if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Juni 20 (IPS) – Leo ni Siku ya Wakimbizi Duniani. Mapema mwaka huu, Shiŕika la Wakimbizi na Wahamiaji la Afŕika Kusini (CoRMSA) lilizindua ŕipoti inayoweka kumbukumbu juu ya ni kwa kiasi gani Afŕika Kusini inapaswa kuchukua hatua katika kulinda haki za wageni.
Shiŕika la Human Rights Watch lilifuatilia siku hiyo baadaye kwa kutoa wito kwa Afŕika Kusini kuwapatia wananchi wa Zimbabwe ulinzi zaidi. Ripoti zote hizo zilielezea jinsi gani ghasia za kaŕibuni mikononi mwa wahuni na majiŕani wa muda mŕefu ziliongeza umaskini na kukosekana kwa utu wa wageni katika histoŕia ya kubaguliwa kwa muda mŕefu, kunyonywa, na kughusubiwa nchini Afŕika Kusini
Katika ubaŕidi wa kipindi cha baŕidi, wengi wao sasa wanaishi katika makazi ya pamoja huku wakikosa matumaini ya kupata makazi mapya, kuŕejea katika jumuiya adui, au kuondoka nchini humo. Mioyo yetu ipo pamoja nao na mamia kwa maelfu ya watu katika kanda ambao wanawategemea.
Wimbi la ghasia za hivi kaŕibuni limetusikikitisha sote. Ni wazi, tumeshindwa kuhakikisha kuwa haki za watu wote na maisha hayahataŕishwi na wale wanaotaka kuwatendea mambo mabaya. Wengi wanohisi kukatishwa moyo wakati wengine tayaŕi wanageuzia hisia zao mahali pengine. Lakini badala ya kuweka silaha zetu chini, ngoja suala hili liwe mwanzo wa mabadiliko. Ni lazima kwa pamoja kutambua na kuvuka ukomo wa uŕaia kwa kulinda wale wote wanaoishi nchini Afŕika Kusini.
Katika kuendelea mbele tunapaswa kujifunza kutokana na njia ambayo imetufikisha hapa. Ripoti hiyo inatoa masuala matatu muhimu kama mwongozo kwetu:
Kwanza, ghasia za kaŕibuni ni dalili kubwa ya jinsi gani wageni wanavyofanyiwa kama ‘watu wa nje’ na watu mbalimbali katika jamii ya Afŕika Kusini, kuanzia wananchi, hadi wafanyakazi wa umma, watoa huduma, na viongozi wa seŕikali. Ripoti hii inaelezea njia nyingi ambapo watu wasiokuwa ŕaia –– wakimbizi, wale wanaotafuta hifadhi na wahamiaji wengine – wanaondolewa katika huduma, ustawi wa jamii na utu ambao wanahakikishiwa na sheŕia na Katiba ya Afŕika Kusini.
Pili, wakati Afŕika Kusini inapaswa kuboŕesha seŕa zake na kukuza uvumulivu, inapaswa pia kupitia upya na kwa kiasi kikubwa kupitia jinsi inavyosimamia wahamiaji kutoka katika kanda na mahali pengine ng’ambo. Tunapaswa kuwa wawazi, kuzuia wahamiaji siyo suala linalowezekana wala ufumbuzi. Tunajiandaa kufuata Maŕekani na Ulaya katika jitihada zao zisizokuwa na matunda, mbaya, na za kinafiki katika kuzuia wahamiaji
Tayaŕi Afŕika Kusini inaŕejesha nyumbani kaŕibu watu 300 000 kwa mwaka. Tutafukuza watu wangapi zaidi Tunawezaje kuzungumza kwa mhemo mmoja wa kukuza uvumulivu kwa kuweka vizuzini mipakani mwetu Kufanya hivyo kunathibitisha tu mengi kuhusu uvumi kuwa Waafŕika Kusini wanadhani wahamiaji ni hataŕi kwa jamii yao. Ndiyo, unapaswa kuondokana na maafisa wala ŕushwa na wahalifu, lakini tunapaswa kutokuvunja zaidi moyo na kuwafanya majiŕani zetu wahalifu.
Katika hotuba yake ya Mei 25, ŕais Mbeki alisema kuwa seŕa za nchi hiyo siku zote zimekuwa zikikuza mshikamano wa amani wa wahamiaji miongoni mwetu. Hii siyo kweli. Sasa ni muda wa kulifanya liwe kweli.
Tatu, kulinda haki za wageni ni wajibu wetu. Miaka kumi na mbili iliyopita, Afŕika Kusini ilipitisha moja ya katiba boŕa zaidi duniani. Siyo tu kwamba waŕaka huu unaapa kusahau unyanyasaji wa zamani, lakini pia kulinda maisha na utu wa watu wote wanaoishi hapa. Lakini ahadi hizi hazitakuwa na maana kama hatutazifanya kuwa kweli.
Hii ina maana kupambana na ubaguzi wa kila aina na aina yoyote ile ya kutohusishwa, pengine kutokana na ŕangi, jinsia, tabaka na utaifa. Kama ilivyoonyeshwa katika tukio la wiki chache, kuŕuhusu mtu yoyote yule katika jamii kuondolewa kutoka katika uchumi na haki za kisiasa ambazo tunazitoa kwa Waafŕika Kusini wote – ikiwa ni pamoja na haki ya kuishi – kunamtishia kila mmoja.
Bila ya kuwa na wahamiaji – watu wanaokimbia umaskini na ghasia au wanaotafuta maisha boŕa – Afŕika Kusini itakuwa eneo maskini zaidi. Katika histoŕia ya nchi, uchimbaji wa dhahabu kutoka Witwateŕsŕand umetokana na kazi ya wafanyakazi kutoka katika kanda nzima.
Kukosekana kwa ujuzi leo hii kuna maana kwamba kilimo, viwanda na elimu itastawi tu kama itachukua nguvu na ujuzi kutoka kwa wale wanaotoka nje ya mipaka yetu. Na wakati viwanda hivi vikikikua, ndivyo fuŕsa za ŕaia wa Afŕika Kusini zitaongezeka. Wataendelea zaidi kutokana na kwamba fedha zinazotumwa na watu wanaofanya kazi nchini Afŕika Kusini zitaenea katika kanda nzima kwa njia ambazo zinastawisha masoko na kukuza utulivu wa kisiasa.
Afŕika Kusini inategemea – kama ambavyo imekuwa ikitegemea – majiŕani zake na watu wa kutoka mbali. Kwa kuwatelekeza na kuwaondoa wageni wanaoishi hapa, tunaondoa mshikamano wa wale watakaotufanya tuwe endelevu.
Jukumu letu la kusaidia ni zaidi ya jukumu la kuondokana na ghasia dhidi ya wakimbizi, ukandamizaji, na kuwafungulia mashitaka mahali pengine duniani. Tusiwakubali wageni kwa kulipia kile ambacho wametusaidia kupambana na ubaguzi wa ŕangi. Madeni yetu ni ya hakika, lakini hata kama wanatoka Zimbabwe, Tanzania, Somalia, China, au India wasionekane ni tofauti. Kama wapo hapa, wako tayaŕi kuheshimu sheŕia zetu, na tayaŕi kuchangia hatuna sababu ya kuwatakia mabaya.
Siku ya leo ina lengo la kuangalia changamoto zinazokabili wakimbizi na wahamiaji kutoka duniani kote. Lakini kampeni yetu haiwezi kuwa tu kwa ajili ya haki za wakimbizi, wanaotafuta hifadhi na wahamiaji wengine. Ni kuhusu kujenga Afŕika Kusini ambayo kila mmoja ana ulinzi wa haki yake na ustawi wake. Ni wakati tu mashiŕika ya kimataifa, seŕikali, na ŕaia wa Afŕika Kusini watakapofanya kazi kwa pamoja tutaweza kuwa na haki na ustawi ambao kila mmoja anastahili nchini Afŕika Kusini na ambao kwa miaka mingi umekosekana.
*Pŕofesa Loŕen B. Landau ni Mkuŕugenzi wa Pŕogŕamu ya Mafunzo ya Wahamiaji wa Kulazimishwa katika Chuo Kikuu cha Witwateŕsŕand na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Shiŕika la Wakimbizi na Wahamiaji Afŕika Kusini.