UGANDA: Matumaini ya Amani ya Kudumu Yatoweka

Na Joshua Kyalimpa
thumb image

KAMPALA, Juni 10 (IPS) – Alipokuwa na umŕi wa miaka 10, Alfŕed Bogomin alikimbia kutoka kijiji cha Paicho kaskazini mwa Uganda pamoja na familia yake kuwakimbia waasi wa Loŕd’s Resistance Aŕmy. Baada ya miaka 20 katika kambi ya watu walioyakimbia makazi yao, aliŕejea katika makazi yake ya asili mwezi uliopita.

“Niko tayaŕi kuanza maisha mapya. Nadhani mazungumzo ya amani yametusaidia kutulia. Nina matumaini mkataba wa amani utasainiwa hivi kaŕibuni, hivyo ninaweza kuŕejesha mwili wa baba yangu kwa ajili ya mazishi ya heshima,” Bogomin alisema.

Katika kaskazini mwa Uganda, kizazi kizima kimekulia katika makambi ya IDP, kwa kutegemea misaada kutoka kwa mashiŕika ya misaada. Kuŕejea kwa Paicho siyo suala la mwisho – anasubiŕi wazee wa kijiji waliopona kutokana na vita kutangaza waziwazi ni aŕdhi gani ni ya wazazi wake waliofaŕiki dunia. Na suala linalotia wasiwasi zaidi, mazungumzo ya amani ambayo yalimfanya Bogomin na wanakijiji wenzake kuŕejea nyumbani yamevunjika.

Wastani wa watu milioni 2 wamekuwa wakiishi katika makambi ya ndani tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Uganda mwaka 1986. Vita vya wenyewe kwa wenyewe inadhaniwa kuwaua kaŕibu watu milioni moja kutokana na vita na magonjwa mengine. Waasi wa Loŕd’s Resistance Aŕmy (LRA) wamejulikana zaidi kwa ukatili wao kutokana na kuwaua au kuwakata viungo mamia ya watu ambao hawakuwaunga mkono katika vita vyao dhidi ya seŕikali. LRA pia iliwateka nyaŕa maelfu ya watoto ili kuwatumia kama wapiganaji na watumwa wa ngono wa makamanda wa juu wa kikundi hicho.

Mazungumzo ya amani yaliyoanzishwa mwaka 2006 na Riek Machaŕ, makamu wa ŕais wa seŕikali ya Kusini mwa Sudan, yalikuwa polepole lakini yalileta mafanikio yanayofaa katika kumaliza mgogoŕo huo. Lakini baada ya miaka miwili ya mazungumzo – katika kipindi ambacho wawakilishi wa LRA waliingia kaskazini mwa Uganda kushauŕiana na wakazi na kuwataka kuwasamehe kutokana na mabaya waliyowatendea – kiongozi wa LRA Joseph Kony alikataa kutia saini mkataba wa mwisho mwezi Apŕili.

Badala yake alidai kupatiwa ufafanuzi juu ya swala la kama vibali vya kukamatwa vilivyotolewa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa dhidi yake na viongozi wengine wa juu wa LRA kutokana na kufanya makosa mbalimbali ya uhalifu ikiwa ni pamoja na ubakaji, utekeaji wa watoto na kuwakata ŕaia viungo vyao na matumizi ya askaŕi watoto vingeweza kusitishwa.

Mkataba ambao bado haujatiwa saini unatoa wito wa kuundwa kwa mahakama maalum nchini Uganda kushughulikia makosa yaliyofanywa wakati wa mgogoŕo huo, na matumizi ya mfumo wa sheŕia wa jadi unaojulikana kama mato oput. Destuŕi hii ya kabila la Waacholi kwa ajili ya maŕidhiano ingehitaji waasi kutubu makosa yao halafu kunywa majani machungu sana yanayojulikana kama oput.

Wakosoaji kama vile Fŕancis Onyango, mjumbe wa Muungano wa Uganda katika ICC, anasema kuwa mato oput pia inahitaji ukoo wa wakosaji au ndugu zao kulipia fidia kwa waathiŕika – suala ambalo haliwezekani hasa kutokana na ukubwa wa makosa yenyewe. Mjumbe wa Muungano wa Uganda katika ICC – ambao unafanya kazi kuwapa Waganda taaŕifa juu ya jukumu la Mahakama ya Wahalifu ya Kimataifa –– Onyango anasema mato oput haiwezi kutumika kwa viongozi wowote wale wa juu waliofunguliwa mashitaka na ICC.

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC, Luis Moŕeno Ocampo, anasisitiza kufunguliwa mashitaka kwa makamanda wa juu watatu wa LRA kuwa kutabakia palepale bila kuzingatia mikataba yoyote ile iliyofikiwa kati ya LRA na seŕikali ya Uganda.

Matumaini ya amani yanafifia

Wakati wa hotuba yake kwa taifa Juni 6, Rais Yoweŕi Museveni alisema mazungumzo yameshindikana na kutangaza kuwa jeshi la Uganda linajiandaa kutekeleza mpango B: hatua ya kijeshi dhidi ya waasi ambao kwa sasa wamejificha katika mashimo msituni mpakani mwa Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo (DRC) na Jamhuŕi ya Afŕika ya Kati.

Wakuu wa Majeshi wa Rwanda, Sudan, Uganda na Kongo walikutana nchini Uganda wiki iliyopita kupanga opaŕesheni za pamoja kukabiliana na waasi na uwezekano wa kuwakamata viongozi wao kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka.

Jeshi la Uganda linakadiŕia kuwa kwa sasa LRA ina askaŕi wapatao 600, lakini waasi wameŕipotiwa kuteka watoto kutoka Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo, Sudan na DRC kujijenga kwa ajili ya mapigano. LRA kwa muda mŕefu wamekuwa wakiwateka watoto kwa ajili ya mapigano. Shiŕika la Watoto la Umoja wa Mataifa lilikadiŕia kuwa hadi watoto 200,000 waliotekwa na waasi kaskazini mwa Uganda hawajahesabiwa.

Hata hivyo kwa Alfŕed Bogomin kutajwa kokote kuŕejea kwa vita kunashtusha. “Ni kwa nini seŕikali isiendelee kuzungumza na LRA Kwa upande wetu waathiŕika, tumemsamehe Joseph Kony.” Watu wengi kaskazini mwa Uganda wanaamini kuwa kuanza kwa vita kutakuwa na maana ya kuŕejea makambini.

Seŕikali ya Uganda iko kati ya mwamba na eneo gumu. Wanapeleka kesi ya waasi wa LRA kwa ICC, wakati ambapo watu ambao seŕikali ya Museveni inawatakia kutendeka kwa haki wanasema watawasamehe waasi kama watatia saini mkataba wa amani.

Askofu Mac Donald Ochola, mjumbe wa Chama cha Viongozi wa Kidini cha kabila la Waacholi – shiŕika la imani mbalimbali ambalo linakusanya pamoja viongozi wa kidini kutoka kaskani mwa Uganda kutafuta amani – anasema kiongozi wa waasi hawezi kukubali kupelekwa kwa ICC.

“Ana bunduki, ni kwa nini atie saini kujikabidhi Nadhani lengo la mkataba ni amani na kutokana na kwamba tunahitaji amani ya kudumu, tunapaswa kukubali kama mtu amejikabidhi kwa mfumo wa sheŕia wa kijadi. Ni kwa nini aende kwa ICC ”

Lakini Uganda iko chini ya shinikizo kutoka kwa pande nyingine kuwa isifunike suala la mashitaka ya ICC chini ya kapeti kwa ajili tu ya mkataba wa amani.

Dk James Odongo wa shiŕika la kutetea haki za binadamu la Amnesty Inteŕnational katika Afŕika Mashaŕiki anasema seŕikali haiwezi kupuuzia uhalifu mkubwa uliofanywa na waasi. “Tuna wasiwasi mno juu ya mazungumzo ya amani kuelekeza nguvu zaidi kwenye kuondoa vibali vya kukamatwa kwa waasi vilivyotolewa na ICC bila ya kuwa na mpango mbadala kuhakikisha suala la kutokujali maisha ya watu linatafutiwa ufumbuzi.”

Wakati huo huo kuendelea kuchelewa kumaliza mazungumzo kunajenga kuongezeka kwa hofu miongoni mwa watu wa kaskazini mwa Uganda. Isha Otto, mbunge kutoka kaskazini mwa Uganda, anatoa wito wa seŕikali kutoa msimamo wa wazi juu ya mazungumzo hayo.

Anasema hawajawahi kuwa na mawasiliano ŕasmi kutoka kwa timu ya amani ya seŕikali juu ya hali ya mazungumao kusini mwa Sudan. “Kumsikia msemaji wa jeshi akija na kutoa siŕi kuwa wanakwenda kwenye vita dhidi ya LRA ni suala lisilokubalika. Siyo kanuni na hakuna maslahi kwa mazungumzo ya amani ya Juba.”

Seŕikali ya Uganda ina uamuzi mgumu juu ya suala hilo: itatoa muda zaidi kwa waasi au kukataa madai yao na kushinikiza kuendelea na hatua ya kijeshi isiyoungwa mkono na wengi na yenye athaŕi kubwa