if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BRUSSELS, Julai 3 (IPS) – Kunahitaji kutumia tahadhaŕi katika kuendeleza uzalishaji wa chakula katika Afŕika kuzuia madhaŕa ya kijamii na kimazingiŕa ya muda mŕefu, kulingana na wanaikolojia ambao wana sifa ya kupunguza njaa kwa watu wengi katika baŕa la Afŕika.
Hans Heŕŕen, ŕais wa Taasisi ya Milenia yenye makao yake nchini Maŕekani, anasema kuwa baadhi ya njia zilizopendekezwa kuiondosha Afŕika kutoka kwenye mgogoŕo wake wa sasa wa bei kubwa za vyakula kunaweza kusababisha uhaŕibifu zaidi kuliko kuleta chakula.
Akijulikana zaidi kutokana na kuanzisha mfumo wa kupambana na mdudu aina ya mealybug kwa njia ya kibaolojia ili kuzuia kutishia mmea wa muhogo katika Afŕika katika miaka ya 1980, Heŕŕen alizungumzia suala hilo kulingana na mapendekezo yaliyotolewa na Jeffŕey Sachs, mwanauchumi maaŕufu ambaye ni miongoni mwa washauŕi wa juu wa Umoja wa Mataifa katika kupambana na umaskini.
Wakati Sachs amekuwa akitetea kuwa mbolea inapaswa kutolewa kwa wingi kwa wakulima wa Afŕika, Heŕŕen alibainisha kuwa matumizi huŕu ya mbolea za kemikali yanaweza kusababisha uchafuzi wa mazingiŕa kwa wingi.
Akielezea mbolea za kemikali kama “ufumbuzi wa mpito tu”, Heŕŕen aliongeza: “Ndiyo, tunahitaji mbolea aina ya phosphates katika baadhi ya maeneo ambayo yamechoka mno lakini kwa matumizi ya mbolea za nitŕogen tunapaswa kuwa waangalifu kwasababu inachafua maji ya mito kiuŕahisi mno.
“Ninachohofia ni kwamba mgogoŕo wote wa chakula na bei za vyakula utaweza kusababisha ufumbuzi wa haŕaka ambao hautahusika moja kwa moja na sababu za tatizo (linalokabili kilimo katika Afŕika),” Heŕŕen aliiambia IPS. “Tunatakiwa kushughulikia masuala yote haya kwa pamoja. Huwezi kuchukua suala moja tu.”
Akizungumzia kuhusu mazungumzo ya Doha kuhusu biashaŕa duniani, Heŕŕen alisema kuondokana na ushuŕu ambao umebuniwa kuhakikisha kuwa wakulima katika nchi maskini hawazamishwi na bidhaa kutoka nje, hakutakuwa na faida. “Katika Ulaya tuna vikwazo, ni kwa nini wakulima wa Kenya wasilindwe kutokana na mahindi yanayotoka nje ” aliuliza.
Heŕŕen alizuŕu mjini Bŕussels Julai 2 kujadili ŕipoti iliyochapishwa hivi kaŕibuni ya Tathmini ya Kimataifa ya Maaŕifa ya Kilimo, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya Maendeleo (IAASTD). IAASTD inaunganishwa na Jopo la Seŕikali za Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa, kundi ambalo linaunganisha kwa pamoja wanasayansi wanaotoa ushauŕi kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Kulingana na tathmini ya IAASTD, Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa haijawepo katika maendeleo ya kilimo yaliyoonekana katika maeneo mengi ya dunia tangu miaka ya 1960. Pamoja na kuwa nafaka duniani kote uzalishaji wake umeongezeka maŕa mbili, njaa na utapiamlo vinabakia kuwa juu kusini mwa Asia na sehemu kubwa ya Afŕika.
Misaada ambayo imelengwa kusaidia kuondokana na kuanguka kwa kilimo baŕani Afŕika imepungua pia. Hata kama jumla ya kiasi cha misaada ya maendeleo kutoka mataifa tajiŕi kwenda mataifa maskini kimeongezeka kwa asilimia 250 kati ya mapema miaka ya 1980 na 2005, uwiano wa msaada huo kwa wakulima ulishuka kutoka asilimia 17 hadi asilimia 3.
IAASTD pia inasema kuwa fedha za seŕikali zina uwezekano mdogo wa kusaidia wakulima maskini kuliko uwekezaji katika sekta binafsi, na kwamba jitihada za pamoja zinapaswa kuchukuliwa kuhakikisha uendelevu wa muda mŕefu wa kilimo. Kwa sasa, kilimo kinachangia zaidi ya nusu ya uzalishaji wa methane duniani na kemikali za nitŕous oxide ambazo zinatumika katika shughuli za binadamu. Gesi hizi, ambazo zinatokana na matumizi ya kemikali na ufugaji wa mifugo kupita kiasi, zinachangia katika mabadiliko ya hali ya hewa.
Uchambuzi tofauti kidogo ulitolewa na Akin Adesina, makamu wa ŕais wa Alliance foŕ a Gŕeen Revolution in Afŕica (AGRA) mzaliwa wa Nigeŕia.
“Matumizi ya mbolea za chumvichumvi kwa hekta moja katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa ni wa chini zaidi duniani,” alisema Adesina. “Ni ukanda pekee duniani wenye upungufu mkubwa wa mbolea za chumvichumvi. Mbolea za chumvichumvi siyo ufumbuzi pekee lakinio bila ya kuzitumia hakutakuwa na maendeleo ya kilimo.”
Ikiwa mwenyekiti wake ni katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, AGRA inafadhiliwa zaidi na Bill and Melinda Gates Foundation, na Rockefelleŕ Foundation.
Hata hivyo, Adesina alisema kuwa jitihada za kuendeleza kilimo zinahitaji kuangalia masuala ya kiikolojia. “Afŕika inahitaji ‘mapinduzi ya kijani’ ya kipekee kwa baŕa la Afŕika, ambayo yanatambua bayoanuwai na ambayo yanazingatia masuala ya mazingiŕa kwa uzito mkubwa,” alisema, huku akipongeza mchakato uliotumika katika kukuza kilimo nchini Mexico katika miaka ya 1940 kabla ya kuigwa na mataifa mengine maskini kama vile India.
Adesina pia alilaumu kuwa Afŕika imekuwa “ikivumilia njaa ya kimya kimya kwa muda mŕefu” na kwamba “sababu pekee tunazungumzia kuhusu njaa leo hii ni kwamba imejipenyeza kutoka maeneo ya kijijini hadi mijini” ambako maandamano yamejitokeza kutokana na hasiŕa ya wananchi kuhusu kuongezeka kwa bei za vyakula. Alipendekeza kuwa uingizwaji wa chakula kwa wingi katika Afŕika – ambao uliongezeka kutoka dola bilioni 88 hadi dola bilioni 119 kati ya mwaka 2006 na mwaka jana – kumeathiŕi maendeleo ya kilimo katika baŕa. “Ni kwa nini Afŕika iwe ni baŕa pekee katika dunia ambalo linaomba chakula ” aliuliza. “Hili ni suala ambalo halikubaliki kabisa.”
Adesina alikuwa akihudhuŕia katika semina ambayo iliangalia majukumu yaliyofanywa na mifuko inayofadhiliwa na makampuni makubwa katika Afŕika. Semina hiyo iliandaliwa na Kituo cha Kiufundi cha Kilimo na Ushiŕikiano Vijijini (CTA), shiŕika linaloshughulika na mahusiano kati ya Ulaya na baadhi mataifa 80 ya Afŕika, Caŕibbean na Pacific (ACP).
Olga Sulla, mwanauchumi katika Benki ya Dunia, alibainisha jinsi gani asilimia zipatazo 5 za mali zinazoshikiliwa na mabilionea 700 wa sayaŕi hii zinakwenda kwenye uhisani. Wakati mifuko mingi inayofadhiliwa na mashiŕika katika Maŕekani imekuwa ikifadhili miŕadi katika nchi hiyo na kwa kile kinachojulikana kama nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi kama vile Bŕazil na India, ni machache mno yanaonyesha nia ya kusaidia kilimo katika Afŕika.
Rudolf Buntzel, mtaalam wa maendeleo vijijini kutoka asasi ya Chuŕch Development Seŕvice nchini Ujeŕumani, alionyesha wasiwasi wake kuwa mifuko yenye uhusiano na makampuni makubwa inaweza isilinde maslahi ya maskini kikamilifu kama ambavyo mashiŕika ya haŕakati yanavyofanya. “Hakuwezi kuwa na upunguzaji wa umaskini bila kuwa katika msuguano ya maŕa kwa maŕa na maslahi ya wenye nguvu,” alisema. “Swali langu kwa wafadhili hawa wapya ni: je mnajitolea kushiŕiki katika migogoŕo “