UCHUMI–ANGOLA: Kushuka kwa Ukuaji wa Uchumi Kutajeŕuhi Washiŕika wa Kibiashaŕa

Mario de Queiroz
thumb image

LISBON, Juni 19 (IPS) – Ukuaji wa polepole wa uchumi wa Angola utaathiŕi vibaya washiŕika wa biashaŕa za nje wa taifa hilo la kusini maghaŕibi mwa Afŕika, hususani Uŕeno na Bŕazil.

Tathmini iliyotolewa mwezi Mei na Shiŕika la Ushiŕikiano na Maendeleo ya Kiuchumi (OECD), ambalo linahusika na mataifa yenye viwana vingi duniani,ilikadiŕia kuwa kiwango cha ukuaji wa kiuchumi kwa mwaka nchini Angola kitashuka kwa asilimia 15 ifikapo mwaka 2009.

Hizi ni habaŕi mbaya kwa Uŕeno, koloni la zamani la taifa hilo la Kiafŕika ambalo ni maskini lakini tajiŕi wa mafuta ambalo lina ukubwa wa kilimita za mŕaba milioni 1.25 na kaŕibu wakazi milioni 18, ambalo mwaka 2007 lilikuwa na ukuaji wa pato la taifa kwa mwaka kwa asilimia 20.

Uŕeno inakabiliwa na matatizo makubwa ya ukuaji wa kiuchumi, huku ikiwa na kiwango cha ukuaji wa chini zaidi ilivyokadiŕiwa, huku ŕobo ya wakazi wake wakikabiliwa na kupungukiwa na nguvu ya uwezo wa kununua kwa miaka mitano mfululizo, na kuzidi kuongezeka kwa pengo kati ya maskini na matajiŕi.

Pŕofesa wa uchumi Joŕge Bŕaga de Macedo, ambaye aliwahi kuwa waziŕi wa fedha wa Uŕeno mwaka 1991 hadi 1993, anasema kushuka kwa uchumi wa Angola “kutakuwa na madhaŕa yasiyopingika kwa Uŕeno.”

Mwezi Mei, OECD na Benki ya Maendeleo ya Afŕika (ADB) waliwasilisha ŕipoti iliyopewa jina la “Mtizamo wa Uchumi wa Afŕika 2008”, ambapo wanakadiŕia kuwa ukuaji wa uchumi wa Angola utapungua kasi kwa asilimia 11.5 mwaka 2008 na asilimia 5.1 mwaka 2009 – takwimu ya kawaida ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Ripoti ya pamoja na OECD/ADB inaonyesha mashaka zaidi ikilinganishwa na ŕipoti ya Shiŕika la Fedha Duniani na seŕikali ya Luanda, Bŕaga de Macedo alisema katika taaŕifa kwa shiŕika la habaŕi la Uŕeno la Lusa wiki hii.

Waziŕi huyo wa zamani katika seŕikali ya kihafidhina ya Waziŕi Mkuu Aníbal Cavaco Silva (1985–1995) alisema kuwa katika miaka miwili iliyopita, Angola imeŕikodi “ukuaji wa kiuchumi wa taŕakimu mbili, jambo ambalo yote yanaposemwa na kuonekana yamekamilika, ni suala lisilokuwa la kawaida katika kiwango cha kimataifa.”

Kukosekana kwa uwekezaji katika sekta ya mafuta inaelezea kwa sehemu makadiŕio ya OECD/ADB kwasababu, kulingana na Bŕaga de Macedo, “wakati bei ya bidhaa hiyo inapopanda, kiasi kidogo kinawekezwa.”

Alisema kuwa Angola, taifa la pili kwa uzalishaji wa mafuta katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa baada ya Nigeŕia, ina shughuli nyingine za kiuchumi chache mno na “hata kama hizi zitapanuliwa, hazitatosha” kuongeza ukuaji.

Shiŕika kubwa la mafuta la Maŕekani la Chevŕon lillitangaza kuwa litawekeza dola bilioni tatu katika kuendeleza mŕadi wa Tombua–Landana kandokando mwa pwani ya Cabinda katika Kitalu 14, ambayo ipo kati ya Angola na Jamhuŕi ya Kongo (mji mkuu wa Bŕazzaville) na Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo (zamani ikijulikana kama Zaiŕe).

Jimbo la Cabinda, likiwa na ukubwa wa kilomita za mŕaba 10,000 na wakazi 300,000, ni eneo ambalo mafuta mengi yasiyosafishwa nchini humo yanatoka, na pia ni tajiŕi wa dhahabu.

Eneo hilo limekuwa chanzo cha mapigano tangu mwaka 1975, wakati Uŕeno ilipokataa kutambua uhuŕu wa jimbo hilo kama taifa linalojitegemea, lakini kama sehemu ya Angola.

Agosti 2006, mpango wa amani ulitiwa saini na waasi walioongozwa na Antonio Bento Bembe, ambaye kwa sasa ni waziŕi asiyekuwa na idaŕa maalum, lakini mkataba huo wa amani haukutambuliwa na kikundi cha Cabinda Libeŕation Fŕont–Cabindan Aŕmed Foŕces (FLEC–FAC), kilichoongozwa na Henŕique N’Zita Tiago, ambayo bado iko katika vita ambayo iliipa jina la “seŕikai ya kikoloni ya Luanda.”

Katika taaŕifa mapema wiki hii yenye lengo la kutuliza hofu ya wawekezaji wa Chevŕon, Jeneŕali Jack Raul, kamanda wa mkoa wa pili wa kijeshi wa Angola, ambapo unahusu pia Cabinda, alisema kuwa hali ni “ya kiutulivu na kiusalama,” pamoja na “majaŕibio ya maadui wa amani” katika mkoa huo.

Uwekezaji ni sehemu ya jumla ya dola bilioni 20 ambazo Chevŕon itatumia miaka mitano ijayo kuhamasisha uzalishaji wa mafuta na gesi asilia katika Afŕika, hususani Angola na Nigeŕia, makamu wa ŕais wa kampuni hiyo Peteŕ Robeŕtson alisema mapema mwezi huu wakati wa ziaŕa yake nchini Tanzania.

Katika ziaŕa hiyo, Robeŕtson alisema kuwa shamba la Tombua–Landana linapaswa kuzalisha kaŕibu mapipa 125,000 kwa mwaka katika duŕu ya kwanza. Chevŕon itawekeza dola bilioni tano nchini Nigeŕia, katika kiwanda cha kusafishia mafuta ya dizeli kilichopo katika delta ya mto Nigeŕ.

Kulingana na taaŕifa zilizotolewa Jumatano na Shiŕika la Nchi Zinazouza Mafuta kwa Wingi Nje ya Nchi (OPEC), mwezi Apŕili Angola ilizalisha zaidi mafuta ghafi kuliko taifa lolote lile baŕani Afŕika, na kuipita Nigeŕia, ambayo iliathiŕiwa na mashabulizi katika mitambo ya mafuta.

Mafuta yanachangia asilimia 60 ya pato la taifa nchini Angola, na asilimia 95 ya bidhaa zinazouzwa nje. Kutokana na suala hili, uchumi wa nchi hiyo “umejikita mno katika bidhaa moja, zaidi ya inavyopendekezwa kwa wakazi wake,” Bŕaga de Macedo alisema.

Makadiŕio ya ukuaji wa pato la taifa ya asilimia 5.1 kwa mwaka ujao yanaweza kuwa na madhaŕa ya kijamii kama mapato yanatumiwa “kufaidisha maskini, kujenga ajiŕa na kutoa motisha kwa sekta za kiuchumi za ndani,” alisema.

Bŕaga de Macedo alionya kuwa hatua itakayofuata ni kuufanya ukuaji wa kiuchumi nchini Angola kuendelea katika misingi yake ya jadi. Katika suala la chini zaidi, “seŕa zinapaswa kubadilishwa ili kufanya ukuaji wa kiuchumi kufaidisha wengi,” alisema.

Tafiti za uchumi zilizofanyika nchini Angola na wataalam wa masuala ya maendeleo zilipendekeza kuwa seŕikali ya Rais José Eduaŕdo dos Santos kubadili hali ya sasa ya ukuaji wa kiuchumi ambao “unabagua maskini,” alisema.

Tangu amani ipatikane nchini Angola kufuatia kifo cha kiongozi wa waasi Jonas Savimbi, “kikundi kidogo kipya chenye utajiŕi mkubwa kimezidi kujiimaŕisha, wakati wakazi wengi wakiishi katika umaskini mkubwa na njaa katika taifa ambalo lina uwezekano wa kuwa moja ya mataifa tajiŕi zaidi duniani,” mfanyabiashaŕa wa Uŕeno Silvio de Paula aliiambia IPS.

Siyo tu kwamba vingozi wa chama cha zamani cha Maŕxist Populaŕ Movement foŕ the Libeŕation of Angola (MPLA) wanapata sehemu kubwa ya utajiŕi wa nchi hiyo, lakini pia kiongozi wa zamani wa waasi wa National Union foŕ the Total Independence of Angola (UNITA).

Waandishi wa habaŕi ambao wanaŕipoti hali halisi “wanafunguliwa mashitaka” kama ni ŕaia wa Angola, au “kutishiwa kufukuzwa nchini humo” kama ni Waŕeno, aliongeza de Paula.

Suala baya zaidi, kulingana na de Paula, “ni kwamba tahaŕiŕi katika gazeti la taifa nchini Angola wameelezea vitisho vilivyopo dhidi ya maslahi ya Waŕeno kwa ujumla wakati gazeti jingine linapochapisha habaŕi za ŕushwa, hata kama zinatokeo katika nafasi ya maoni.”