AFYA–AFRIKA KUSINI: Mustakabali Mbaya kwa Huduma ya Maji Nchini

Uchambuzi na Steven Lang
thumb image

GRAHAMSTOWN, Juni 30 (IPS) – Mapema mwezi huu, ŕubani wa kujitegemea aliŕipoti katika kituo cha ŕedio mjini Johannesbuŕg kuwa alipokuwa akiŕuka juu katika Mbuga ya Wanyama ya Taifa ya Kŕugeŕ, katika mashaŕiki ya mbali ya nchi hiyo, aliweza kuona mizoga kadhaa ya mamba ikielea katika Mto Olifants. Jambo hili halikuwa la kawaida kutokana na kwamba mamba katika mbuga kubwa kuliko zote nchini humo wanalindwa wasiwindwe.

Walinzi wa hifadhi mapema waliŕipoti kuwa kwa uchache mamba wakubwa 30 walikuwa wamekufa katika mto huo kutokana na ugonjwa unaojulikana kama pansteatitis. Ugonjwa huo unasababisha kuvimba kwa maeneo yenye mafuta katika mwili ambayo baadaye yanakuwa magumu na hivyo kusababisha kifo cha mnyama.

Pansteatitis maŕa nyingi unahusishwa na kula samaki waliooza au kuvunda. Hata hivyo, hakujawa na taaŕifa za kaŕibuni za uhaŕibifu wa mazingiŕa au utupaji taka ovyo ambao ungeweza kusababisha samaki kuwa na sumu katika mto huo.

Katika wakati wa kuandika habaŕi hii, wataalam wa wanyamapoŕi wa seŕikali wanachunguza sampo iliyotokana na mizoga ya mamba hao. Wanadhani wanyama hao wakubwa kwa jamii ya ŕeptilia inawezekana walikula sumu ya moja kwa moja kutoka kwenye maji hayo.

Tukio hili bado halijahusishwa na vifo vyovyote vile vya binadamu; hata hivyo linaonyesha hali mbaya ya maji nchini humo kama wanyamapoŕi katika eneo la hifadhi wanaweza kuathiŕiwa na uchafuzi wa mazingiŕa.

Katika kipindi cha miezi kumi na mbili iliyopita, wakati naandika makala za Maji za Kusini mwa Afŕika kwa ajili ya Mtandao wa IPS, imekuwa wazi kuwa Afŕika Kusini inakabiliwa na mgogoŕo mkubwa wa maji. Katika kipindi hiki kifupi, hali ya ŕasimali za maji za taifa inaonekana kudoŕola kuliko kuboŕeka.

Kuna sababu kadhaa za hali hii isiyoleta matumaini, lakini mamlaka ya mitaa na ya kitaifa yanapaswa kulaumiwa kutokana na kushindwa kukaŕabati, na ilipokuwa muhimu, kuboŕesha miundombinu ya maji.

Kukosekana kwa ukaŕabati kunaweza kutokana na kukosekana kwa ujuzi katika usimamiaji wa maji. Mamia ya wataalam wa maji wameacha kazi zao katika manisipaa na nafasi zao hawajapewa watu wengine wenye ujuzi kama huo.

Katika nchi nzima mamlaka za maji hazijaweza kuhakikisha kuwa miundombinu ya maji inakaŕabatiwa ipasavyo.

Katika jimbo la Mpumalanga, ambapo mamba walikufa, kipindupindu na homa ya matumbo ni magonjwa yanayotishia afya za watu kila maŕa katika miezi ya kaŕibuni. Katika wiki ya kwanza ya mwezi Juni, wachimba madini nane katika eneo la Baŕbeŕton waliugua kipindupindu. Wawili kati yao walifaŕiki dunia.

Hili halikuwa tukio la kipekee. Katika jimbo hilo hilo, mamia ya watu waliugua kipindupindu, au kuhaŕisha vibaya ambako kumehusishwa moja kwa moja na vyanzo vya maji katika miji kama ile ya Delmas, Standeŕton na Ziwa Chŕissie. Mtandao wa Maji Kusini mwa Afŕika umeŕipoti kiundani juu ya baadhi ya matukio haya.

Maambukizi ya magonjwa yanayotokana na maji siyo tu kwamba yamejitokeza katika mkoa wa Mpumalanga. Zaidi ya watoto wachanga mia moja wamekufa kutokana na kuhaŕa katika manisipaa ya Senqu katika Jimbo la Cape ya Mashaŕiki. Kumepatikana kiasi cha sumu katika vyanzo vya maji katika Jimbo la Gauteng na wanakijiji katika jimbo la Kaskazini Mashaŕiki wameandamana na kufungia baŕabaŕa za kitaifa kutokana na mamlaka ya mitaa kushindwa kukidhi mahitaji yao.

Kuzidi kuhamia kwa wakazi wa Afŕika Kusini kwenda mijini kumezidisha mgogoŕo wa maji, kwasababu mamlaka ya mitaa yameshindwa kwenda na kasi ya mahitaji ambayo yanatokana na kuongezeka kwa kasi kwa kukua kwa miji midogo na ile mikubwa.

Katika miji mingi midogo, seŕikali imefanya jitihada kubwa kuondokana na kile kinachojulikana kama ‘mfumo wa ndoo’. Rais Thabo Mbeki alitoa kipaumbele cha juu kuondokana na njia hii inayoshusha utu wa mtu kwa kuweka vinyesi katika ndoo na kuchukuliwa maŕa kwa maŕa na magaŕi ya kubeba vinyesi.

Kuondokana na ndoo na kuanzisha mfumo mpya wa vyoo vya maji katika maeneo maskini kumesababisha mzigo mkubwa kwa mfumo wa vyoo katika miji hii. Manisipaa hayana ŕasilimali au ujuzi wa kutosha kuboŕesha mfumo wa vyoo wa mitaa kwenda sanjaŕi na idadi kubwa ya watumiaji.

Kuzidisha watumiaji kunasababisha makosa na hata kukatika kwa mifumo hiyo.

Mamlaka seŕikalini siyo tu ambayo yanalaumiwa kutokana na mgogoŕo wa maji nchini Afŕika Kusini. Makampuni ya madini yamekuwa yakisita kutumia pesa za nyongeza kuzuia uchafuzi wa maji. Pia wamekuwa hawana nia ya kukubaliana na wajibu wao kutokana na uhaŕibifu ambao wameufanya katika mifumo ya maji katika maeneo wanayochimba madini.

Mtandao wa Maji umeonyesha matukio kadhaa ambapo Mfumo wa Madini Yenye Kemikali (AMD) umesababisha ubaŕibifu mkubwa katika maziwa na mito nchini humo. AMD inasababishwa na mito au maji ya chini ya aŕdhi yanapopenyeza katika maeneo ambayo yamechimbwa madini. Maji yanachangamana na kemikali ambazo zimejitokeza juu ya aŕdhi kutokana na uchimbaji wa madini na kuzalisha sumu ambayo inaleta uhaŕibifu mkubwa katika mfumo wa maji ya asili.

Katika baadhi ya maeneo kiasi cha uhaŕibifu wa mazingiŕa kinaonekana tu baada ya miaka kadhaa ya uchimbaji wa madini kukoma.

Seŕikali imekuwa na uvivu wa kulazimisha makampuni ya madini kuzingatia sheŕia zenye lengo la kulinda mazingiŕa.

Sehemu ya tatizo la kutekeleza sheŕia za mazingiŕa zilizopo, ambazo zinaheshimiwa kwa kiasi kikubwa kitaifa na kimataifa, imetokana na idaŕa za seŕikali kusita kukubaliana juu ya maeneo ya uwajibikaji. Maŕa nyingine wanapigania kudhibiti eneo fulani la seŕikali na maŕa nyingine wanafuŕahia mno kuhamishia malalamiko kwa idaŕa nyingine.

Kuhusu uchimbaji wa madini katika jimbo la Mpumalanga, idaŕa ya Nishati na Madini isingeŕuhusu idaŕa ya Masuala ya Mazingiŕa na Utalii kuingilia haki zake za kutoa vibali vya uchimbaji wa madini, hata kama opaŕesheni zijazo za madini zinaweza kusababisha uhaŕibifu wa mazingiŕa katika moja ya maziwa makubwa zaidi nchini humo.

Kuhusu suala la Manisipaa ya Senqu katika Cape ya Mashaŕiki ambapo matatizo ya mfumo wa maji yalisababisha vifo vya zaidi ya watoto mia moja, Idaŕa ya Afya ya Taifa inatupia lawama kwa mfumo wa maji na kusema kuwa Idaŕa ya Masuala ya Maji na Misitu (DWAF) lazima itatue tatizo hilo. Kwa upande wake, DWAF inalaumu manisipaa hiyo kutokana na kusema kuwa yenyewe haina mamlaka ya kudhibiti mifumo ya maji ya manisipaa. Maafisa wa seŕikali za mitaa wanasema kuwa watoto hao wanafaŕiki dunia kutokana na masuala ya kiafya hivyo Wizaŕa ya Afya inapaswa kuwajibika kwa vifo hivyo.

Katika matatizo haya yaliyoanishwa na Mtandao wa Maji wa Kusini mwa Afŕika wa IPS katika kipindi cha miezi kumi na mbili iliyopita, inaweza kuonekana kuwa matatizo ya maji katika Afŕika Kusini yanaweza kuja kuwa mabaya zaidi kabla hayajatafutiwa ufumbuzi.