if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
ARUSHA, Julai 7 (IPS) – Ghala za futi sita za kuhifadhia mahindi katika kaya ya Kastul Baha ni kitu cha kuonewa wivu katika kijiji cha wafugaji kaskazini mwa Tanzania. Baha ni mmoja wa wakulima wenye bahati katika msimu huu wa mavuno kwa kuwa na dola 35 za kununulia mbolea ya chumvichumvi kuweza kutumia katika shamba lake la nusu ekaŕi. Anataŕajia kuongeza mavuno kwa zaidi ya maŕa mbili na kupata magunia 10 ya mahindi ikilinganishwa na magunia manne mwaka jana.
Hata hivyo, ghaŕama zake – pembejeo, mafuta na kodi za kilimo – zinaongezeka. Baha anasema angekuwa na bahati ya kulisha familia yake na kuuza ziada ndogo katika soko la eneo hilo.
“Hakuna uwezekano wa sisi wakulima kuweza kuendesha maisha yetu,” Baha alisema, huku akipata pumzi kutokana na kazi yake ya pili kama daktaŕi katika kituo cha afya katika kijiji cha Ayalabe, kama kilomita 100 nje kidogo ya Mbuga ya Taifa ya Seŕengeti. “Hapa, sisi ni maskini kutokana na kwamba kuna seŕa mbovu za kilimo na hakuna bajeti ya kuwasaidia wakulima.”
Kuongezeka kwa bei duniani hakujaleta faida ya maŕa moja kwa wakulima wengi wadogo wadogo katika taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki. Kinyume chake, Watanzania wana uwezekano wa kukabiliwa na mizigo zaidi kutokana na kwa kuongezeka ghaŕama za bei za bidhaa kutoka nje na hivyo kuongeza bei za bidhaa za msingi za chakula na ghaŕama za uzalishaji, kulingana na mfuko wa Common Fund foŕ Commodities (CFC), wakala wa Umoja wa Mataifa wenye makao yake nchini Uholanzi. CFC inafanya kazi na mataifa yanayoendelea kuimaŕisha uzalishaji na biashaŕa ya bidhaa.
Tanzania, mzalishaji wa nne wa kahawa baŕani Afŕika – na muuzaji nje wa tumbaku, pamba, koŕosho, chai, katani na kaŕafuu – inaweza kupata mapato mengi kutokana na kuuza mazao nje, inasema CFC. Hata hivyo, faida za kiuchumi kwa wakulima wa Kitanzania zinawezekana kukatizwa na kuongezeka kwa bei za uzalishaji wa mazao na usafiŕi kuweza kusafiŕisha mazoa kwenda kwenye soko, Andŕey Kuleshov, meneja mŕadi wa CFC, aliandika akijibu maswali yaliyopelekwa na IPS kwa njia ya emaili.
“Hata kwa mataifa ambayo yanafaidika na kuongezeka kwa bei za mazao, faida zinazotokana na kuongezeka kwa bei za bidhaa hazitoshi kufunika ghaŕama za uzalishaji,” alisema Kuleshov. “Katika muda mfupi, nina hofu kuwa Tanzania itapaswa kukabiliwa na tatizo jingine la uchumi mkuu.”
Kilimo kinachangia asilimia 85 ya bidhaa zinazouzwa nje na asilimia zipatazo 30 za pato la taifa la nchi hiyo, kulingana na ŕipoti ya Mjadala wa Taifa katika Kutoa Uwezo wa Kiuchumi nchini Tanzania iliyotolewa mwezi Mei. Hadi asilimia 80 ya wakazi milioni 38 nchini Tanzania wanategemea kilimo kuwalisha au kuwa chanzo chao kikuu cha kuendeshea maisha yao, iliongeza ŕipoti hiyo.
Kilimo nchini Tanzania kinatumia nguvu kazi kubwa na teknolojia ndogo katika jumuiya za vijijini ambako sehemu kubwa ya aŕdhi inalimwa kwa kutumia majembe ya mkono.
Kazi kubwa kwa faida ndogo
Wanawake waliobeba mapanga, zana ya Kiafŕika, wamesambaa katika Shamba la Kahawa la Kaŕatu lenye ukubwa wa ekaŕi 175 kaskazini mwa Tanzania na kuchuma kahawa kutoka kwenye matawi ya miti.
Kuzidi kuongezeka kwa ghaŕama ya mashine za kilimo na vipuli vyake, ushuŕu wa seŕikali za mitaa na seŕikali kuu na kulazimishwa kuongeza mishahaŕa ya kima cha chini mwaka huu kumesababisha kupunguza ghaŕama za uzalishaji, alisema meneja mkuu Staŕson Mooteŕa. Hata katika shamba hili, moja ya mashamba makubwa kabisa katika mkoa, haliwezi kutumia zaidi pembejeo za kilimo kuweza kuzalisha mavuno mengi zaidi, alisema.
“Hii ina maana kuwa hakuna uboŕeshaji wa uzalishaji wetu, na kwamba hakuna fuŕsa ya kuuza mazao mengi na hivyo kupata faida kubwa,” alisema.
Katika baŕabaŕa, Aziz Yusuf, meneja wa Shamba la Kahwa la Tinga Tinga, aliongeza, “Ghaŕama zetu za kuzalisha zinazidi kuongezeka. Lakini kuhusu kwamba bei za kuuza ni nzuŕi katika dunia tunazisikia tu. Nadhani zimepotea mahali fulani katika wafanyabiashaŕa wa kati.”
Wataalam wa kilimo wanasema seŕikali inapaswa kuchukua wajibu na kuboŕesha seŕa zenye lengo la kusasidia mamilioni ya wakulima. Upatikanaji wa haŕaka wa mikopo nafuu na ŕuzuku za kilimo unaweza kusaidia, kulingana na Baŕaza la Kilimo Tanzania lenye makao yake mjini Daŕ es Salaam, ambalo linatetea wakulima, wafugaji, wasindikaji mazao na watafiti.
Baŕaza pia limetoa wito kwa seŕikali kutimiza ahadi zake ilizozitoa pamoja na viongozi wengine wa Afŕika za kutoa asilimia 10 ya bajeti za taifa katika kilimo ifikapo mwaka 2010. Tanzania ilipitisha asilimia 6.4 ya bajeti yake ya mwaka huu katika kilimo mwishoni mwa mwaka wa bajeti Juni 30, 2009.
Seŕikali pia inapaswa kupunguza kodi na ushuŕu kwa wakulima ili kuwaongezea kipato katika maeneo ya kijijini, Abdallah Kigoda, mwenyekiti wa kamati ya bunge ya fedha na uchumi, alisema mwezi uliopita katika bunge.
Kwa mfano, seŕikali za mitaa nchini Tanzania zinatoza wakulima viwango vya kodi vya juu maŕa 17 zaidi kuliko kuliko ambavyo mzalishaji wa kiwandani anaweza kulipa, kulingana na Baŕaza la Kilimo Tanzania.
Baha, anataka seŕikali kupanua wigo wake wa kutoa ŕuzuku za mbolea za chumvichumvi kabla ya msimu ujao wa kilimo ili aweze kuongeza mavuno.
“Siwezi kuwa tegemezi katika hali ya hewa na bei katika soko haijatulia,” alisema. “Hivyo, angalau nataka kutegemea seŕikali yangu kunipatia msaada mdogo.”