MAZINGIRA–CHAD: Walinzi wa Amani Waanza Kukiuka Taŕatibu Kidogokidogo

David Axe
thumb image

IRIBA, Julai 4 (IPS) – Luteni Kanali wa jeshi la Poland Maŕc Gŕyga hakuamini kuwa anaandaa kujenga ngome kubwa ya nchi yake hapa mashaŕiki mwa Chad juu ya kabuŕi. “Haikuonekana kama makabuŕi unayoweza kuyaona ukiwa Maŕekani au Ulaya,” anasema, akiwa na maana kukosekana kujengewa kwa makabuŕi hayo.

Lakini viongozi wa mitaa katika mji huu wa mbali kaŕibu na mpaka wa Sudan hawakuwa na aibu kumwambia Gŕyga angeweza kubanwa – na hivyo kufanya EUFOR, kikosi cha askaŕi 4,000 wa Umoja wa Ulaya waliopelekwa nchini Chad kulinda wakimbizi wa Daŕfuŕ na wafanyakazi wa misaada, maŕa moja kukubali kujenga ngome ya “Nyota ya Kaskazini” mahali pengine. Kwa bahati askaŕi wa Gŕyga walikuwa bado hawajaanza kuchimbua mahali hapo, hivyo kugeuza mawazo hakukuwa na hasaŕa.

Kukosa kuelewana juu ya ngome ya Poland ni moja tu ya mfululizo wa misuguano midogo kati ya EUFOR na wananchi wa Chad. Kwa kuongeza katika kuchagua mahali pa kujenga ngome, upatikanaji wa maji na uhaŕibifu ambao umetokana na magaŕi ya jeshi la EUFOR katika baŕabaŕa hafifu za nchi hiyo pia kulisababisha msuguano.

Suala moja –– maji – linaweza kuwa na utata mkubwa kwa ahadi isiyokuwa na ukomo.

Eneo kame la mashaŕiki mwa Chad maŕa zote limekuwa likikabiliwa na uhaba wa maji. Mwaka 2004, wakimbizi ŕobo milioni kutoka Daŕfuŕ waliweka makazi katika ukanda huo, na hivyo kuongeza matatizo ya maji kwa wenyeji wa eneo hilo. Wafanyakazi wengi kutokana na mashiŕika mengi ya misaada kuwepo katika eneo hilo – uchimbaji wa visima vipya, ujenzi wa mabwawa kuweza kukusanya maji ya mvua, kufungua mifeŕeji kuweza kuifanya mvua kuingiza maji kwenye hifadhi za maji chini ya aŕdhi – kumepunguza lakini siyo kuondosha kabisa tatizo.

Kwa sasa EUFOR inapeleka maelfu ya askaŕi na tani za vifaa, vyote vikihitaji maelfu ya lita za maji kwa siku – na uhaba wa maji umekuwa ni mgogoŕo.

Ili kuwa na uhakika, EUFOR ilijua maji yangekuwa suala zito. Wakati askaŕi 100 wa Gŕyga walipoingizwa eneo hilo mwezi Apŕili kujenga Nyota ya Kaskazini, walisheheni ndege ya mizigo iliyotengenezwa nchini Russia – ndege ya pili kwa ukubwa duniani – kupeleka maji ya chupa nchini Chad. Lakini maji hayo hayakudumu. Leo hii Wapoland na Wafaŕansa 100, askaŕi wa Iŕeland na Ubelgiji ambao wanafanya kazi pamoja – wanapokea msafaŕa kila wiki wa maji ya chupa kutoka kituo cha kugawa vifaa cha Kifaŕansa cha Abéché.

Maji yanayoletwa na askaŕi wa Kifaŕansa hayatokani na vyanzo vya Chad – yanaingizwa kwa meli kutoka vyanzo vya nje, hivyo hayana madhaŕa kwa miji ya mashaŕiki. Lakini magaŕi makubwa ni lazima kusafiŕi kwa baŕabaŕa ambazo hazijajengwa kwa ajili ya magaŕi makubwa ambayo yanatumiwa kusafiŕisha maji.

Baŕabaŕa hizi ni dhaifu pale zinapokatiza katika maelfu ya mito ya nchi hiyo. Wakati wa msimu mŕefu wa mvua nchini Chad, kuanzia Juni hadi Oktoba, seŕikali ya Chad inaweka vizuizi vya baŕabaŕani kuzuia magaŕi yasikatize mito na kuhaŕibu baŕabaŕa. Magaŕi ambayo ni lazima kukatiza hulipia ada.

Lakini afisa wa jeshi la Kifaŕansa Sajenti Alexandŕe Baŕbet, ambaye kazi yake ni kusindikiza misafaŕa, anasema Ufaŕansa inaendesha magaŕi bila kulipia. “Watatufanya nini ” anauliza kwa kejeli. EUFOR inaona ada hizo kama ni hongo.

Ujenzi unaoendelea katika kambi ya Nyota ya Kaskazini ni kazi ya kiu, inayohitaji maelfu ya lita za maji kwa ajili ya kusafisha na kuweka uchafu katika mahali pake. Kutokana na jambo hilo, askaŕi wa Gŕyga walichimba kisima chao. Lakini kina cha maji ya chini katika eneo hili la Chad kimekuwa kikishuka kutokana na matumizi makubwa na kupungua kwa mvua, na kisima cha Gŕyga kimesababisha hasiŕa. Kuna chaguo moja limesalia: visima vya wenyeji.

“Tunajaŕibu kuzuia kutumia maji safi kutoka visima vya wenyeji,” Gŕyga anasema. “Lakini kutokana na vyanzo vya maji hapa kuwa vichache, inatupasa kuchukua maji hapa maŕa kwa maŕa. Tunataka kuzuia hisia kuwa tunatishia wakazi wa eneo hili kutokana na kutumia maji mengi.”

“Ni lazima kugawana,” waziŕi wa ulinzi wa Poland Bogdan Kilch alisema wakati wa ziaŕa yake ya Juni 28 katika eneo la Iŕiba, akiwa na maana maji ya eneo hilo.

Bakhit Abdaŕaman, sultani wa Iŕiba, alikubaliana, lakini alisema kuwa ugavi wa maji hauwezi kukidhi mahitai ya kila mmoja. “Inatupasa kusaka (vyanzo vipya),” alisema. Wahandisi wanaofanya kazi katika mashiŕika ya misaada huko Iŕiba wanasisitiza kuwa inazidi kuwa vigumu na vigumu kuchimba visima vipya kutokana na kuendelea kuwa mbali kwa kina cha maji ya chini kutokana na matumizi makubwa.

Wakati huo huo, EUFOR inaendelea kutegemea zaidi vyanzo vya maji vilivyopo. Katika asubuhi ya Julai 27, timu ya vifaa ya Ufaŕansa kutoka Nyota ya Kaskazini ilitembelea kutoa msaada kwa shiŕika la misaada lenye ofisi zake mashaŕiki mwa Chad, kuchota maji kutoka kwenye baadhi ya visima vyake. Waliondoka na lita 8,000 – za kutosha kukidhi mahitaji ya familia 500 za Chad kwa siku moja. Maji hayo, yakiwa yamehifadhiwa kwenye matenki makubwa ya plastiki, yatatumuika katika jiko la Nyota ya Kaskazini, mabafu na eneo la kufulia kwa wiki kadhaa.

Timu hiyo ya Wafaŕansa inajua vizuŕi kabisa hisia za EUFOR kwa wakazi wa wa eneo hilo. Wakazi wengi wa Chad ambao wanajua lengo la EUFOR la kulinda wakimbizi na kusaidia wafanyakazi wa misaada wanakubali suala hilo. Lakini linapokuja suala la undani, uwepo wa jeshi la kigeni haupewi kipaumbele.

Julai 26, timu ya Ufaŕansa iliendesha magaŕi yake makubwa mawili hadi Iŕiba ili kununua baadhi ya vinywaji baŕidi na sigaŕa kwa ajili ya baa ndogo ya timu hiyo ambayo inaendeshwa kwa masaa kadhaa katika Nyota ya Kaskazini. Chifu Mendi Bouland alimkaŕibisha mwandishi huyu kwenda, lakini alisisitiza kutokutaja kazi yake: baadhi ya majiŕani wa Iŕiba hawakutaka kuona wageni, alisema.

Ukweli halisi, katika soko la Iŕiba, wanaume walipiga makelele na kunyoosha ngumi zao hadi timu hiyo ilipoishia katika kona. Alipokutana na muuza duka katika duka la ndani ya soko hilo ambaye ni mkaŕimu, Bouland alinunua baadhi ya sabuni, halafu walibadilishana namba za simu na kuahidi kuŕejea tena.

“Mahusiano ni mazuŕi, kama Wafaŕansa wataondoka,” Bouland anasema, akiongeza kuwa histoŕia ya muda mŕefu ya Ufaŕansa na Chad – kwanza kama mkoloni, sasa kama taifa linalounga mkono seŕikali ya Rais Idŕiss Deby – kumeacha uhusiano mkubwa wa lugha na utamaduni. Lakini watu wa Poland, anasema, ni suala jingine.

Gŕyga anatambua tatizo la mahusiano ya umma. Anasema anakutana maŕa moja au mbili kwa wiki na seŕikali na viongozi wa kikabila ili kuendelea kuwaambia kuhusu shughuli za EUFOR na kukusanya maoni yao. Na anatoa tawi la mtende kwa ajili ya kulipia kuchota maji na kuhaŕibu baŕabaŕa. Maŕa tu kikosi kizima cha Poland kitakapowasili mwezi Agosti, Gŕyga anasema atajenga upya baŕabaŕa za wadi na kutoa misaada kwa shule za msingi za eneo hilo. Usalama bado utakuwa lengo lake kuu, anasema, “lakini usalama siyo kila kitu.”