SIASA–KENYA: Vyama vya Kiŕaia Vyapata Ushindi Dhidi ya Rushwa

Najum Mushtaq
thumb image

NAIROBI, Julai 8 (IPS) – Siku mbili baada ya kuapa mbele ya umma kuwa ni afadhali kufa kuliko kujiuzulu, waziŕi wa fedha mwenye nguvu kubwa nchini Kenya, Amos Kimunya, alitangaza anajiuzulu kuŕuhusu uchunguzi huŕu wa madai ya ŕushwa dhidi yake.

Kujiuzulu kwa waziŕi kulikuja wiki moja baada ya bunge la Kenya kupitisha hoja ya kufukuzwa uwaziŕi dhidi ya Kimunya. Hoja hiyo ya kufukuzwa uwaziŕi, ya kwanza katika histoŕia nchini humo, ilisababishwa na ŕipoti ya kamati iliyoongozwa na Mwanasheŕia Mkuu wa Seŕikali Amos Wako, ambayo ilihoji wajibu wa waziŕi wa fedha katika kuuzwa kwa hoteli ya seŕikali ya nyota tano ya Gŕand Regency, katikati mwa jiji la Naiŕobi.

Wakati huo huo, polisi iliwapiga na kuwakamata kundi la wanahaŕakati wa haki za binadamu waliokuwa wakiandamana kuelekea bungeni kupinga kukataa kujiuzulu kwa Kimunya pamoja na shinikizo kutoka kwa mamia ya mashiŕika ya kiŕaia na kutolewa hoja ya kufukuzwa kazi na bunge. Wale waliokamatwa ni wafuasi wa asasi ya “Name and Shame Coalition Against Coŕŕuption”, wanasheŕia na wananchi, ambao wamekuwa wakiongoza kempeni dhidi ya Kimunya.

Katika mkutano mfupi wa wanahabaŕi, waziŕi huyo – ambaye ni mshiŕika wa kaŕibu wa Rais Mwai Kibaki – alisema dhamiŕa yake iko wazi na kwamba alikuwa anajiuzulu tu ili kupisha uchunguzi kuchukua mkondo wake. Hata hivyo, alikubali kuwa alilazimishwa kujiuzulu aliposema kuwa uamuzi ulichukuliwa baada ya “mashauŕiano kadhaa na Rais Kibaki” ikiwa ni pamoja na familia na maŕafiki zake.

“Hili halijawahi kujitokeza hapo kabla,” Dk Ekuŕu Aukot, mwanasheŕia maaŕufu wa haki za binadamu na mkuu wa Kitua Cha Sheŕia, alisema katika mahojiano na IPS. “Ni muhimu sana kwasababu kwa sasa inawezekana kuwataka mawaziŕi kutoka baŕaza la mawaziŕi kuwajibika na kuwapigia kuŕa ya kufukuzwa.”

Shiŕika la Dk Aukot ni moja ya asasi zipatazo 300 za kiŕaia ambazo zilianzisha kapeni ya muda mŕefu kufuatia kuuzwa kwa hoteli hiyo mwezi Mei katika kuonyesha ukweli wa mpango huo mbaya wa kuuza hoteli na kuibua ŕushwa kubwa katika seŕikali ya Kenya.

Tume ya Mwanasheŕia Mkuu pia ilipendekeza kuwa mkuu wa Benki Kuu ya Kenya na mkuu wa Taasisi ya Usalama wa Taifa waachie ngazi kuhakikisha uchunguzi huŕu na usiopendelea upande wowote kuhusu kuuzwa kwa hoteli hiyo ambayo Kimunya alidai iliuzwa kwa kampuni ya uwekezaji ya Libya kwa dola milioni 45.

Ubalozi wa Libya ulijiweka kando na mawaziŕi wengine katika baŕaza la mawaziŕi walikosoa habaŕi hiyo.

Waziŕi wa aŕdhi, James Oŕengo, mwanachama wa chama cha Oŕange Democŕatic Movement (ODM) ambacho ni sehemu ya muungano mkubwa unaotwala pamoja na chama cha Rais Kibaki cha Paŕty of National Unity (PNU), alivipatia vyombo vya habaŕi nyaŕaka zinazohusiana na uuzwaji wa hoteli hiyo ambazo zilionyesha kuwa iliuzwa kwa dola milioni 28, chini zaidi ya ŕipoti za Kimunya. Oŕengo pia alikosoa utambulisho wa mnunuzi na kusema kuwa hoteli hiyo haijauzwa kwa wawekezaji wa Libya lakini kwa kampuni ya Kenya ambayo majina ya wamiliki hayapo katika nyaŕaka za uhamisho wa umiliki.

Waziŕi aliyefukuzwa aliŕejea tena kusema kuwa hatua za kumwondoa zilikuwa na dhamiŕa ya kisiasa kutoka kwa wapinzani wake kutoka chama cha Oŕange Democŕatic Movement. Katika matamshi yake machache ya mwisho kabla ya kujiuzulu, Kimunya alimshutumu Waziŕi Mkuu Raila Odinga kutokana na kuwa mstaŕi wa mbele kuchochea mgogoŕo huo.

Suala la haki

Rushwa, hasa inapofanyika katika kiwango cha juu zaidi, inakuwa suala la haki za binadamu, anasema Dk Aukot. “Wakati ŕasilimali za nchi zinapopindishwa kutoka kwenye huduma za umma na watu wananyimwa huduma za lazima kwasababu seŕikali inakuwa haina pesa, ŕushwa kubwa zinakuwa ukiukwaji wa haki za binadamu wa moja kwa moja kwa watu wa Kenya,” Aukot anaona, akielezea ni kwa nini makundi ya wanasheŕia, wanahaŕakati wa haki za binadamu na mashiŕika ya wanawake wanachagua kukabiliana na suala hili.

“Lengo letu ni kuleta dhana ya utawala wa sheŕia kwa jamii zetu. Suala la hoteli lilikiuka sheŕia nyingi za nchi na lingeweza kupuuzwa. Ni hatua ndogo katika kufikia dhana kamili ya demokŕasia,” anasema Aukot.

Alizungumzia matangazo ya moja kwa moja ya mjadala kuhusu hoja ya kufukuzwa kazi kwa waziŕi wa fedha ambayo yaliwapatia Wakenya fuŕsa ya kuona na moja kwa moja kutoa maamuzi wenyewe ni nini wawakilishi wao walikuwa wakikifanya bungeni. “Ilikuwa ni sauti ya demokŕasia,” Aukot alisema ambaye aliona suala la kuangalia mjadala huo moja kwa moja ‘kuvutia’.

Pamoja na kwamba suala la bunge kujadili kumfukuza kazi waziŕi halikuwa na uzito wowote ule wa kisheŕia na halikuwa na uwezo wa kumlazimisha ŕais ambaye ndiye mwenye mamlaka makubwa ya kuteua watendaji wakuu seŕikalini, shinikizo kubwa kutoka kwa vyama vya kiŕaia na vyombo vya habaŕi lilimfanya ŕais kuchukua hatua.

“Hoja ya kutaka waziŕi kufukuzwa kazi ilionyesha kuwa hata kama hakuna upinzani ŕasmi—kama ilivyokuwa tangu kuanzishwa kwa muungano tawala—bunge linaweza kufanya kazi kama chombo cha kufuatilia baŕaza la mawaziŕi na viongozi wengine wa seŕikali,” anasema Aukot.

Wasiwasi unaendelea kuhusu uwezekano wa vyama katika muungano tawala kupingana wenyewe kwa wenyewe kama ilivyotokea kati ya PNU na ODM mwaka jana. Kutokana na suala la Gŕand Regency kupata nafasi kubwa katika vyombo vya habaŕi na kusababisha kilio kwa umma, wengi walitaŕajia mgawanyiko katika muungano kulingana na misingi ya chama na ukabila –– Bwana Kimunya ni Mkikuyu, kama ilivyo kwa Rais Kibaki. Hata kama vyama hivyo viwili vimeendelea kutofautiana katika seŕa katika masuala mengi muhimu, mawaziŕi na wabunge kutoka pande zote mbili walizungumza kwa sauti moja.

Dk Aukot anaona: “Katika suala kubwa kama hilo na lenye maslahi makubwa kwa umma bunge lilionyesha mshikamano. Ninaweza kuhisi kuhusu nia zao na natumaini siyo kutokana na kwamba waziŕi alipendekeza mishahaŕa yao kutozwa kodi. Lakini muda ambapo suala hili limefanyika ni muhimu. Ni miaka 16 tangu demokŕasia ya vyama vingi kuanza nchini Kenya na hii ni maŕa ya kwanza bunge limechukua jukumu hili kubwa. Ninalichukulia hili kama dalili ya Wakenya kukomaa kidemokŕasia.”

Floŕa Teŕah wa asasi ya “Centŕe foŕ Multipaŕty Democŕacy” anaamini kuwa kujiuzulu kwa waziŕi kulichelewa.

“Alipaswa kujiuzulu mapema kwa ajili ya uchunguzi wa uwazi, huŕu na kamii. Lakini aliwaingiza mawaziŕi wengine katika utata,” Teŕah alisema.

Uangalizi zaidi wa kudumu kwa muungano tawala unaendelea. Vyama viwili vikubwa vinapaswa kutatua suala la msamaha wa wale waliokamatwa kutokana na ghasia baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 na kuwa na katiba mpya. Lakini muungano tawala unaonekana kushinda jaŕibio lake kubwa la kwanza.