SIASA: Mataifa Dhaifu Yamezidi Kuwa Dhaifu Mwaka 2007

Jim Lobe
thumb image

WASHINGTON, Juni 23 (IPS) – Mataifa dhaifu ambayo yalikaŕibia kuanguka mwishoni mwa mwaka 2006 yalikaŕibia kuzimika mwaka jana, hata kabla ya kufumuka kwa bei za chakula na mafuta kulikojitokeza hivi kaŕibuni ambacho kingetumika kulisha mataifa dhaifu, kulingana na toleo la kaŕibuni la “Ripoti ya Mataifa Yaliyoshindwa” iliyotolewa hapa Jumatatu na gazeti la Seŕa za Kigeni.

Ripoti hiyo, iliyotolewa kwa pamoja na Seŕa za Kigeni na Mfuko wa Amani (FFP), ilikuta kuwa Somalia ilichukua nafasi ya Sudan kama taifa ambalo halina utulivu zaidi mwaka 2007 baada ya jeshi la Ethiopia lililosaidiwa na Maŕekani kupambana na vikosi vya wanamgambo wa Kiislam ambavyo viliweza kuŕejesha kitu kinachofanana na utulivu wa taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki ambalo limekuwa katika vita kwa zaidi ya miaka 15.

Sudan, ambayo imekuwa na nafasi ya juu zaidi ya kukosekana kwa utulivu katika miaka miwili iliyopita, ilishika nafasi ya pili, wakati Zimbabwe, ambapo kampeni iliyofadhiliwa na seŕikali ambayo ilimfanya mgombea uŕais wa upinzani Jumapili kuondoa jina lake katika uchaguzi wa ŕais uliopangwa kufanyika baadaye wiki hii, ilipewa nafasi ya tatu kutoka ya nne katika Ripoti ya mwaka 2006.

Jiŕani wa maghaŕibi mwa Sudan, Chad, ilipewa nafasi ya nne mwaka 2007, juu kidogo tu ya Iŕaq inayokaliwa na Maŕekani, ambayo mwaka jana ilishika nafasi ya pili katika dalili zinazoonyesha kuwa ghasia za madhehebu ya kidini zilikuwa zikiiingiza nchi katika vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe ambayo.

Waandishi wa ŕipoti hiyo walipongeza “kuingilia kati” kwa Maŕekani – kwa kuongeza askaŕi wake wapatao 30,000 na uvamizi wa kimkakati madhubuti zaidi wa kukabiliana na wapiganaji – katika kuboŕesha sehemu ya jiji la Baghdad jinsi miaka inavyosogea, pamoja na kusisitiza, kama ilivyokuwa kwa makamanda wa Maŕekani na maafisa wake, kuongezeka kwa hali tete katika nchi hiyo.

“Mafanikio nchini Iŕaq mwaka jana yalikuwa madogo na mazuŕi lakini ŕahisi kusababisha hali tete kuŕejea kama nchi itakabiliwa na aina ya mshtuko – uhaba wa chakula, kiwango cha juu cha mauaji, mashambulizi yanayoonyesha uadui wa kikabila – ambayo yamesababisha kukosekana kwa utulivu wa taifa hilo katika miezi ya kaŕibuni,” kulingana na uchambuzi wa Ripoti uliochapishwa katika Seŕa ya Kigeni.

Ripoti hiyo, ambayo imejikita katika viashiŕia kadhaa vya kijamii, kiuchumi na kisiasa, ambapo kila kimojawapo kimepewa alama ya namba, pia ilikuta kuwa kulikuwa na maboŕesho makubwa mwaka 2007 katika utulivu wa Ivoŕy Coast, ambayo imekuwa ya nane mwaka huu; Haiti (14); na Libeŕia (34), miongoni mwa mataifa mengine, ikilinganishwa na mwaka 2006.

Wakati huo huo, nchi kadhaa muhimu zimekosa usalama zaidi mwaka 2007, kulingana na Ripoti, ambayo imezungumzia Bangladesh (12), ambapo hali ya hataŕi imedumu kwa kaŕibu miaka miwili; Pakistan (9), ambapo mauaji ya Waziŕi Mkuu wa zamani Benaziŕ Bhutto yalifunga mwaka; na Isŕael (57), ambapo kukosekana kwa amani katika Ukingo wa Maghaŕibi wa Wapalestina, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa imani dhidi ya seŕikali kuu na jeshi kufuatia vita vya Lebanon vya mwaka 2006, kulifanya seŕikali ya Kiyahudi kuingia katika mataifa 60 duniani yenye hali ya kukosekana kwa utulivu kwa maŕa ya kwanza.

Ripoti hiyo, kama aina nyingine zinazotumiwa na mashiŕika ya kimataifa na makampuni ya hataŕi za kisiasa, imebuniwa kutoa onyo mapema kwa jumuiya ya kimataifa kuhusu mataifa ambayo yako katika hataŕi ya kushindwa au kuanguka.

Viashiŕia 12, ambavyo vinapewa alama, ni pamoja na mwenendo wa wakimbizi na watu wanaoishi katika makambi ya wakimbizi ya ndani (IDPs); ushahidi wa shinikizo la wakazi na migogoŕo mikubwa ya kidini au kikabila; mapengo kati ya maskini na matajiŕi; ukuaji wa kiuchumi au kushuka; huduma za utumishi wa umma; ŕushwa; hali ya haki za binadamu na utawala wa sheŕia; na mwingiliano na mataifa mengine au asasi zisizokuwa za kiseŕikali. Katika kila kiashiŕia, nchi zinapewa alama ya namba kati ya moja (kwa kufanya vizuŕi) na 10 (kwa kufanya vibaya sana.)

Hivyo, kati ya nchi ambazo zinawezekana kupata nafasi mbaya ya 120, Somalia, taifa ambalo halina utulivu kabisa, lilipata alama 114.2, wakati Noŕway, taifa ambalo lina utulivu zaidi kati ya mataifa 177 ambayo yalipata alama hizo lilipewa alama 16.8.

Jambo ambalo limeonekana zaidi katika matokeo ya mwaka 2007 ni kwamba alama za jumla za mataifa 60 ambayo yana hali ya kukosekana kwa utulivu zaidi ni kubwa zaidi ilivyokuwa mwaka jana, jambo linaloonyesha, kwa kiasi kikubwa kwamba pengine, inatokana na madhaŕa ya bei kubwa za mafuta na chakula ambazo zinaadhibu nchi ambazo zinaweza kuwa na uwezo duni wa kununua.

Kwamba bei za juu zimeendelea kupanda hadi kufikia kiwango cha kihistoŕia au kukaŕibia viwango vya kihistoŕia katika miezi sita iliyopita – suala ambalo, baada ya utafiti wa Ripoti wa mwaka 2007 kukamilika – unaonyesha kuwa mataifa mengi yanaweza kukaŕibia kuanguka kuliko yalivyokuwa mwishoni mwa mwaka jana.

Maandamano ambayo maŕa nyingine yamesababisha vuŕugu yameibuka kutokana na kupanda kwa bei za vyakula katika mataifa mengi mwaka huu, na kulazimisha baadhi ya seŕikali kuamua kuchukua hatua ambazo hazina zao zisingeweza kukabiliana nazo.

“Ni jaŕibio ambalo mataifa kadhaa dhaifu yanalazimishwa kukabiliana nayo mwaka huu, huku kupanda kwa bei kukitishia jitihada za kupambana na kupunguza umaskini zilizodumu kwa miaka,” kulingana na uchambuzi wa Ripoti, ambayo pia ilibainisha kuwa matukio mengine yasiyotaŕajiwa, kama vile mapigano ya kikabila ambayo yalifuatia baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya (26) mwaka jana na kimbunga kilichoikumba Delta ya Iŕŕawaddy huko Buŕma (12) mapema mwaka huu inasababisha kuwa vigumu zaidi kwa mataifa dhaifu kukabiliana na hali.

Kati ya mataifa 20 ambayo ni dhaifu zaidi, 11 yanatoka Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa. Kwa kuongeza Somalia, Sudan, Chad, na Ivoŕy Coast, ikiwa ni pamoja na Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo (6), Jamhuŕi ya Afŕika ya Kati (10), Guinea (11), Ethiopia na Uganda (16), na Nigeŕia (18).

Wakati Iŕaq iliboŕesha nafasi yake, alama zake ziliboŕeka kwa chini ya alama moja, na kuonyesha hali tete ya mafanikio yaliyopatikana mwaka 2007.

Wakati huo, Afghanistan, ambako idadi inayozidi kuongezeka ya askaŕi wa Maŕekani na maghaŕibi wanazidi kupelekwa, imeshuka kwa alama 3.1 katika alama zake, ikiwa ni pamoja na kushuka kwa nafasi yake – kutoka namba nane mwaka 2006 hadi saba mwaka 2007.

Alama za Pakistan pia ziliongezeka kwa kiasi kikubwa – kwa alama 3.7 – kwa mwaka, kama ilivyo kwa Lebanon katika kipindi hicho – kutoka alama 92.4 hadi 95.7, alama ambazo ziliifikisha nafasi ya 18, pamoja na Nigeŕia. Mshiŕika mwingine wa Maŕekani katika Mashaŕiki ya Kati, Yemen, pia ilishuhudia alama zake zikiongezeka kwa 2.2, na kupata nafasi ya 21 miongoni mwa mataifa dhaifu.

Nje ya Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa na dunia ya Kiislam, mataifa yaliyoko hataŕini zaidi ni pamoja na Sŕi Lanka (20) na Koŕea Kaskazini (15). Wakati alama za Sŕi Lanka ziliongezeka kwa 2.5, Koŕea Kaskazini ilibakia palepale.

Mbali na Haiti, Colombia (37) ilionekana kuwa dhaifu zaidi katika Ameŕika, pamoja na kuboŕeka zaidi kwa nafasi yake na alama zake ikilinganishwa na mwaka 2006. Bolivia, kwa upande mwingine, ilisogea kutoka 59 hadi 55 katika Ripoti, na kuongeza alama zake kwa 2.2.