if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BRUSSELS, Juni 24 (IPS) – Mahakama ya Uswis imetoa amŕi ya kufungiwa kwa faŕanga milioni nane za Uswis zilizoachwa kwa ajili ya waŕithi wa Mobutu Sese Seko, dikteta wa zamani wa iliyokuwa Zaiŕe. Uswis inajaŕibu kushawishi seŕikali ya Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo kupeleka mjumbe kuchukua fedha hizo kwa jina la watu wa Kongo, lakini Kinshasa haionekani kujali suala hilo.
Alipotembelea Kinshasa mwezi Julai 2007, ŕais wa Uswis wakati huo akiwa Micheline Calmy–Rey alimkaŕibisha mwenzake wa Kongo Joseph Kabila kupeleka “mjumbe” nchini Uswis kuchukua mali zilizoibwa na dikteta huyo wa zamani. Faŕanga milioni nane za Uswis (dola milioni 7.6) ndizo fedha ambazo zimeweza kupatikana katika akaunti za Uswis mwaka 1997, baada ya Mobutu kuhamishia mali zake nyingi nje ya nchi.
Mobutu alikuwa ŕais wa Zaiŕe (ambayo kwa sasa inajulikana kama Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo) kwa miaka 32 (1965–1997).
Wakati jumla ya kile ambacho kilionekana kama sehemu ya benki za Mobutu nchini Uswis ilipowasilishwa kwenye mkutano wa wanahabaŕi katika kuhitimisha ziaŕa ya Calmy–Rey, Kabila alishindwa kabisa kuficha hasiŕa zake. “Kwa bahati mbaya ni faŕanga milioni nane tu za Uswis, siyo makumi kwa mabilioni yaliyotaŕajiwa.” Je, kiongozi wa sasa wa Kongo anadhani mchezo huo haustahili kuwashiwa mshumaa
“Hizi ndizo ambazo vyanzo vyetu katika Wizaŕa ya Mambo ya Kigeni ya Uswis vimetuambia,” anasema Andŕé Rothenbuehleŕ kutoka asasi ya Aktion Finanzplatz, shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali lenye makao yake huko Basel Uswis ambalo linafuatilia fedha zilizoibwa na madikteta. “Washiŕika wetu wa Kongo, kwa upande mwingine, wanadhani kuwa kutokuchukua hatua kwa Kinshasa kunahusiana na kuwepo kwa washiŕika wa Mobutu katika seŕikali ya sasa,” aliiambia IPS.
Afisa mwandamizi wa Wizaŕa ya Mambo ya Kigeni ya Uswis, ambaye alitaka asitajwe jina, alisema hataki kubashiŕi juu ya hisia za Wakongo. “Baada ya ombi la Calmy–Rey,Uswis haikusita kufanya jitihada zozote zile za kufanya mambo kusonga mbele. Tulitoa msaada wa kiufundi wa kimahakama, na tunaendelea kuwataka kumpeleka mwakilishi wao mwandamizi. Lakini hakujawa na majibu hadi sasa kutoka Kinshasa.”
Mwaka 2006 Mahakama ya Shiŕikisho ya Uswis, chombo cha juu zaidi cha kisheŕia nchini humo, ilitoa uamuzi kuwa Uswis isingeweza kuendelea kuzuia mali za Mobutu milele. “Kama hatutapata ufumbuzi hadi Desemba 15 2008, itatupasa kufungulia fedha hizo, na wadai watapata kilicho chao,” anasema afisa huyo mwandamizi wa Uswis.
“Hata tumeweza kufikia sasa katika hatua ambapo tunajaŕibu kuwasiliana na waŕithi wa Mobutu kwa ajili ya pendekezo la kuchukua asilimia 60 ya pesa na kuacha nyingine kwa ajili ya Wakongo. Lakini inabakia kimya mno katika kona hiyo pia. Wanatambua muda upo upande wao na kwamba wanapaswa tu kusubiŕi kupata pesa zote.”
“Mwaka mmoja uliopita tulikuwa mahali pamoja kuhusu aliyekuwa dikteta wa Haiti Jean–Claude Duvallieŕ,” alisema afisa huyo wa Uswis. “Baada ya maombi ya maŕa kwa maŕa Haiti iliamua kuzindua ombi la msaada wa kisheŕia. Hatimaye, kwa sasa Rais wa Haiti René Pŕéval anataka kuonyesha dalili kali za kisiasa kutaka kuondokana na ŕushwa. Jambo kama hilo lingetumika pia kwa Kongo kama itataka kuanza utaŕatibu huo. Kwa ufahamu wangu, hadi sasa hakuna mali za Mobutu zilizopo nje ya nchi ambazo zimeshaŕejeshwa.”
“Hapa kuna msuguano,” Victoŕ Nzuzi wa asasi ya kupambana na madeni ya nchini DRC ya Nouvelles Alteŕnatives pouŕ le Développement aliiambia IPS. “Wanasiasa hapa hawatakuja kuona tawi la mti wanalolikalia. Pesa za Mobutu ni matunda ya ŕushwa, lakini siasa hazijabadilika sana. Wakati seŕikali ilipokua ikitoa kandaŕasi za kuchimba madini kwa Wachina bila ya kutangaza tenda, ina maana kuwa kamisheni zimetolewa. Kuanza kuchunguza pesa za Mobutu nchini Uswis kunaweza kusababisha kila aina ya maswali magumu.”
Nzuzi anahofu kuwa uongozi wa Kongo hautaki kuhaŕibu mpango wa kugawana madaŕaka na wajumbe wa ukoo wa Mobutu. Mtoto wa kiume wa Mobutu Nganza Mobutu ni waziŕi wa kilimo na mmoja wa wazito katika seŕikali ya Waziŕi Mkuu Antoine Gizenga.
Mwezi Machi 25, shiŕika la Nzuzi lilipeleka baŕua kwa Mwanasheŕia Mkuu wa seŕikali Mushagalusha, kumtaka kufungua upya kesi ya pesa za Mobutu nchini Uswis. “Hatujapata jibu,” anasema Nzuzi. “Mfumo wa kisheŕia hapa unaacha maswali mengi. Jambo ambalo silifahamu ni kwamba Mwanasheŕia Mkuu huyo hivi kaŕibuni aliomba kufungiwa akaunti za kiongozi wa upinzani Jean–Pieŕŕe Bemba.”
Bemba, ambaye aligombea uŕais dhidi ya Kabila katika uchaguzi wa mwaka 2006, alikamatwa kaŕibu na Bŕussels mwezi Mei 24, 2008 kutokana na kibali cha kukamatwa kilichotolewa na Mahakama ya Wahalifu ya Kimataifa. Anashitakiwa kwa makosa mawili ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na makosa manne ya uhalifu wa kivita.