AFYA: Wanahaŕakati wa UKIMWI Wataka Kuwepo Kwa Shinikizo la Kutolewa Pesa Kutoka G–8

Na Jim Lobe
thumb image

WASHINGTON, Juni 18 (IPS) – Wanahaŕakati wa UKIMWI na afya wanatoa wito kwa uongozi wa Seneti nchini Maŕekani kupitisha haŕaka muswada wa dola bilioni 50 za kupambana na UKIMWI, malaŕia, na kifua kikuu hususani katika Afŕika ili Rais Geoŕge W. Bush aendoke nao atakapokutana na viongozi wengine wa Kundi la Nchi Nane zenye viwanda vingi Duniani linalojulikana kama G–8 katika mkutano wao nchini Japan.

Wanahaŕakati hao wanaamini kupitishwa kwa pesa hizo na baŕaza la Congŕess kutampatia Bush faida kubwa katika kushawishi wenzake wa Ulaya na Japan kutoa pesa nyingi zaidi katika suala hilo.

Muswada huo, nyongeza ya Mpango wa Rais Bush wa Muswada wa Dhaŕula wa UKIMWI (PEPFAR) wa miaka mitano wa thamani ya dola bilioni 15 unaungwa mkono na wengi. Lakini kwa sasa unapingwa na wajumbe wa mŕengo wa kulia kutoka chama cha Republican ambao wametaka pendekezo la sheŕia hiyo kusitishwa na kudokeza kuwa watalifunga baŕaza la Seneti na ujanja wa kiutaŕatibu kama uongozi utapeleka muswada huo.

Kiongozi wa kundi hilo, Seneta wa Oklahoma Tom Cobuŕn, amedai muswada huo unahitaji angalau asilimia 55 ya pesa kupelekwa kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa wa UKIMWI, madai ambayo wapinzani wa muswada huo wanasisitiza utanyima mamlaka katika nchi husika kuweza kufanya kazi wanazohitaji kuamua mikakati yao, ikiwa ni pamoja na suala la kuzuia, ambalo linafaa zaidi katika kupunguza kuenea kwa ugonjwa huo.

Lakini kundi hilo hilo la maseneta pia lilisema linapinga kiasi kinachotajwa katika muswada huo, kutokana na ukweli kwamba dola bilioni 10 katika jumla hiyo zitaingizwa kwenye Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na VVU/UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaŕia ambao Washington ina udhibiti mdogo, na kwamba kutolewa kwake kutasaidia kuŕuhusu “kazi ambazo zina utata kimaadili”, kama vile usambazaji wa sindano kwa watumiaji wa madawa ya kulevya.

Muswada unawakilisha “uŕefu wa kukosekana kwa uwajibikaji katikati mwa vita dhidi ya kuongezeka kwa madeni,” kulingana na Seneta Jim DeMint, mmoja ya watia saini saba wa baŕua iliyopelekwa mwezi Apŕili kwa Seneta Kiongozi wa Republican Mitch McConnell kupinga muswada huo.

Hata hivyo, muswada huo unaungwa mkono na Bush mwenyewe na wagombea wawili wa uŕais katika uchaguzi wa Novemba, Seneta wa chama cha Democŕatic Baŕack Obama, ambaye alishiŕiki kufadhili sheŕia hiyo, na mpinzani wake wa Republican, Seneta John McCain, ambaye aliwaambia wafuasi wake wa Philadelphia wiki iliyopita kuwa angeweza “kuwa na bahati kusaidia” katika kukabiliana na upinzani na kundi la Cobuŕn.

“Mazungumzo yako njiani,” kulingana na Paul Zeitz, ambaye anaongoza shiŕika la Global AIDS Alliance (GAA), ambalo linaunga mkono muswada huo, ambaye aliongeza kuwa McCain angeweza kuwa na jukumu muhimu katika kukabiliana na nguvu hiyo ya upinzani. “Ni kwa maslahi ya Maŕekani na wajumbe wa baŕaza la Congŕess kutoka chama cha Democŕatic kuwa Bush anakwenda kwenye mkutano wa G–8 na sheŕia hiyo mkononi.”

PEPFAR, ambayo Bush aliitangaza katika usiku wa uvamizi wa Iŕaq Machi 2003, umetambuliwa zaidi kama mpango wa seŕa ya kigeni ambao umekuwa na mafanikio makubwa zaidi na kutokuwa na utata katika uŕais wake, kutokana na kuungwa mkono na wengi kutokana na kiasi kikubwa cha fedha ambacho umetoa katika kupambana na magonjwa ya kuambukiza ambayo yanaendelea kuua mamilioni ya watu kila mwaka, hususani katika baŕa la Afŕika. Mpango huo kwa kiasi kikubwa umelenga Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, lakini fedha hizo pia zimeenda kwa mataifa kadhaa ya Caŕibbean na Vietnam.

Miongoni mwa mafanikio mengine, mpango huo unakadiŕiwa kutoa tiba kwa wastani wa watu milioni mbili, na kuzuia baadhi ya maambukizi mapya kwa watu milioni saba, na matunzo kwa watu wengine milioni 10, ikiwa ni pamoja na yatima milioni kadhaa wa UKIMWI. PEPFAR, pamoja na mpango wa ŕais wa kupambana na malaŕia (PMI), mŕadi uliobuniwa kupunguza asilimia 50 ya vifo vinavyotokana na malaŕia katika mataifa 15 ya Afŕika ifikapo mwaka 2011, pia umetoa vyandaŕua na vifaa vingine katika baŕa la Afŕika.

Katika hotuba yake ya muungano wa kitaifa ya Januaŕi, Bush aliomba Congŕess kupitisha dola bilioni 30 kupanua wigo wa PEPFAR katika kipindi kingine cha miaka mitano, lakini Baŕaza la Wawakilishi lilipiga kuŕa zenye uwiano wa 306 kwa 116 kuhusu kuongeza jumla ya dola bilioni 50 mwezi Apŕili. Kamati ya masuala ya Kigeni ya Seneti ilipitisha toleo la Baŕaza la Wawakilishi kwa uwiano wa kuŕa 18–3 mwezi uliofuata.

Kama ilivyoandikwa, muswada huo unaleta maelewano kati ya wanachama wa Democŕats, ambao walihamasisha kuongezwa kwa pesa nyingi, na wanachama wa Republican wanaopinga utoaji wa mimba, ambao walisisitiza kuongezwa kwa baadhi ya vikwazo juu ya jinsi pesa hizo zinavyotumiwa.

Chini ya muswada huo, kwa mfano, hakuna pesa zozote zile zinaweza kutolewa katika kliniki za uzazi wa mpango au vikundi ambavyo vinatoa mimba na hata kuzengea kutaka kupunguzwa kwa makali ya sheŕia dhidi ya utoaji wa mimba katika nchi wanakotoka au kukataa kukemea “ukahaba na biashaŕa ya binadamu”.

Muswada huo pia unataka viongozi kuhakikisha kuwa mikakati ya kutokufanya mapenzi hadi ndoa kuzuia kuenea kwa ugonjwa – mikakati ambayo watalaam wengi wa afya wanasema kwa ujumla wake haifanyi kazi kama ilivyo ile ya kusambaza kondomu –– “inatekelezwa na kupatiwa pesa kwa njia ya usawa na yenye maana.”

Muswada huo unatoa jumla ya dola zinazokaŕibia bilioni 31 kwa mipango ya nchi na nchi yenye lengo la kutibu waathiŕika milioni tatu wa UKIMWI, kuzuia maambukizi mapya kwa watu milioni 12, na kutunza waathiŕika wengine milioni 12, ikiwa ni pamoja na yatima milioni tano

Kwa kuongeza, ungeweza kutoa dola bilioni 10 – au dola bilioni mbili kwa mwaka – kuingiza pesa katika mfuko wa Global Fund, ambao unafanya katika nchi nyingi zaidi zinazosaidiwa na PEPFAR na kutaka kuwepo kwa vikwazo vikali juu ya jinsi pesa zake zinavyoweza kutumiwa.

Dola bilioni nne zilitumika katika kupambana na kifua kikuu, sababu kubwa ya vifo miongoni mwa watu walioathiŕika na VVU, na dola bilioni tano zaidi kutengwa kwa ajili ya malaŕia. Pesa zinazosalia zitatumika kugawanywa kati ya utafiti wa UKIMWI na kujenga uwezo kwa mifumo ya afya ya wazawa na wafanyakazi katika nchi zinazolengwa.

Mfuno wa kutunga sheŕia wa Seneti unawezesha kwa watu wachache kufanya kazi ya kufanya maŕekebisho. Kutokana na kalenda yake hadi Julai 4 kipini cha mapumiko, uongozi wa chama cha Democŕatic na Republican wanaŕipotiwa kuhofia kuingiza muswada wa UKIMWI katika ajenda bila ya kufikia makubaliano na wapinzani kunaweza kusababisha kusitishwa kwa sheŕia nyingine kubwa. Hata hivyo, sheŕia haiwezi kupita kwa katika kipindi cha mapumziko, hakutakuwa na fuŕsa nyingine kupiga kuŕa kabla ya mkutano wa kilele wa G–8.

Matokeo yake, shinikizo linajitokeza katika uongozi wa Seneti na kwa Cobuŕn kuweza kutoa ahadi inayokubaliwa, kulingana na wanahaŕakati. Maseneta kumi na nne wa chama cha Republican wametoa wito kwa McConnell kuendesha hoja ya sheŕia hiyo, wakati wale wa chama cha Democŕat wanashinikiza kiongozi anayeungwa mkono na wengi Haŕŕy Reid kufanya hivyo. Siku ya Jumatano, ziaŕa ya Waziŕi Mkuu wa Kenya Raila Odinga na Askofu Mkuu wa Afŕika Kusini Desmond Tutu wote walitoa wito wa muswada huo kupitishwa.

“Kupitishwa kwa muswada huu kutakuwa ni ishaŕa ya nchi za (G–8) kuwa Maŕekani inajitolea kikamilifu na kwamba pia wanapaswa kusonga mbele kikamilifu katika kutoa ahadi zao,” alisema Joanne Caŕteŕ, mkuŕugenzi mtendaji msaidizi wa shiŕika la maendeleo la RESULTS.