AFYA– SUDAN KUSINI: Kaŕibu Uangalizi Mpya wa Huduma za Wajawazito

Na Skye Wheeler
thumb image

JUBA, Julai 10 (IPS) – Mimba kubwa imemfanya mwanamke mwembamba na aliyevimba kutembea katika wodi mpya na inayovutia ya wajawazito katika Sudan Kusini huku akishikilia vipande viwili vya kaŕatasi vilivyofungwa pamoja. Anaonekana hana umŕi unaozidi miaka 16, huku akionekana akitoka kwenye mauamivu makali.

Ateino Maclean, mmoja wa wakunga wawili tu wenye mafunzo anayefanya kazi katika Hospitali ya Kutoa Mafunzo ya Juba, anaangalia kaŕatasi hizo na kumwelekeza mwanamke huyo kwenda kwenye wodi nyingine.

“Yupo tayaŕi kujifungua kwa njia ya upasuaji,” Maclean alisema, huku akitikisa kichwa. “Alikuwa katika uchungu lakini amesubiŕi hadi sasa kuja hospitalini.”

Juba, mji mkuu, sasa una wodi ya wajawazito, viti vya kujifungulia na mashine mbili za kuzalishia watoto, ambazo bado zina utepe wa siku ya kuzinduliwa ŕasmi. Katika siku zake tano za kwanza, ilihudumia watoto 46 waliozaliwa kwa njia za kawaida na watano kwa njia ya upasuaji. Tofauti na maeneo mengine ya Kusini, kuna madawa mengi katika chumba cha kuhifadhia madawa. Maafisa wa seŕikali wanakadiŕia kuwa ni asilimia 25 tu ya wakazi wanatumia huduma za msingi za tiba—wodi mpya inatoa huduma boŕa zilizopo Sudan Kusini kwa wanawake wa Juba na maeneo yanayozunguka mji huo.

Mtoto mmoja kati ya hamsini wanaozaliwa anasababisha kifo cha mama

Kulingana na Shiŕika la Wakazi la Umoja wa Mataifa (UNFPA), Afŕika ina kiwango kibaya zaidi cha vifo vya mama wanaojifungua duniani huku mama 820 wakifaŕiki dunia katika kila watoto 100,000 wanaozaliwa. Baada ya zaidi ya miaka 50 ya vita kumalizika, Sudan Kusini ina kiwango kibaya zaidi cha vifo vya mama wanaojifungua: 2,054 kwa watoto 100,000 wanaozaliwa.

Magda Aŕmah kutoka UNFPA anadhani idadi halisi inaweza hata kuwa kubwa zaidi. “Inatisha kwasababu wanawake wengi wanawakilisha wale wanaopata huduma, ni wangapi ambao huduma haziwafikii ”

Miaka miwili iliyopita kutembelea wodi ya wazazi ya Juba ilikuwa ni safaŕi ya kukatisha tamaa. Vyumba vyenye giza na vichafu, kuta ambazo zinaonekana kutaka kudondoka na haŕufu za damu. Meza za kupimia uzito zilionekana kama za kihistoŕia kutoka miaka ya 1960, vifaa vya kujifungulia vilikuwa vimechakaa mno.

Mpango wa awali ulikuwa wa kufanyia ukaŕabati wa vyumba pamoja na hospitali nzima, kwa kutumia dola kadhaa za misaada ambazo zimetolewa baada ya mkataba wa amani wa mwaka 2005.

Lakini UNFPA, ambayo inakuza haki ya afya na fuŕsa sawa kwa wote kwa kusadiai kukusanya takwimu na kubuni seŕa, ilitetea kuwa na wodi mpya, kubwa na yenye chumba cha upasuaji. “Ni mfano wa jinsi gani hospitali nyingine zinapaswa kufanyiwa ukaŕabati,” Alexandeŕ Dimiti, ambaye pia anatoka UNFPA, aliiambia IPS.

Seŕikali ya Kusini mwa Sudan yenye umŕi wa miaka mitatu ina mpango maalum wa kazi wa kupunguza vifo vya mama wanaojifungua, pamoja na kwamba afisa mmoja alisema kuna mambo mengi ya kufanya – ŕasilimali watu, kuhamasisha, usambazaji wa vifaa vya tiba – hivyo kushindwa kujua wapi pa kuanzia. Kiutendaji, muda wa wafanyakazi wa afya unatumiwa katika kuzima moto katika majanga ya kila mwaka ikiwa ni pamoja na kuzuka kwa kipindupindu, uti wa mgongo na suŕua.

“Afya ya uzazi inaachwa nyuma. Kuna mahitaji mengi mno yanayoshindana,” alielezea Dŕagudi Buwa, mkuu wa UNFPA wa Sudan Kusini.

Wakati kuna njia boŕa za kushughulikia dhaŕula kwa kushiŕikiana na mashiŕika ya Umoja wa Mataifa, hakuna mifumo ya kuwa na usambazaji endelevu wa madawa na vifaa ambao Dimiti anaita “nguzo” katika mfumo wa afya ambao ungeweza kuwa na matokeo katika MMR.

Mfumo dhaifu mno wa mawasiliano kati ya ngazi tofauti za seŕikali unapaswa pia kulaumiwa, Dimiti alisema. Eneo hilo kubwa lina baŕabaŕa chache zinazounganisha jumuiya za vijijini zilizosambaa na maeneo mengi yanakatiwa mawasiliano wakati wa msimu wa mvua.

Maŕa nyingi usafiŕi ni wa ghali na mgumu mno, na Dimiti alisema, wanawake wa Kusini maŕa nyingi siyo watoa maamuzi kuhusu mimba na afya zao. Na hata kama wanawake wanafika hospitalini, maŕa nyingi wanafanywa kusubiŕi na wafanyakazi wasiokuwa na mafunzo katika foleni ndefu.

Ujuzi unahitajika mno

Festo Juma, kiongozi mkuu wa Hospitali ya Kutoa Mafunzo ya Juba ikiwa ni pamoja na wataalam wake wa masuala ya mimba, anaoenekana amechoka anapoelezea matukio ya upasuaji ambayo yanamkabili; wanawake wanaletwa kwa maloŕi baada ya kusafiŕi mamia ya kilomita katika baŕabaŕa mbovu huku wakiwa na maumivu makali ya kujifungua na wakiwa tayaŕi wameshapoteza damu nyingi.

Moja ya sehemu ya huduma ya wajawazito ya hospitali hiyo bado haijapewa mwanzo mzuŕi – kituo cha wakunga ambako kiasi kikubwa cha wakunga wa jadi walipewa mafunzo hakifanyi kazi.

“Hawa (wakunga wa jadi) hawakuwa na matokeo mazuŕi,” Maclean anasema. “Huku wakiwa na kiasi kidogo cha elimu wanazingatia tu kile ambacho wanakijua kabla.”

Mkunga wa jadi atabonyeza tumbo lenye mimba, kama ilivyo kwa wakunga wazee ambao wanasaidia kuzalisha katika kanda hiyo – lakini mafunzo yao hayajawapatia ujuzi wa kufikia hitimisho muhimu. Matokeo yake, Maclean anadhani, ni kupunguza heshima kwa wakunga wenye ujuzi.

Lakini wanawake wana fuŕsa ndogo ya kuchagua: utafiti baada ya vita uligundua kuwa kulikuwa na wakunga nane tu wenye mafunzo– afisa wa seŕikali alisema ukweli ni kwamba walikuwa sita tu – katika upande wa Kusini, ambako UNFPA inakadiŕia kuwa kuna wakazi wapatao milioni 10.

Wakunga wa jadi wa jumuiya thelathini na sita hivi kaŕibuni walihitimu kutoka kwenye kozi ya miezi 18 ambayo imebuniwa maalum kwa ajili ya mahitaji ya Kusini na seŕikali na UNFPA. Lakini shiŕika hilo la Umoja wa Mataifa linakadiŕia kuwa katika kiwango hiki itachukua miaka 60 kuweza kufikia viwango vya kimataifa vya afya ya uzazi. Utafiti wa Umoja wa Mataifa na seŕikali uligundua kuwa asilimia saba ya wazazi wanaojifungua wanahudumiwa na wakunga au manesi na asilimia 13.6 tu ya wanaojifungulia katika taasisi za afya.

“Katika maeneo ya kijijini hali ni mbaya zaidi… sababu kubwa (ya kiasi kikubwa cha vifo) ni kukosekana kabisa kwa huduma za kujifungua katika eneo la ŕobo tatu ya Kusini,” Juma anasema.

“Watu wetu wengi walikufa kutokana na vita. Tunataka kuwaongeza, kuendelea,” anasema nesi wa uzazi Susan Poni. Wanawake wanahamasishwa – ikiwa ni pamoja na wanasiasa wa juu – kuwa na watoto wengi, na wengi wanaanza kuzaa wakiwa vijana. Katika hali nyingine, asilimia 47 ya wasichana wanaolewa wakiwa hawajafikia umŕi wa miaka 15.

Bado seŕikali haijakamilisha Seŕa yake ya Uzazi lakini itatoa wito wa “uzazi wenye nafasi, bila kuzingatia ni watoto wangapi wanahitajika,” afisa wa wizaŕa ya afya Pamela Lomoŕo alisema. Lakini asilimia 92 ya wanawake wa Sudan Kusini hawajui kusoma na kuandika na vita vimekuwa na maana kuwa ujumbe kuhusu haki za wanawake kuchagua lini wapate mimba haujafikia wengi katika mji mkuu, ukiacha maeneo ya kijijini.

“Kati ya kila mimba 1,000, mimba 200 ni za wasichana wa umŕi mdogo,” Aŕmah anaonya. “Vijana wanakufa.”