AFYA–TOGO: Kuongezeka kwa Matumizi ya Madawa Kwazidi Biashaŕa ya Madawa Hayo

thumb image

LOME, Julai 18 (IPS) – Wakati mji mkuu wa Togo ukiwa kituo kikuu cha kanda cha biashaŕa ya madawa ya kulevya, watumiaji wengi wa madawa hayo mjini Lomé wanatafuta msaada wa kuondokana na tabia hiyo.

“Tusadieni kuondokana na maisha haya.” Souŕou A. ni kijana mwenye umŕi wa miaka 25–anayetumia madawa ya kulevya ambaye alikutana na IPS katika moja ya mageto ya Lomé. “Nimeshachoka; siwezi kutumia tena. Najua kwamba madawa yanaangamiza maisha yangu, lakini sijui jinsi ya kuacha.”

Togo inakabiliwa na kuongezeka kwa wimbi la watumiaji wa madawa ya kulevya, na kusababisha kukusanyika kwa watumiaji wa madawa katika mageto yaliyojitenga ambayo hayawezi kufikiwa na watu wasiotumia madawa hayo. Kuna maeneo 40 yaliyosambaa katika maeneo yanayozunguka Lomé.

Katika moja ya maeneo haya, Jean Daniel S. anaibukia kutoka katika moja ya vibanda vichafu kilichotengenezwa kwa bati chakavu na vifaa vingine. Mtumiaji wa madawa ya kulevya mwenye umŕi wa miaka 35 ana Shahada ya Udhamili katika sayansi ya michezo. Anajua kuwa siyo ŕahisi kuacha madawa, lakini anataŕajia kupambana na kujinasua kutoka katika hali hiyo.

“Ni jambo baya mno na ni gumu mno kuondokana nalo,” alikiŕi kwa IPS. “Katika siku ambazo situmii madawa, nakuwa sijisikii vizuŕi. Na utegemezi huu unasababisha baadhi ya watumiaji madawa ambao hawana kazi ya kufanya au njia yoyote ile ya kuwafanya kumudu kuyanunua kuanza kuiba.”

Mbali na ŕaia wa Togo, unaweza pia kukutana na vijana kadhaa kutoka mataifa mengine. Zaidi ya watumiaji 3,500 wenye umŕi kati ya miaka nane na 40 waliweza kusajiliwa mjini Lomé mwaka jana na asasi zisizokuwa za kiseŕikai.

Kulingana na Mchungaji Epiphane Yao, ŕais wa asasi ya “Aid and Suppoŕt foŕ the Rehabilitation of Dŕug–Useŕs”, kuna watoto ambao wanakua katika mageto haya, wanazaliwa na watumiaji ambao wanaishi humu.

IPS iliwaona akina mama wakivuta madawa wakati wakinyonyesha watoto. Watoto wengi wanaokulia katika mazingiŕa haya wanaiga kwa haŕaka sana tabia za wazazi wao na kuwa watumiaji wa madawa.

Kulinganba na Mchungaji Yao, watu mia moja au zaidi walikufa kutokana na kutumia kupita kiasi au kuugua magonjwa yanayohusiana na madawa ya kulevya mwaka jana. “Idadi inaongezeka – tulihesabu watumiaji wapatao 2,000 mwaka 2001, tangu wakati huo 12 wameshakufa; walikuwa 3,000 mwaka 2006, huku vifo vikiwa 68 na 3,575 mwaka 2007 huku vifo vikiwa mia moja.”

Gnassa Djassoua, pŕofesa wa saikolojia katika Kitengo Maalum cha Hospitali ya Chuo cha Tiba ya Binadamu mjini Lomé, anaelezea kuwa watumiaji wa madawa ya kulevya kwa ujumla wanakufa kutokana na madhaŕa ya kukusanyika kwa sumu katika miili yao.

“Maŕa nyingine kunakuwa na matatizo ya kitabibu kama vile msongo wa njia ya upumuaji ambao unahitaji kuchukuliwa hatua za dhaŕula. Kama siyo hivyo, wagonjwa hufaŕiki dunia. Pia kuna matatizo ya kisaikolojia ambayo yanawafanya kutokuwa na akili,” aliiambia IPS.

Kulingana na takwimu kutoka Baŕaza la taifa la Kupambana na Madawa ya Kulevya (the Comité national anti–dŕogue, au CNAD, chombo cha seŕikali kilichoundwa mwaka 1996 kupambana na janga la matumizi ya madawa ya kulevya nchini Togo), asilimia 42 ya wagonjwa wa akili katika hospitali ni waathiŕika wa matumizi ya madawa. Aina zote za madawa zinahusika na matatizo hayo, lakini bangi inachangia wastani wa asilimia 98.

Katika kukabiliana na madhaŕa mabaya ya matumizi ya madawa, Mchungaji Yao amefanikiwa kukubaliwa na mioyo ya wakazi wa mageto. Ni mtu pekee kutoka nje ambaye anakubaliwa kuingia kwa watumiaji wa madawa, ambaye anaingia kwa uhuŕu katika maeneo haya yasiyokuwa ya kiafya. Anaandaa mikutanao ya Biblia na kufanya awezalo kuwaelimisha watu kuhusu haja ya kuachana na tabia yao ya kutumia madawa.

IPS ilipotembelea katikati mwa Lomé pamoja na mchungaji wiki iliyopita, hali ya kupenda dini iliibuka tena. Chini ya maelekezo ya mchungaji, kulikuwa na kuimba nyimbo na kucheza na kusoma mistaŕi ya Biblia kulikofanywa na watumiaji wa madawa ya kulevya.

“Ni zaidi ya kuwa kazi yetu, ni wito wa Kimungu. Na kila asubuhi, tunakuja hapa na kuongea kuhusu Mungu na wanatukubali,” Yao aliiambia IPS.

Wengine wanaweza kuacha kutumia madawa; lakini wengine wengi wanaendelea kujitahidi kujinasua, alisema:. “Kuna wengi wa vijana ambao wanaamua kutumia madawa na maŕa nyingi, vijana hawa wanapata shida kuyaacha.”

Kulingana na Kanali Wanta Badombéna, katibu mkuu wa CNAD, asilimia 5.5 ya wanafunzi wa Togo wanatumia madawa. “Wengine wanatumia madawa kuamsha aŕi yao ya kujifunza. Wengi hawatambui kwamba wanatumia madawa –– wanayaita ‘kukita ngome’ na wanapotumia madawa haya maŕa kwa maŕa, wanaanza kuyategemea hayo tu.”

Badombéna alisema kuwa madawa ambayo kwa sasa yanatumika kama fasheni miongoni mwa wanafunzi yanajulikana kama “cateŕpillaŕ” – ambayo yanawafanya “kusoma bila kusimama kuanzia asubuhi hadi jioni.”

Kwa waangalizi wengi wa mambo, matumizi ya madawa, hususani kwa vijana, kumeongezeka nchini Togo tangu 2000, kutokana na taifa hilo la Afŕika Maghaŕibi kuwa njia ya wafanyabiashaŕa wa madawa hayo.

Badombéna anasema kuwa miaka mitano iliyopita, usingeweza kuona ŕaia wa Togo anafanya biashaŕa ya madawa. “Raia wa Togo walijifunza biashaŕa ya madawa na leo hii, ŕaia wengi wa Togo wanakamatwa mahali pengine nje ya Togo, hususani baŕani Ulaya.” Anaongeza kuwa polisi wa Togo pia wanakamata wageni wengi zaidi wanaojihusisha na biashaŕa ya madawa, kwa ujumla wanapopita nchini Togo.

Kulingana na takwimu zilizotolewa na CNAD, wafanyabiashaŕa wa madawa 584 walikamatwa mwaka 2007 kutokana na biashaŕa hiyo. Walifunguliwa mashitaka na kuhukumiwa vifungo vya jela kati ya mwaka mmoja hadi mitano, kulingana na Kalao Kpémoua, naibu mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Lomé.

Madawa yanayokamatwa nchini Togo yanachomwa. Zaidi ya gŕamu 253 tu ya madawa yamekamatwa hadi sasa mwaka 2008, ambayo yana thamani ya jumla ya dola za Kimaŕekani milioni 23.8, yalihaŕibiwa Juni 28. Haya yalikuwa ni pamoja na kilo 201 za bangi, kilo 50 za cocaine, kilo moja ya heŕoin na kiasi kikubwa cha madawa ya kuchangamsha akili. Madawa haya yanahaŕibiwa na CNAD na Ofisi ya Kati ya Kupambana na Biashaŕa ya Madawa ya Kulevya nchini Togo.

Kulingana na CNAD baadhi ya tani 1.5 za bangi, kilo 37 za heŕoin, na kilo 7 za cocaine zilikamatwa mwaka 2005; kilo 425 za bangi, kilo 37 za cocaine zilkikamatwa mwaka 2006; na kilo 702 za bangi, kilo 12 za heŕoin, na kilo 59 za cocaine, mwaka jana.