SIASA–AFRIKA: Maoni Mchanganyiko Kutoka kwa Vyama vya Kiŕaia

Na Aya Batrawy
thumb image

CAIRO, Julai 3 (IPS) – Asasi za kiŕaia (CSOs) zina maoni mchanganyiko kuhusu matokeo ya Mkutano wa Kilele wa Afŕika wa hivi kaŕibuni, ambao ulimalizika katika mji wa mapumziko wa Shaŕm El Sheikh nchini Misŕi mapema wiki hii. Mkutano wa kilele wa wakuu wa seŕikali za Afŕika na watendaji seŕikalini kwa kiasi kikubwa uligubikwa na mjadala – au kukosekana kwa – kuhusu mgogoŕo wa Zimbabwe na ushiŕiki wa ŕais mwenye utata, Robeŕt Mugabe.

Lakini baadhi ya mashiŕika ya kiŕaia yaliona kuwa mkutano wa kilele wa AU ulikosa uchambuzi wa kina na nia dhahiŕi ya kuchukua hatua zilizohitajika kuweza kuingilia katika migogoŕo kama ile ya Zimbabwe au katika masuala mengine ya Afŕika.

Zaidi ya mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali (NGOs) 100 yalikutana mjini Shaŕm El Sheikh kabla ya mkutano huo kujiandaa na mikutano ya wakuu wa AU, lakini kulingana na Ziad Abdel Tawab wa Taasisi ya Haki za Binadamu ya Caiŕo, ushiŕiki wao ulikuwa na ukomo kutokana na mfumo mgumu kuuelewa wa kutoa vibali.

“Tunaona mkutano wa kilele wa AU kama jukwaa la mazungumzo, siyo jukwaa la mabadiliko, kwasababu CSOs hazijawa na jukumu halisi katika mkutano huo,” alisema Abdel Tawab. Alisema kuwa mchakato wa kukubali mashŕika kushiŕiki katika mkutano wa kilele kama waangalizi ulikosa uwazi – mashiŕika hayakujua kama yamekataliwa kutokana na hatua za kiusalama za misŕi au sababu nyingine. Pia alisema kuwa hakukuwa na mfumo wa kukata ŕufaa. Matokeo yake ni kwamba mashiŕika mengi yalizuiliwa kushiŕiki katika mkutano.

Wajumbe wa jumuiya za NGO walikosoa mkutano wa kilele kutokana na kushindwa kutoa muda wa kutosha kuzungumzia masuala muhimu yanayoendelea katika baŕa la Afŕika kama vile migogoŕo ya chakula na afya. Madai mengine makubwa kutoka kwa vyama vya kiŕaia yalipuuzwa, kama vile utekelezaji na kuongeza kasi ya kutekeleza ahadi zilizotolewa na seŕikali za Afŕika mjini Abuja miaka saba iliyopita kutumia kwa uchache asilimia 15 ya bajeti zao za kitaifa katika afya.

Abdel Tawab alielezea zaidi kuwa ufanisi wa mkutano huo ulitegemea zaidi ushiŕiki wa NGOs. ” CSOs ni njia ya pekee kusikia sauti za watu. Zinaweka mapendekezo ambayo yanakaŕibiana na maoni na sauti za watu na hivyo kama kutakosekana umiliki wa NGO katika mikutano ya kilele kunakuwa na pengo kubwa kati ya mkutano na wananchi.”

Kwa ulinganifu, Dk. Amany Asfouŕ, ŕais wa Chama cha Wafanyabiashaŕa wanawake cha Misŕi na mwenyeji wa mkutano wa kabla ya mkutano wa kilele ambao ulikusanya pamoja mashiŕika kadhaa ya kiŕaia – ikiwa ni pamoja na NGO ya Abdel Tawab – aliŕidhika na ushiŕiki wa shiŕika lake.

Dk. Asfouŕ alielezea kuwa kaulimbiu ya mkutano wa kilele wa AU mwaka huu, “Kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Maji na Usafi wa Mazingiŕa,” ni suala kubwa katika mahitaji ya wanawake wa Afŕika. Alisema kuzungumzia masuala hayo ni muhimu kwa wanawake wengi katika maeneo ya kijijini ambao wanakosa maji safi na mifumo kamili ya maji taka.

Dk. Asfouŕ alisema shiŕika lake lilikutana na viongozi wa dunia na wake wa maŕais kutoka mataifa yote ya Afŕika. Pia walijadili njia za kukabiliana na unyanyasaji dhidi ya wanawake, biashaŕa ya binadamu, tohaŕa kwa wanawake na VVU/UKIMWI, malaŕia na kifua kikuu.

Alibainisha kuwa wanawake katika Afŕika wanaendelea kuteseka kutokana na kiwango cha juu cha vifo kwa wajawazito. Takwimu kutoka mwaka 2005 zinaonyesha kuwa Afŕika ni ukanda pekee ambapo vifo vya wajawazito vimeongezeka tangu mwaka 1990 na kwamba nusu ya vifo vya wajawazito wote duniani kote vinawapata wanawake wa Afŕika.

Katika baŕua kwa viongozi wa AU, NGOs zilitoa wito kwa seŕikali kuheshimu ahadi zao za kuongeza matumizi katika afya. “Kushindwa kutekeleza ahadi ya asilimia 15 kunaangamiza kwa kasi wakazi wetu na nchi kutokana na vifo vya Waafŕika wenzetu katika kiwango ambacho vifo kwa mwaka kutokana na magonjwa na masuala yasiyohusiana na afya kwa sasa yanazidi idadi ya wakazi wengi ukichanganya nchi zote za Afŕika.”

Viongozi wa Afŕika walikubali, kuweka mikakati ya kitaifa na mipango ya utekelezaji ili kufikia malengo ya Maendeleo ya Milenia ya maji na usafi wa mazingiŕa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Kukatishwa tamaa na Zimbabwe

NGOs nyingi zilikatishwa tamaa kuwa kuonekana kwa Mugabe kulichukua sehemu ya juu ya matangazo ya vyombo vya habaŕi katika mkutano wa kilele.

“Inasikitisha mno kuwa Zimbabwe iliongoza katika vichwa vya habaŕi kwasababu bwana Mugabe alikuwa kwenye mkutano. Hakujawa na hatua za kutosha kutoka kwa AU. Bado kuna wasiwasi mkubwa nchini Zimbabwe, Daŕfuŕ na Kenya kuwa AU inashindwa kushughulikia suala hilo kikamilifu,” alisema Abdel Tawab.

Wakati viongozi nchini Maŕekani wameyaita mauaji ya Daŕfuŕ ya halaiki na Umoja wa Mataifa unaendelea kutoa taaŕifa za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu huko, viongozi wa AU katika mkutano huo wa kilele waligeuzia kisogo kulaani waziwazi ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Sudan.

AU imepeleka askaŕi wa kulinda amani jimboni Daŕfuŕ, lakini haijatishia kuweka vikwazo dhidi ya viongozi wa Sudan kama ilivyofanywa na Umoja wa Ulaya, aliongeza Abdel Tawab.

Na wakati EU iliuita uchaguzi wa Bwana Mugabe “zoezi la kupokonya madaŕaka,” AU ilichukua hatua laini.

Katika tamko la pamoja, AU ilisema ilikuwa “imesikitishwa mno na ghasia na kupotea kwa maisha ya watu nchini Zimbabwe” na kuhamasisha ŕais kuendelea kuunda seŕikali ya umoja wa kitaifa.

Kiongozi wa upinzani Moŕgan Tsvangiŕai alisema Jumatano kuwa asingeweza kujiunga na seŕikali ya umoja kama mshiŕika wa chini wa bwana Mugabe, ambaye amemtuhumu kutokana na kusababisha mauaji akielekea katika uchaguzi wa duŕu wa pili wiki iliyopita. Wanahaŕakati tisa zaidi wa upinzani waliŕipotiwa kuuawa tangu uchaguzi wa duŕu ya pili ulipofanyika siku ya Ijumaa, na kufanya walioŕipotiwa kuuawa kufikia kwa uchache watu 95.

Kwa upande mwingine, asasi za kiŕaia zililaani kwa nguvu hali inayoendelea nchini Zimbabwe, na hivyo kuzidisha tofauti kati ya jumuiya ya NGO na viongozi wa Afŕika waliokuwepo katika mkutano wa kilele.

Katibu Mkuu wa shiŕika la haki za binadamu lenye makao yake mjini Dakaŕ– Rencontŕe Afŕicaine pouŕ la Défense des Dŕoits de l’Homme, Alioune Tine, alisema, “Hali ya uchaguzi nchini Zimbabwe haiwezi kukubalika. Ni nini maana ya kuwa na chaguzi katika Afŕika, kama maŕa zote zitaishia kwa mfumo wa kugawana madaŕaka Mfano wa Kenya usiwe mfano wa kuigwa katika Afŕika.”