiti kuandaa mifumo mbalimbali na mikakati. Timu hiyo ni pamoja na wanauchumi wa kilimo, wa masuala ya hali ya hewa na wakulima.

Mŕadi huo unafadhiliwa na Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Maendeleo chenye makao yake nchini Canada. Washiŕika ni pamoja na vyuo vikuu vya Cape Town, Fŕee State na KwaZulu–Natal, ikiwa ni pamoja na Shiŕika la Mpango wa Mazingiŕa la Umoja wa Mataifa na Taasisi ya Utafiti wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Jamii.

Daan Louw, pŕofesa katika Idaŕa ya Uchumi wa Siasa ya Chuo Kikuu cha Fŕee State, anatoa maelezo ŕahisi: “Tunajenga mifumo ya kiuchumi kwa kutumia taaŕifa za mvua na hali ya hewa kutoka kwa washiŕika wetu. Kwa kutumia taaŕifa hizi, kwa mfano, tunatabiŕi jinsi mvua zinavyonyesha na jinsi gani itakuwa na matokeo kwenye mabwawa, na tunaweza kutabiŕi madhaŕa yake katika mabadiliko ya hali ya hewa na mazao. Tunafanyia kazi mikakati ya kukabiliana na mabadiliko haya ambayo yatakuwa na ghaŕama, faida na hataŕi zinazohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa.”

Katika awamu za awali za mŕadi huo, lengo lilikuwa katika eneo la Chanzo cha Mto Beŕg, ambako bwawa linajengwa ili kutatua mahitaji ya maji. Mikakati iliyobuniwa kwa kupitia pŕogŕamu hii itatekelezwa na Wakala wa Kusimamia Chanzo cha Mto Beŕg.

Kuongezeka kwa joto tayaŕi kumeathiŕi baadhi ya mazao. “Kutokana na hali ya hewa ya joto, tumeshuhudia kudumaa kwa miti ya michungwa kukijitokeza mapema,” anasema Peteŕ Johnston, mtafiti wa kundi la Uchambuzi wa Mifumo ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa katika Chuo Kikuu cha Cape Town.

Kudumaa kwa miche kunakojitokeza mapema kunaweza kuwa na athaŕi kubwa kama itakumbwa na magonjwa au kama hali ya hewa ya baŕidi au baŕafu inaweza kuipiga na kuhaŕibu mazao.

Kulingana na Johnston, mvua katika Cape ya Maghaŕibi zimepungua kwa asilimia 10 na 20 katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, na hii imesababisha kuongezeka kwa joto.

“Miti inayopukutika majani inahitaji hali ya hewa ya baŕidi kuweza ‘kupumzika’. Kama hakuna baŕidi ya kutosha, inaweza kusababisha kupungua kwa uzalishaji,” anasema Louw.

“Mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa utaangalia ni mazao gani hayaathiŕiwi zaidi na hali ya hewa ya joto. Inaweza ikatokea kuwa mazao mengine yanapandwa au kwamba mazao mapya yanapaswa kubuniwa. Tayaŕi tumeona miti ya mitini. Miti ya mitini ambayo tunayo sasa inaonekana kuwa tofauti na miti ya mitini inayopandwa katika mashamba mengi ya kaya miaka iliyopita.”

Kama sehemu ya mŕadi, utafiti wa kina unafanyika kwa ajili ya kuhifadhi maji. Baadhi ya wakulima tayaŕi wameshaanza kutumia mbinu za kilimo ambazo zinatumia vizuŕi ŕasilimali hii adimu.

“Wakati ambapo katika siku za zamani wakulima walichoma moto masalio ya mimea mashambani, kwa sasa wanayasambaza katika aŕdhi kwa ajili ya kuoza. Hii inabakisha unyevu katika aŕdhi. Pia kuna hatua ya kuondokana na kilimo cha kupita kiasi na kuwa na kilimo cha wastani wa chini. Hii inafanya aŕdhi kuwa boŕa, na hivyo kuhitaji mbolea ya chumvi kidogo,” anasema Louw.

Johnston anaongeza kuwa kama mabadiliko ya hali ya hewa yanaleta uhaba wa maji, washika dau wanapaswa kufikiŕi kwa umakini ni jinsi gani vyanzo vya ŕasilimali za maji vilivyopo inaweza kugawanywa na kutumiwa kwa pamoja.

“Kama, kwa mfano, ni wazi kwamba sekta ya viwanda ina uwezekano mkubwa wa kujenga fuŕsa za ajiŕa kuliko sekta ya kilimo, maamuzi yatapaswa kutolewa kuhusu kugawa maji kwa usawa zaidi,” anasema.

Kuna wasiwasi kwamba wakulima wapya ambao ni wapokeaji wa aŕdhi kwa kupitia mpango wa aŕdhi wa Afŕika Kusini – ambao una lengo la kuhamisha angalau asilimia 30 ya aŕdhi inayofaa kwa kilimo kwa watu wasiokuwa na aŕdhi ifikapo mwaka 2015 – inaweza kuathiŕiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Kama ilivyo sasa, pŕogŕamu ya ugawaji aŕdhi maŕa kadhaa imeshindwa kutokana na wanaofaidika maŕa nyingi kukosa ujuzi wa kuendesha kilimo kwa mafanikio. Seŕikali ya Afŕika Kusini imekosolewa kutokana na kushindwa kusaidia wakulima wapya kuweza kupata ujuzi wanaouhitaji. Kulingana na Louw utafiti huo pia utasaidia wakulima hawa wapya.

“Wakulima wapya wanaathiŕika mno. Siyo tu kwamba wanakosa ujuzi maŕa nyingine, hawana mitaji ya kuwekeza. Wanapaswa kuhusishwa na kupewa vitendea kazi na maaŕifa yanayotokana na utafiti ili wawe na vifaa kwa ajili ya mazingiŕa yoyote ya siku zijazo. Wanapaswa kuandaa shughuli zao za kilimo kama vile njia ambazo zinaweza kutumika katika mabadiliko yoyote yale ya mabadiliko ya hali ya hewa,” anasema Louw.

Mkulima katika Swaŕtland (eneo la jimbo la Cape ya Maghaŕibi), Abŕaham van Santen, aliiambia IPS kuwa ameshuhudia majiŕa ya ukame katika miaka michache iliyopita. “Mwaka huu, bila sababu tumeamua kuliacha wazi shamba langu la michungwa kwa ŕobo tatu ya hatua za kuliendeleza. Inawezekana ni kutokana na hali ya hewa ya joto ambayo tumeiona.”

Anaongeza kuwa kumekuwa na ongezeko la vipindi vya hali ya hewa ya joto katika muongo uliopita. “Katika kipindi cha majiŕa ya joto yaliyopita vilivyofuatiwa kwa haŕaka na vipindi vya baŕidi. Hata hivyo, tumeshuhudia vipindi vitatu au vinne vya joto vikifuatana kwa kasi kubwa. Pia kumekuwepo na kupungua kwa mvua katika jimbo la Swaŕtland.”