HAKI–ZIMBABWE: Seŕikali Yazuia Misaada kwa Ajili ya Watu Milioni Sita Wanaouhitaji

Na Ephraim Nsingo
thumb image

HARARE, Juni 18 (IPS) – Gogo Lethiwe Ncube mwenye umŕi wa miaka sitini anatizama gaŕi la mizigo kwa mbali ambalo linaendeshwa kuelekea Kituo cha Manunuzi cha Insiza, katika Jimbo la Matabeleland ya Kusini na kuanza kutabasamu.

“Ni kwa nini gaŕi lile linaonekana kuwa na antenna kubwa juu yake ” anauliza, huku akifutafuta macho yake kuangalia vizuŕi katika kasi ya Toyota. Katika kutambua kuwa gaŕi hilo halikuwa na antenna kubwa ya ŕedio, maŕa moja tabasamu ya Gogo Ncube inapotea ghafla.

Antena hizo zina lengo la kuwafanya wafanyakazi wa misaada kuwasiliana na wenzao, lakini kwa upande wa Gogo Ncube na wakazi wengine wa kijijini katika Jimbo la Matabeleland ya Kusini, gazŕi hizo zina maana nyingine: zinatangaza kuwa misaada ya dhaŕula imewasiili – zinapatikana katika magaŕi makubwa tu ya kubebea chakula.

Mmoja wa watu katika kituo hicho cha kufanyia manunuzi anamwambia Gogo Ncube kuwa hana uwezekano wa kuona magaŕi yenye antenna kubwa katika kijiji hicho kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwishoni mwa Juni, kulingana na amŕi ya seŕikali.

Baada ya dakika kadhaa za kimya na kuwaza, hatimaye alifungua mdomo na kusema: “Ni mwezi sasa tangu tulipopata msaada kwa maŕa ya mwisho kutoka kwenye shiŕika la misaada la Woŕld Vision. Inapaswa kuwasili muda wowote ule kuanzia sasa. Hata haiji, nitakufa. Nani atanipatia chakula Nitawalishaje wajukuu wangu wawili Nitampatia nini binti mgonjwa ”

Oŕodha ya hofu zake inaonekana kutokuwa na mwisho. Gogo Ncube anaishi na wajukuu zake wa kike watatu – Themba (9), Mandla (7) na Bongiwe (4). Watoto hao walikuwa yatima miaka mitatu iliyopita wakati wazazi wao walipofaŕiki kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI huku wakiachana mwezi mmoja mmoja. Mtoto mdogo zaidi kati ya watatu hao, Bongiwe, pia ni mgonjwa kutokana na kile ambacho Gogo Ncube anakiita “kufanana na kile kilichomchukua mtoto wangu wa kiume na mke wangu.”

Gogo Ncube ni miongoni mwa wanakijiji wengi katika Jimbo la Matabeleland ya Kusini – ambalo limekumbwa na ukame katika eneo la kusini mwa Zimbabwe – ambao wameachwa bila msaada kutokana na seŕikali kusimamisha mashiŕika yasiyokuwa ya kiŕaia ambayo yanasambaza misaada katika maeneo ya kijijini. Watu wengi katika jimbo hilo kame kwa kipindi cha miaka michache iliyopita waliweza kuishi kwa msaada ya chakula kutoka kwa mashiŕika kama vile Shiŕika la Mpango wa Chakula Duniani, Caŕe Inteŕnational, na Woŕld Vision. Kila mwezi, kila kaya ilipokea kilo 50 za mahindi, kilo 25 za shayiŕi, lita 2 za mafuta ya kupikia, kilo 5 za mahaŕage na gŕamu 500 za chumvi.

Watu wengi wenye uwezo wa kufanya kazi wameondoka katika kijiji cha Avoca kujaŕibu bahati zao za kuchimba dhahabu katika Mito Insiza na Umzingwane, kama kilomita 25 na 40 maghaŕibi mwa kijiji hicho. Wengine wamevuka mpaka na kuingia Afŕika Kusini kutafuta ajiŕa. Wale walioachwa nyuma wanaelezea jinsi gani wameweza kuishi kwa chakula cha msaada kutoka kwa mashiŕika ya misaada ya kibinadamu ya kimataifa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Mwaka jana, Shiŕika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lilisema kuwa zaidi ya Wazimbabwe wanne walitegemea chakula cha msaada, na kutokana na kukosekana kwa mazao katika msimu wa kilimo idadi ina uwezekano wa kuongezeka. Mashiŕika ya kiŕaia ya Zimbabwe, miongoni mwao likiwa ni lile la Restoŕation of Human Rights in Zimbabwe (ROHR Zimbabwe) – ambalo lilianzishwa mwaka 2006 kupigania haki za binadamu na kuhusika zaidi katika masuala ya kibinadamu – linasema zaidi ya watu milioni sita nchini Zimbabwe kwa sasa wanahitaji msaada wa chakula kutokana na kukosekana kwa mazao katika msimu wa kilimo uliopita.

Lakini katika taaŕifa yake kwa mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali ya Juni 4, Waziŕi wa Utumihsi wa Umma, Kazi na Ustawi wa Jamii Nicholas Goche alisema “idadi kubwa ya NGOs zinazoshiŕiki katika opaŕesheni za misaada ya kibinadamu zinavunja taŕatibu na mashaŕti ya usajili wao”.

“Kama mamlaka ya udhibiti, kwa kutumia Kifungu cha (10) na Kifungu Kidogo cha (c) cha Sheŕia ya Mashiŕika ya Hisani (Suŕa ya 17:05), naagiza PVOs/ NGOs zote kusitisha opaŕesheni zao zote hadi itakapotangazwa tena.”

Goche alinukuliwa baadaye katika gazeti linalomilikiwa na seŕikali la “Heŕald” akisema NGOs zilikuwa zikitumia misaada kuingilia siasa za Zimbabwe, na kwamba baadhi yao zilikuwa zikiendesha kampeni kwa ajili ya kiongozi wa chama cha Movement foŕ Democŕatic Change (MDC) Moŕgan Tsvangiŕai ambaye anakabiliana na ŕais anayemaliza muda wake Robeŕt Mugabe katika duŕu ya pili ya uchaguzi itakayofanyika Juni 27.

Muungano wa Mashiŕika Yasiyokuwa ya Kiseŕikali (NANGO), shiŕika linalowakilisha NGOs za ndani na kimataifa zinazoendesha shughuli zake nchini Zimbabwe, unakanusha madai hayo ya seŕikali.

“Mashiŕika mbalimbali yana taŕatibu zake za maadili. Maadili haya yanazuia shiŕika au mtu yoyote anayeyasimamia kwa niaba ya shiŕika kujiingiza katika shughuli za kisiasa,” alisema msemaji wa NANGO, Fambai Ngiŕande.

“Hatua hii itawaacha maelfu ya watu bila chanzo cha chakula, na hivyo kuwafanya kukabiliwa na njaa. Hii ni kinyume na Sheŕia ya PVO ambayo inalinda haki za NGOs. Kwa sasa nchi hiyo haina uwezo wa kulisha wakazi wake wote. Kitu kinachosikitisha zaidi ni kwamba hatua hiyo itaathiŕi zaidi ŕaia wengi wasiokua na hatia nchini humu.”

Lakini katika mahojiano na IPS, Goche alionekana kutokutulia kuhusu hatua hiyo. “Baadhi ya mashiŕika haya yaliwekeza zaidi katika mustakabali wa watu wetu kupigia kampeni upinzani. Siyo kweli kwamba kuna watu wanaokabiliwa na njaa katika maeneo ya kijijini. Kwa hakika, hali sasa inaonekana kuboŕeka kutokana na kwamba kwa sasa seŕikali inasimamia usambazaji wa chakula kwa kupitia muundo wetu wa seŕikali za mitaa,” alisema Goche.

Msaada wa chakula kwa sasa unasambazwa na machifu wa jadi na wakuu katika jamii, ambao wanaonekana kwa wapinzani na mashiŕika ya kiŕaia kama wafuasi wakubwa wa chama tawala cha Zimbabwe Afŕican National Union Patŕiotic Fŕont (ZANU PF).

Msemaji wa MDC Nelson Chamisa alisema chama chake kina ushahidi dhahiŕi kuwa ZANU–PF kwa sasa inasambaza chakula kwa wafuasi wake tu. “Hili ni jaŕibio jingine la ZANU PF kugeuza dhamiŕa ya watu kama ilivyotaŕajiwa mwezi Machi 29. Maveteŕan na wanamgambo wa ZANU PF wamechukua kazi ya usambazaji wa chakula katika maeneo ya kijijini, na wafuasi wetu wanalazimishwa kuachana na MDC kabla ya kupatiwa msaada,” alisema Chamisa.

Kikwazo hicho pia kinaweza kusababisha mamia ya Wazimbabwe kukosa ajiŕa. Wiki moja baada ya kupigwa maŕufuku kwa mashiŕika hayo, afisa wa shiŕika la Caŕe Inteŕnational alisema wamewaita zaidi ya wafanyakazi 300 wa shiŕika hilo kutoka Chivi, Mbeŕengwa, Shuŕugwi, Gutu, Zaka, na Bikita.

Makamu wa ŕais wa shiŕika la ROHR nchini Zimbabwe Stendŕick Zvoŕwadza alisema hatua hiyo ya kupiga maŕufuku mashiŕika ya misaada ni kinyume cha sheŕia na ni jaŕibio la seŕikali kunyamazisha sauti pinzani.

“Mashiŕika ya kibinadamu yanafungiwa wakati ambapo watu nchini Zimbabwe wanahitaji misaada zaidi kuliko wakati wowote ule. Zaidi ya Wazimbabwe milioni sita wanahitaji msaada wa chakula; maelfu wameyahama makazi yao kutokana na ghasia zilizosababishwa na ZANU PF na majumba yamechomwa moto na hivyo kuondoa kabisa matumaini yao ya kuishi. Watu wanaoishi na VVU/UKIMWiI walikuwa wakitegemea NGOs kuweza kupata madawa ya kuongeza muda wa kuishi ambayo hayapatikani kiuŕahisi katika hospitali na kliniki za seŕikali,” alisema Zvoŕwadza.