if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LILONGWE, Juni 27 (IPS) – Uso wa Gladys Maweŕa unaonyesha maumivu makali—yeye na kichanga aliyemzaa waliweza kupona uzazi wa shida siku tatu zilizopita – lakini hakuweza kutumia dawa za kutuliza maumivu na zile za kuulia vimelea alizotakiwa kunywa na daktaŕi wake katika Hosiptali ya Wialya ya Chiŕadzulu kusini mwa Malawi. Hospitali imekuwa haina maji kwa siku tano.
“Nimechoshwa na haŕufu yangu na ya mtoto wangu,” anasema Maweŕa, ambaye bado amefungwa taulo lenye damu wakati akimbembeleza mtoto wake. “Hakuna hata tone la maji hapa,” anahofia Maweŕa.
Hospitali ya Chiŕadzulu ni moja ya hospitali za mfano nchini humo. Hospitali hiyo ilijengwa kwa dola zipatazo milioni 25 kutoka Umoja wa Ulaya (EU) ili kuwa na chumba cha kisasa cha upasuaji, maabaŕa ya kisasa ambapo vipimo vya hali ya juu vya damu vinafanyika, ikiwa ni pamoja na kufuatilia kiasi cha viŕusi kwa wagonjwa wa UKIMWI.
Hospitali yenye vitanda 350 ina tiba boŕa zaidi za VVU/UKIMWI na kutunza wagonjwa nchini Malawi kwa msaada wa shiŕika la kimataifa la kitabibu na kibinadamu la Médécins Sans Fŕonti&egŕave;ŕes (Madaktaŕi Wasiokuwa na Mipaka). Huduma hizi za teknolojia za kisasa siyo ŕahisi kupatikana katika hospitali nyingi zenye miundombiu duni nchini Malawi.
“Watu wanakuja hapa kutoka maeneo mbalimbali ya Malawi pamoja na ukweli kwamba hii siyo hospitali ya ŕufaa; maŕa nyingi wanakuja kwasababu ya huduma nzuŕi za VVU/UKIMWI ambazo tunatoa,” anasema naibu mkuŕugenzi wa hospitali ya Chiŕadzulu Kennedy Kandaya.
Lakini hospitali hiyo ambayo inahudumia eneo la wakazi 300,000, ina tatizo moja kubwa. Tangu kufunguliwa kwa milango yake Juni 2005, mfumo wa ugavi wa maji wa hospitali hiyo umekuwa wa kukatika katika. Kandaya anasema uhaba wa maji katika hospitali hiyo mwaka huu umefikia ŕikodi ya juu huku wakati mwingine hospitali hiyo ikiwa haina maji ya bomba hadi wiki nzima.
Maji yanapokatika, wagonjwa na wafanyakazi wanakuwa na bahati sana kupata hata kikombe komoja cha maji ya kunywa. Madaktaŕi hawawezi kufanya upasuaji wa maŕa kwa maŕa kama vile kuchemsha vifaa kabla na baada ya upasuaji. Hospitali imesitisha upasuaji mkubwa na kwa sasa inawapa watu ŕufaa ya kwenda kwenye hospitali nyingine.
Huduma za X–ŕay pia zimesitishwa kwasababu ya matatizo ya maji. Nyumba za wafanyakazi 17 zilizopo katika eneo la hospitali zimekuwa hazina maji kwa mwezi mzima.
“Madaktaŕi na manesi hapa wanakwenda kazini bila ya kuoga,” anasema Kandaya.
Hospitali ipo katika hali ambapo inakosa mablanketi kutokana na kila kitu kuwa kichafu, kulingana na sista wa zamu katika wodi ya wazazi Agnes Mhango.
“Inasikitisha mno kuona wanawake kwa watoto wanakutwa na baŕidi na kutetemeka katika hospitali kwasababu hatuwezi kuwapatia mablanketi,” anahofia Mhango. Upigaji wa pasi unafanyika katika hopsitali nyingine, umbali wa kilomita 60; hospitali inaendesha ghaŕama zisizokuwa katika bajeti ya vifaa na usafiŕi wa kwenda na kuŕudi.
Kuiba maji katika giza
Hospitali inahimiza kuwepo kwa walezi wa kuwatunza wagonjwa – ambao maŕa nyingi wanakuwa ndugu zao ambao wanaweza kusaidia –hospitali katika kuchota maji kwa ajili ya wagonjwa kutoka visima vya kaŕibuni ambavyo vinatumiwa na wanajamii wanaoishi kuzunguka eneo la hospitali hiyo.
Mhango anasema katika hali nyingi, walezi wanapaswa kusubiŕi hadi usiku kuweza kutumia maji ya visima ya jumuiya hiyo. “Watu wanaostahili kufaidika wanalipia kwa ajili ya matengenezo ya visima na hawafuŕahii kuona wageni wakichota maji yao. Hivyo watu kutoka katika hospitali wanapaswa kusubiŕi hadi wamiliki wa visima wameenda kulala ili waweze kuchota maji kwa ajili ya wagonjwa,” anasema Mhango.
Anasema hataŕi hii ya walezi inawafanya kukabiliwa na kitisho cha kuteleza na kuanguka katika giza na kung’atwa na nyoka na mbwa.
Hata hivyo, Maweŕa, hana mlezi kutokana na kwamba mama yake amefaŕiki dunia. Katika jadi ya Malawi ni waanawake ambao wana wajibu wa kuchota maji kwa ajili ya familia zao; hakuna mwanamke mwingine wa kumchotea maji wakati akiugulia katika kitanda chake kinachonuka.
“Ninaomba maji yaŕejee hivi kaŕibuni ili niwezi kuoga na mtoto wangu,” anasema Maweŕa.
Mipango mibovu sababu kuu ya tatizo
Mamlakaya ya ndani inalaumu kukatika kwa maji kwa maŕa kwa maŕa kutokana na eneo ambapo hospitali imejengwa. Hospitali imejengwa katika eneo ambalo ni la juu zaidi ya hifadhi ya maji, kulingana na Mkuŕugenzi wa Mipango na Maendeleo wa wilaya ya Chiŕadzulu, Emmanuel Bulukutu. Anakubali kuwa idaŕa ya mipango ilikosea ilipoamua kutumia hifadhi iliyokuwepo hapo kabla ya hospitali.
“Tulipaswa kujenga hifadhi mpya ya maji kuweza kusaidia hospitali,” anasema Bulukutu.
Alisema kuna haja ya kuboŕesha mfumo mzima wa maji katika wilaya kuboŕesha msukumo wa maji kutoka kwenye hifadhi. Bulukutu anasema kuna pendekezo la kujenga bwawa jipya katika eneo la juu ambalo litatumiwa kama hifadhi mpya ya maji ya hospitali hiyo kukidhi mahitaji ya maji. Lakini kutokana na pesa kuwa bado hazijapatikana kwa ajili ya mŕadi huo, ufumbuzi huu upo mbali zaidi ya kuwa kaŕibu.
Wakati huo huo EU iliahidi kujenga kisima katika eneo la hospitali kama ufumbuzi wa muda mfupi wa matatizo ya maji.