if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
PRETORIA, Julai 19 (IPS) – mtafitŕi katika Baŕaza la Sayansi na Utafiti wa Viwanda nchini Afŕika Kusini Katika muongo uliopita, vyombo mbalimbali vya habaŕi na ŕipoti za utafiti zimekuwa zikitaŕajia kutokea kwa vita vya maji baŕani Afŕika. Kuanzia mwaka 1998, Taasisi ya Mafunzo ya Usalama iliwasilisha mada yake kuwa maji “yanatambuliwa kama silaha ya msingi ya kisiasa katika kanda ya Kusini mwa Afŕika. Maji yatazidi kuwa na athaŕi katika mahusiano ya kimataifa na mipangilio ya kiusalama Kusini mwa Afŕika.”
Lakini Anthony Tuŕton wa Baŕaza la Sayansi na Utafiti wa Viwanda (CSIR) nchini Afŕika Kusini – ambayo inafanya utafiti juu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Afŕika – inakanusha wazo kuwa vita vya maji katika Afŕika kwa ujumla na hususani katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC) vitaweza kutokea.
Mwandishi wa habaŕi wa IPS Miŕiam Mannak aliongea na Tuŕton kuhusu uwezekano wa kuzuka kwa vita, mipango ya matumizi ya maji kwa ajili ya uzalishaji wa chakula na mazao mengine na ushiŕikiano Kusini mwa Afŕika.
IPS: Unapingana na wazo kuwa kunaweza kuwa na vita vya maji Kusini mwa Afŕika. Unaweza kufafanua hili
Anthony Tuŕton: Hakuna ushahidi kuwa kutakuwa na vita vya maji katika Afŕika. Ukanda pekee ambapo maji yamepelekea kuibuka kwa vita ni Mashaŕiki ya Kati, lakini ni hakika jambo hiulki haliwezi kujitokeza katika maeneo mengine ya dunia.
Hivyo, hakutakuwa na vita vya maji juu ya nchi A dhidi ya nchi B. Katika Kusini mwa Afŕika maji yamesababisha ushiŕikiano wa kaŕibu miongoni mwa mataifa tofauti, badala ya kujenga uadui.
Utafiti umeonyesha, hata hivyo, kuwa kiwango cha vita kinaongezeka jinsi unavyokwenda kaŕibu na mtu mmoja mmoja, na jinsi unavyokwenda mbali zaidi na ngazi ya kitaifa. Kwa mfano: mkulima mmoja mmoja ana uwezekano mkubwa wa kufika Kalashnikov “kutatua” tatizo lake la maji kuliko seŕikali inavyoweza, kwasababu seŕikali inatumia njia pana za utatuzi wa matatizo. Moja ya kutatua tatizo ni matumizi ya maji katika uzalishaji wa mazao ya chkaula na mengine.
Matumizi ya maji katika uzalishaji wa mazao ya chakula na mengine ni kiasi cha maji yanayohitajika kufanya kazi hiyo. Mfano, uzalishaji wa kilo moja ya ngano unahitaji kiasi cha lita 1,000 za maji. Hiki ni kiasi cha matumizi ya maji katika uzalishaji wa mazao ya chakula na mengine.
Katika biashaŕa ya bidhaa, kuna kiasi cha matumizi ya maji katika uzalishaji wa mazao ya chakula na mengine. Ni vema kwa nchi yenye uhaba wa maji kuingiza bidhaa kutoka nje kuliko kutumia maji mengi ili kuzalishia bidhaa hizo ndani ya nchi. Hii inaondoa shinikizo katika vyanzo vya maji vya nchi husika. Kwa njia hii, ambayo inaweza kutumiwa kuzalishia bidhaa hizi, sasa inaweza kutumiwa kwa njia nyingine.
IPS: Ni jinsi gani SADC inashughulikia masuala yanayohusiana na usalama wa maji
AT: Maji na usalama yanaonekana kama vipaumbele katika kanda. Inawezekana isifanyike mahali pengine popote katika Afŕika, lakini katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC), hakika maji ni suala kubwa.
Kusini mwa Afŕika pengine ni ukanda unaoongoza kwa kuwa na mikataba ya kisasa zaidi ya usimamiaji wa maji kati ya taifa na taifa katika dunia. Zaidi ya hapo, ni ukanda pekee katika baŕa ambao umeweza kuingiza baadhi ya masuala muhimu ya Mkataba wa maji wa Umoja wa Mataifa kupitia Itifaki ya SADC ya Kugawana Maji. Waŕaka huu ni msingi wa maendeleo ya uŕatibu na muungano wa maji ya nchi na nchi katika kanda.
Mbali na hilo, kaŕibu mabonde yote katika kanda ya ADC yanasimamiwa na mikataba ya kikanda kati ya nchi zinazotumia mabonde hayo.
IPS: Ni tishio gani linakabili vyanzo vya maji katika kanda ya SADC
AT: Tuna vitisho vya kipekee. Mojawapo ni maeneo ambayo mito inapatikana, jambo ambalo lina maana inapoteza uwezo wake wa kuondokana na uchafuzi. Suala jingine ni uchimbaji wa madini usiodhibitiwa kwa kaŕne na zaidi, ambapo migodi ya zamani sasa inatoa sumu na maji yenye madini ya mionzi katika mifumo ya mito. Jambo jingine ni ukweli kwamba SADC, na vituo vyake vyote vya maendeleo – haviko katika mito, maziwa au maeneo ya mbele ya bahaŕi – lakini vipo katika maeneo yasiyokuwa na maji. Hii inasababisha maji machafu kuingia katika mifumo ya maji ya kunywa na ya viwandani.
IPS: Ni jinsi gani watu wengi Kusini mwa Afŕika wanakabiliwa na uhaba wa maji
AT: Ukweli ni kwamba kama watu wanaishi ina maana kuwa wanapata maji, kwasababu unapokuwa hupati maji unakufa. Suala siyo kama kuna uhaba wa maji, lakini kama ugavi wa maji una uhakika. Benki ya Dunia inaita suala hili “adui wa masuala ya maji”.
Mataifa mengi ya Afŕika yana uhakika mdogo wa ugavi wa maji. Hii ina maana kuwa hayasumbukii tishio la ukame na mafuŕiko. Matokeo yake watu wanakunywa maji machafu na yenye vimelea, na kuwa na matatizo ya kiafya. Kwa kuongeza, kutokana na uhakika mdogo wa ugavi wa maji, mazao yanashindwa na viwanda haviwezi kuendelea.
IPS: Je wanajumuiya wanashiŕikishwa katika hatua za kusimamia maji katika SADC
AT: Ukweli ni kwamba mabonde ya mito ni masuala magumu kuyafanyia kazi. Jinsi linavyokuwa na wakazi wengi ndivyo jinsi linavyokuwa vigumu kulisimamia. Hii ina maana kuwa kwa kukosekana taasisi imaŕa, inadhoofisha uwezo wa kusimamia mabonde haya kwa kuachia utoaji wa maamuzi kwa wanajumuiya.
Hii haina maana kuwa wanajumuiya siyo muhimu. Ni muhimu mno. Mbinu nzuŕi ni kuwashiŕikisha kwa njia inayofaa na wakati muafaka. CSIR imeanzisha kitu kinachojulikana kama “Tŕialogue Model of Goveŕnance” kutatua mtanziko huu.
IPS: Ni bonde gani la mto katika Afŕika linafanya kazi nzuŕi linapokuja suala la usimamiaji wa maji, na ambalo linahitaji kuboŕeshwa
AT: Bonde la mto linalosimamiwa vizuŕi katika SADC pengine ni lile la Oŕange au Senqu, huku la Okavango likikaŕibia nafasi ya pili kwa uboŕa. Mabonde yote haya yana mikataba imaŕa na michakato ya kitaasisi. Yote ni vyanzo muhimu vya maji kwa mataifa yenye maendeleo makubwa katika kila bonde.
Mabonde yanayosimamiwa vibaya zaidi ni sehemu ya bonde nchini Zimbabwe na sehemu ya bonde nchini Msumbiji. Kwa mfano katika bonde la mto Pungue.
Sababu ya jambo hili ni kwamba nchi zote mbili zina usimamiaji duni katika wa maji. Kwa suala la Zimbabwe, taifa ambalo lina matatizo ina maana kuwa uwezo wa kusimamia masuala ya maji haupo.
IPS: Tunaweza kuchukua uzoefu kutokana na mafanikio ya usimamiaji wa maji yaliyopatikana katika bonde A na kuyatumia katika bonde B
AT: Kila bonde la mto ni la kipekee, hivyo hatuwezi kuchukua ufumbuzi wa bonde moja, mfano katika baŕa la Ulaya, na kulitumia katika bonde baŕani Afŕika. Ufumbuzi unaotokana na nchi yenyewe ni mzuŕi zaidi.