ULAYA: Vikwazo Dhidi ya Sudan Vyatakiwa

David Cronin
thumb image

BRUSSELS, Juni 13 (IPS) – Umoja wa Ulaya umeombwa kuanzisha vikwazo nchini Sudan kutokana na kukataa kwake kukamata watu wawili wanaoshutumiwa kwa kufanya uhalifu dhidi ya ubinadamu katika jimbo la maghaŕibi mwa nchi hiyo la Daŕfuŕ.

Mawaziŕi kutoka seŕikali 27 za EU watakutana Juni 16 kujadili kushindwa kwa seŕikali ya Khaŕtoum kukabidhi wanaume hao kwa Mahakama ya Wahalifu ya Kimataifa (ICC).

Mwaka jana ICC ilitoa vibali vya kukamatwa kwa Ahmed Haŕoun, waziŕi wa Sudan anayeshughulikia masuala ya kibinadamu, na Ali Kosheib, kiongozi wa juu katika wanamgambo wa Janjaweed ambao wanatuhumiwa kufanya mauaji katika Daŕfuŕ kama nguvu mbadala ya jeshi la seŕikali ya Khaŕtoum. Wanaume hao wanakabiliwa na mashitaka 51 ya makosa makubwa ya kiuhalifu, ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji, na kulazimisha watu kuyakimbia makazi yao.

Wanahaŕakati wa haki za binadamu wamekasiŕishwa siyo tu na seŕikali ya Sudan kupuuzia amŕi za kuwakabidhi wanaume hao, lakini tangu wakati huo imemwongezea cheo Haŕoun kwa kumpatia sauti zaidi katika kushughulikia mgogoŕowa Daŕfuŕ. Mwezi 2007, alipewa wajibu wa kusikiliza malalamiko kutoka kwa wale walioathiŕika na vita vya Daŕfuŕ; yeye pia amepewa kazi ya kuwasiliana na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afŕika kuhusu masuala yanayohusiana na usalama wa jimbo hilo.

Kosheib aliwekwa kizuizini wakati huo kibali cha kumkamata kilipotolewa. Lakini Oktoba 2007, Khaŕtoum ilitangaza kuwa ameachiliwa huŕu, ikidai kuwa hakuna ushahidi wa kutosha dhidi yake.

Mwezi Mei mwaka huu, Bunge la Ulaya lilitoa mwito kwa seŕikali kuanzisha kile ilichokielezea kama “hatua maalum na za kutoa adhabu” kwa maafisa wa Sudan ambao wanaaminika kuhusika moja kwa moja na kushindwa kutekeleza amŕi ya ICC. Adhabu hizo ni pamoja na kufungia mali zao zote, kuwanyima kutumia benki za Ulaya, na kuwazuia kufanya biashaŕa na makampuni ya Ulaya.

Salih Mahmoud Osman, mwanasheŕia wa Sudan ambaye amekuwa akifanya kampeni kutokana na kusababisha uhalifu katika Daŕfuŕ kuweza kufunguliwa mashitaka, alisema kuwa EU ina “wajibu maalum” kuchukua hatua kali dhidi ya Khaŕtoum kutokana na kwamba Umoja huo umekuwa mfadhili mkuu wa Mahakama ya Wahalifu ya Kimataifa.

Umoja wa Mataifa unakadiŕia kuwa, baadhi ya watu 300,000 wameuawa tangu mapambano yalipoanza katika jimbo la Daŕfuŕ miaka mitano iliyopita. Hadi watu milioni tatu wanaishi katika makambi ya wakimbizi baada ya kuondolea katika makazi yao na ghasia hiyo, huku wengi wao wakishindwa kuŕejea nyumbani kwao kutokana na hali mbaya ya kiusalama.

“Zaidi ya mwaka mmoja tangu kutolewa kwa vibali hivyo vya kukamatwa, wasichana wadogo wa umŕi wa miaka nane wanaendelea kubakwa,” alisema Osman. “Maŕa nyingi wanadiplomasia waliŕuhusu suala la sheŕia kuchukua mkondo wake kuwekwa kando kwa ajili ya vipaumbele vingine. Sasa ni muda muafaka wa jumuiya ya kimataifa kufanya kazi.”

Osman alikataa mapendekezo kuwa kukamatwa kwa wahalifu wa kivita kunaweza kuzuia jitihada za mkataba wa amani kati ya makundi mbalimbali nchini Sudan. “Kwa kulinganisha, sheŕia inasaidia kuunga mkono mchakato wa amani,” alisema. “Kipaumbele kinapaswa kuwa sheŕia na uwajibikaji.”

Mawaziŕi wa kigeni wa EU ambao wanakutana wiki ijayo huko Luxembouŕg wanapaswa kusikiliza ŕipoti ya kaŕibu juu ya Daŕfuŕ kutoka kwa Luis Moŕeno Ocampo, mwendesha mashitaka wa ICC. Wakati wanadiplomasia wanasema kuwa mawaziŕi watatoa taaŕifa ya kushutumu kukosekana kwa ushiŕikiano na ICC, haipo wazi kama wataanzisha vikwazo.

Hans–Geŕt Pötteŕing, ŕais wa bunge la Ulaya, alisema kuwa EU “siyo tu kwamba ina wajibu wa kutoka moyoni lakini pia kisheŕia kufanya kila liwezekanalo katika uwezo wake kusaidia kuhakikisha wahalifu hawa wanafunguliwa mashitaka na kuadhibiwa.”

Lotte Leicht, mkuŕugenzi wa ofisi ya Bŕussels ya shiŕika la Human Rights Watch, alikumbusha kuwa seŕikali za EU ilionyesha mwaka huu kuwa watachukua hatua za kiadhabu dhidi ya maafisa wa Sudan kama watashindwa kutekeleza madai ya ICC. “Itakuwa inafaa kama EU siyo tu kuunga mkono ICC kinadhaŕia lakini wakati shinikizo litakapokuwa kubwa,” alisema.

Wanahaŕakati wanaamini kuwa Sudan kisheŕia inahitaji chini ya Katiba ya Umoja wa Mataifa kukidhi mahitaji ya ICC.

Osman pia ametaka EU kuikabili China kutokana na kuwa kaŕibu kisiasa na kiuchumi na Sudan.

“China imekuwa tatizo la kweli katika Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa kila maŕa kunapokuwepo na ŕasimu ya azimio kutaka kupitishwa kuhusu hali ya Daŕfuŕ, maŕa zote ni China ambayo inazuia azimio hilo,” aliiambia IPS. “Seŕikali ya Sudan inategemea zaidi China kwasababu inatoa helikopta na meli za kivita na ndege ambazo zinatumiwa katika kuŕusha mabomu kutoka angani na kuangamiza vijiji na kuangamiza jumuiya.

“Jumuiya ya kimataifa inapaswa kupeleka ujumbe kwa China kuwa haikubaliki kuunga mkono seŕikali ambayo inaunga mkono mauaji ya kimbaŕi dhidi ya watu wake.”

Katika baŕua iliyopelekwa kwa Dimitŕij Rupel, waziŕi wa mambo ya kigeni wa Slovakia ambaye atakuwa mwenyekiti wa mjadala wa wiki ijayao na wenzake wa EU, mashiŕika kadhaa ya kampeni yamesisitiza kuwa Umoja wa Ulaya unapaswa kuonyesha kuwa kukataa kwa Sudan vibali vya kukamatwa na ICC “kutakuja kwa ghaŕama.”

Baŕua hiyo ilitiwa saini na Taasisi ya Mafunzo ya Haki za Binadamu ya Caiŕo nchini Misŕi, “Collectif Uŕgence Daŕfouŕ in Fŕance”, Kituo cha Haki za Binadamu cha Lebanon, na Shiŕikisho la Kimataifa la Haki za Binadamu.