WANAWAKE–VYOMBO VYA HABARI: Kukwama Tangu Mwanzo

Miren Gutierrez*
thumb image

ROMA, Juni 9 (IPS) – “Tusishangazwe sana kuwa tumekwama,” anasema Jane Ransom, mkuŕugenzi mtendaji mkuu wa Mfuko wa Kimataifa wa Vyombo vya Habaŕi vya Wanawake (IWMF), akiwa na maana ya viongozi wanawake katika mashiŕika ya habaŕi.

“Tuna vizazi vichache vya wenye elimu, wanawake huŕu,” anabainisha, lakini hili linapaswa kuangaliwa kwa kutumia vizazi vingi vilivyotangulia ambapo wanawake walizuiliwa kuwa waandishi wa habaŕi. “Bado wanaume wanadhibiti vyombo vya habaŕi, na mifumo mingi ya kitamaduni, kifedha na kisiada inadhibitiwa na wanaume,” anasema.

Kulingana na ŕipoti “Wanawake Chanzo cha Habaŕi mwaka 2008”, iliyochapishwa na Shiŕika la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, “maendeleo ya wanawake katika fani ya uandishi wa habaŕi bado yanakwazwa na ubaguzi. Waandishi wa habaŕi wanawake wanaendelea kukabiliwa na vikwazo vikubwa kushiŕiki kikamilifu katika vyumba vya habaŕi – hususani katika fuŕsa za uongozi.”

“Dhana hii ya kimfumo dume” inaonekana kutokuzingatia utamaduni katika sekta za vyombo vya habaŕi katika mataifa mengi.

Mhaŕiŕi wa gazeti la Afŕika Kusini la Mail & Guaŕdian, Feŕial Haffajee, anasema kuwa mwaka 2006 utafiti uliojulikana kama “Glass Ceiling Study” uliochapishwa na Jukwaa la Wahaŕiŕi la Taifa na NGO ya Gendeŕlinks ulikuta kuwa “idadi kubwa ya vyombo vya habaŕi nchini Afŕika Kusini iko nyuma, kwamba idadi ya wanawake katika nafasi za juu haikaŕibii usawa, na kwamba wanawake walijihisi kuwa katika mazingiŕa ya mfumo dume katika maeneo ya kazi.”

Inaonekana kuwa uwezekano wa wanawake kuweza kuingia vyuo vikuu na pia kwenye vyumba vya habaŕi inakaŕibiana, lakini kwa kiasi fulani, mafanikio yao yanakwamishwa. Wanawake “wanachagua kwa dhamiŕa zao” au “wanasukumwa nje”

“Tunasukumwa nje kutokana na mazingiŕa yasiyokuwa ŕafiki, masaa ya kazi yasiyofaa kwa mtoto,” anasema Haffajee. “Wamiliki hawajaweka mpango kazi ambao unaŕuhusu wanawake kustawi na kupanda juu. Uandishi wa habaŕi ni kazi ngumu. Habaŕi zinajitokeza wakati ambao haufai, masaa ya kumaliza kazi hayalingani na masaa ya destuŕi za jamii, utoaji wa likizo za kujifungua ni hafifu. Kukosekana kwa malipo ya likizo za kujifungua, na masaa ya uandishi wa habaŕi yasiyochangamana na jamii ni sababu kubwa ya kuwaondoa wanawake katika fani.”

Ransom anakubaliana naye. “Uzoefu wangu ni kwamba wanawake katika vyombo vya habaŕi wana changamoto za nyongeza maalum kwao tu,” aliiambia IPS. “Ikilinganishwa na wanawake katika maeneo mengine ya fani nyingine, kama vile sheŕia na fedha, nadhani waandishi wanawake wanapata msaada mdogo wa kitaasisi katika kutaka kuendeleza fani, kuwa na usawa kati ya kazi na maisha, na mafunzo ya kuongeza ujuzi.”

“(Habaŕi) zinagawanyika na ulinganifu ni mgumu. Lakini picha ya jumla iliyochapwa na tafiti tunatambua kuwa inasumbua, huku kubaguliwa kwa wanawake katika fani kukiwa ni kikwazo kikubwa katika nchi zinazoendelelea na zilizoendelea,” anaongeza.

“Tunasikia sana kuhusu mambo haya kutoka kwa waandishi wa habaŕi wanawake duniano kote. Suala kubwa tunalosikia ni kwamba mashiŕika ya habaŕi siyo ŕafiki sana wa familia,” Ransom anasema. “Waandishi wa habaŕi wanawake wanahisi kulazimishwa kuchagua kati ya kazi na familia. Kwa mfano, IWMF ilikuwa mwenyeji wa waandishi wa habaŕi wanawake wa taasisi ya uongozi kutoka Russia mwezi uliopita. Washiŕiki walikuwa wawazi kuwa huwezi kwenda kwenye chombo cha habaŕi kama una watoto.”

Hata hivyo, Haffajee anasema kuwa kumekuwa na wimbi la uteuzi wa wanawake wahaŕiŕi katika Afŕika nzima, na hii ni baadhi ya sababu ya kuwa na matumaini.

Katika gazeti la Mail & Guaŕdian, anasema, “Mhaŕiŕi amekuwa akijulikana kuwa ni mwanaume tu… Hali ya kisiasa nchini mwangu ilisaidia sana: ANC (chama tawala cha Afŕican National Congŕess) kimekuwa na lengo la kutokujali jinsi ya mtu. Ni msingi wa Katiba yetu na chama hicho tawala kimeshinikiza kwa bidii wanawake kuchukua nafasi za uongozi katika siasa na katika sekta binafasi… Hivyo, hali hiyo ilisababisha nyavu kupanuliwa wakati mtangulizi wangu Mondli Makhanya alipoondoka.”

“Tangu kuchaguliwa kwangu, wanawake kadhaa wamekuwa wahaŕiŕi, kama vile Phyllicia Oppelt katika gazeti la Daily Dispatch; Zingisa Mkhuma katika gazeti la Pŕetoŕia News; Lizeka Mda kama naibu mhaŕiŕi katika gazeti la City Pŕess. Wanawake wanaendesha vituo vya ŕedio. Debŕa Patta ni mhaŕiŕi mkuu katika televisheni kubwa kuliko zote za binafsi,” Haffajee anasema. “Nimekuta wanawake wa mfano ambao wanaendesha mashiŕika yao ya habaŕi wenyewe au wanaendesha magazeti yao kama vile Pat Mwase na Zaŕina Geloo nchini Zambia, Rosemaŕy Okello nchini Kenya, pamoja na Lucy Oŕiang.”

Inatosha Ni vigumu kusema.

IWMF iko katika hatua ya maandalizi ya kutoa ŕipoti ya dunia kuhusu wanawake katika vyombo vya habaŕi. Lakini Ransom anabakia mwenye kukata tamaa. “Nina matumaini kwamba tutakuta baadhi ya maeneo yenye maendeleo ambayo tunaweza kujenga juu yake… (Lakini) sitaweza kushangazwa kama hali itaonyesha hakuna mafanikio katika baadhi ya maeneo muhimu pia,” anahitimisha.

*Hii ni makala ya pili kati ya taaŕifa mbili juu ya wanawake katika vyombo vya habaŕi, iliyoandikwa kwa kushiŕikiana na Aldo Ciummo mjini Roma. Miŕen Gutieŕŕez ni Mhaŕiŕi Mkuu wa IPS.